Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Haji Mponda, akizindua Atlasi ya afya ya upatikanaji wa huduma za afya katika mkoa wa mbeya, iliyochapishwa na Mpango wa pamoja wa Tanzania na Ujerumani(TGPSH).Atlasi hiyo ya kwanza inatoa maelezo ya kina ambayo itawawezesha watunga sera za afya,kuona udhaifu na kushughulikia kwa kuchukua hatua maalum.
Waziri Dkt. Haji Mponda akionyesha atlasi hiyo kwa watu waliohudhuria uzinduzi huo.Atlasi hiyo inatoa maelezo kwa picha na ramani ambayo inaweza kutumiwa na watu wengi katika kuchangia kuleta maendeleo zaidi katika uwanja wa mifumo ya habari

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...