Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), ameondoka nchini leo tarehe 30 Desemba 2010 kwenda Brazil kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe za kumwapisha, Rais Mteule wa Brazil, Bibi Dilma Rousseff zitakazofanyika mjini Brasilia tarehe 1 Januari 2011.

Wakati wa sherehe hizo, Mhe. Membe atawasilisha salaam maalum kwa Mhe. Dilma Rousseff kutoka kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete.

Aidha katika ziara hiyo, Mhe. Membe atapata fursa ya kufuatilia makubaliano mbalimbali ya ushirikiano yaliyofikiwa baina ya Tanzania na Serikali ya Brazil wakati wa ziara yake aliyoifanya nchini humo mwezi Septemba, 2010.

Makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara hiyo ni pamoja na Brazil kuisaidia Tanzania katika sekta ya kilimo, kuendeleza mradi wa kufua umeme katika Bonde la Mto Rufiji (Stigler’s Gorge), uzalishaji nishati mbadala ya umeme kwa kutumia mimea, miundombinu viwanda na biashara.

Mhe. Membe atarejea nchini tarehe 3 Januari, 2011.

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 DESEMBA 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...