Uongozi na aAfanyakazi wa Paradise All suites hotel kwa kushirikiana na Angella Bondo Show (kipindi kilichopewa msukumo na kipindi cha Oprah Winfrey) wanawakaribisha katika “Christmas brunch” (mlo ujumuisho asubuhi na mchana) itakayofanyika Jumamosi tarehe 18,Desema 2010.

Meneja Mgahawa wa Hoteli hiyo iliyo chini ya umiliki mpya, Bw. Anold Lema amesema kuwa siku hiyo itakuwa mahsusi ya kuwafurahisha tuwapendao hivyo ni siku itakayokuwa na mambo mbalimbali ikiwemo michezo kati ya kina mama, kina dada, marafiki na binti zao. Michezo hii itawasaidia kina mama hawa kutumia muda huo kukaa na kufurahi na wale wawapendao katika msimu huu wa sikukuu.

Tiketi za kiingilio tayari zimeanza kuuzwa sehemu mbali mbali jijini, hoteli ya Paradise iliyopo katika jingo la Benjamin Mkapa katikati ya jiji na Chicken Hut Mlimani City. Tunawakaribisha wote kujumuika nasi katika sherehe hii.

Ticketi zinauzwa Tsh 30,000 kwa mtu mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...