Mabaki ya coaster ya 'Another G' baada ya ajali hiyo
Sehemu ya mbele ya lori likiwa mtaroni
Lori lililohusika na ajali hiyo likiwa katika mtaro

Habari na Picha na Francis Godwin
WATU wanne wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 8 kujeruhiwa vibaya baada ya costa yenye namba za usajili T 885 BNQ mali ya Another G ' kugongwa na lori wakati akishusha abiria .

Ajali hiyo mbaya ambayo ni ajali ya kwanza kutokea mkoani Iringa kwa mwaka huu 2011 na ajali ya pili mbaya kutokea nchini ikiwemo ajali ya basi la Sumry kugongana na Lori Mikumi mkoano Morogoro na kusababisha vifo vya watu 8 na kujeruhi 22 imetokea leo majira ya saa 10 jioni katika kijiji cha Tangangozi wilaya ya Iringa vijijini barabara kuu ya Iringa- Mbeya.

Wakielezea juu ya ajali hiyo majeruhi walisema kuwa wakati ajali hiyo inatokea costa hiyo ilikuwa imesimama kando ya barabara eneo hilo kwa ajili ya kushusha abiria na ndipo lori hilo lilipoivaa costa hiyo ubavuni na kuigonga vibaya na kupelekea nusu ya costa hiyo kuchanwa vibaya na lori hilo.

Walisema kuwa katika ajali hiyo abiria watatu wa costa hiyo walikufa papo hapo huku mwananchi mmoja wa aeneo hilo ambaye alikuwa akitembea kwa miguu kugongwa na lori hilo ambalo lilikuwa katika mwenda wa kasi .

Hata hivyo alisema kuwa mwendo kasi wa lori hilo ndio chanzo cha ajali hiyo na kuwa inaonyesha dereva wa lori hilo alikuwa amesinzia na ndio sababu ya kuigonga costa hiyo ambayo ndani ilikuwa na abiria zaidi ya 30 ambao walikuwa wakielekea Njombe.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kikosi cha usalama barabarani limethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kuwa idadi kamili ya waliokufa itafahamika baada ya kufika hospitali ya mkoa wa Iringa alisema mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi ambaye alifika eneo la tukio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Je ni karibu na lilipokuwa kaburi la Marehemu Kiyeyeu? Poleni wafiwa ktk kipindi hiki kigumu kwenu, Mungu awape subira ktk wakati huu
    Mdau Ned

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...