Hasheem Thabeet akiwa katika tizi na timu ya Vijana Basketball 'City Bulls' uwanja wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini Dar, kabla hajapaa kuelekea masomoni Marekani na hatimaye kutinga katika ligi ya NBA akiwa na Memphis Grizzlies. Kujituma na kufanya unachoikipenda kwa moyo wote husaidia sana kukufikisha kwenye malengo yako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani mimi kama Mtanzania nilifarijika sana kuona Hasheem anatinga NBA - Ligi ambayo mamimlioni ya wamerekani wanatamani kuingia ila hawawezi. Kitu ambacho sikielewi na ninaomba msaada wa wadau ni kwamba kwa nini huyu bwana mdogo meneja wake ni Mnigeria? anyways inawezekana ailikuwa mstari wa mbele ku -motivate dogo afike alipo ila kwangu haiingii akilini, si kwamba nalalamika kuwa hiyo chance naitaka mie la hasha , sijawahi hata ku-mmanage mmachinga, naomba jibu wadau

    ReplyDelete
  2. DAH HUYO JAMAA WA MBELE MFUPI KWELI HATA NATE ROBINNSON KAMZIDI LOL

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza, ofcourse wapopo ndo wajanja wa Afrika, nadhani unalijua hilo. Wanajua jinsi ya kukaba, hata ukitema mate wanafukia.lol!

    ReplyDelete
  4. Hii namba imeenda hewani????kah!
    Kamua mwana na try ligi ya nyumbani iwe inatoa ajira kwa namna yoyote uwezayo na itawezekana ukiamua tu!
    Najua unasoma humu,nani hasomi michudhi jamani??

    ReplyDelete
  5. HII SIO TIMU YA VIJANA BASKETBALL (aka CITY BULLS).. HIZI SURA ZOTE NI WACHEZAJI WA "UDSM OUTSIDERS"..
    Kutoka kulia: Dawson (yellow TShirt), Lloyd (aliyeshika kiuno, red shoes), Manase (Blue track trousers) na aliye mbele ya Hasheem ni Albert.. WOTE HAWA NI BAADHI YA WACHEZAJI WA "UDSM OUTSIDERS" NA NDIYO TIMU ALIYOKUWA AKIFANYIA MAZOEZI NA NDIKO ALIKOANZIA KUJIFUNZA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU.. BAADAE VILE VILE ALIKUWA AKICHEZEA TIMU YA SHULE ALIYOKUWA ANASOMA YA MAKONGO SEC SCHOOL.

    HAJAWAHI KUCHEZEA TIMU NYINGINE YOYOTE TANZANIA, ISIPOKUWA HIYO YA SHULE YA MAKONGO NA VILE VILE KUFANYA MAZOEZI KTK UWANJA WA CHUO KIKUU (UDSM) AMBAPO NDIPO PALIKUWA KARIBU NA NYUMBANI KWAO SINZA-MAKABURINI, MIAKA HIYO.. UWANJA HUO WA CHUO HUWA UNATUMIWA NA TIMU YA "UDSM OUTSIDERS".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...