Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Adoral Mapunda akimkaribisha Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda (MB) chumba namba 60 Jengo Jipya la Wagonjwa wa Nje.Katikati Prof. Victor Mwafongo Bingwa wa Magonjwa ya Dharura akitfafanua jambo kwa Mh. Waziri juu ya huduma bora zinazotolewa na Idara ya Magonjwa ya Dharura. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Makwaia Makani
Daktari Bingwa wa Watoto Dkt. Masawe akimweleza changamoto Waziri wa Afya zinazopelekea vifo visivyo vya lazima kwa akina mama na watoto katika wodi mojawapo ya Jengo la WazaziDaktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Dkt.Joseph Kissanga akitoa taarifa kwa
Mh. Waziri wa Afya juu ya huduma ya uchunguzi na tiba ya figo.
Prof. Victor Mwafongo Bingwa wa Magonjwa ya Dharura akifafanua jambo kwa Mh. Waziri juu ya huduma bora zinazotolewa na Idara ya Magonjwa ya Dharura.
Mh. Waziri wa Afya Dkt. Hadji Hussein Mponda akizungumza na wanahabari juu ya ziara yake Hospitali ya Taifa Muhimbili. Picha zote na mdau Aminiel Aligaesha wa Muhimbili



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Accident and Emergency (A&E)ndo sawa na Magonjwa Ya Dharula?

    ReplyDelete
  2. wadau naomba msaada,anaposema daktari bingwa anamaanisha nini,ni cheo ama alishindana akashinda sijaelewa..

    ReplyDelete
  3. daktari bingwa tunaelewa lakini hilo la " magonjwa ya dharula" ni kiboko!!! nisaidieni sielewi kiswahili au ndio kiswahili kinakuwa siku hizi?

    ReplyDelete
  4. bingwa ni yule alieshinda! umesomea udaktari kwa ujumla....halafu uka-amua kuisomea, kuijua, na kufanya utafiti na tiba katika pua na koo tu,au figo au ngozi tu! hapo wewe ndio bingwa....huwezi kuwa sawa na Daktari mwingine wa kawaida.Yaani wewe ni BINGWA katika eneo hilo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...