


Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Br. Michuzi,
ReplyDeleteNaomba niwapongeze African Lyon kwa juhudi zao za uhakika. Huu ni mwanzo mzuri na kusema kweli ndio changamoto kubwa wa vilabu vyengine kuiga mfano huu mzuri. Jambo la msingi linalojitokeza hapa ni Uongozi madhubuti pamoja na nguvu ya fedha na uwekezaji katika soka. African Lyon naamini sana kwamba itafika wakati nao watabadilishana jezi na timu ngeni kama hao wageni walivyowapa jezi yao. Aidha hili ni somo kwa vilabu vya Simba n Yanga kwamba watanzania wanataka bidhaa mpya mpya katika soka na si kupambwa katika magazeti na baadae uwanjani hauna burudani huku timu zikisheheni mapro. Kombe la Mapinduzi Zanzibar ni uthibitisho.TFF nayo ina haki ya kupunguza idadi ya wachezaji wa ligi wanaotoka nje ya Tanzania kwani ni vyema wawasaidie hawa viongozi ambao inaonekana dhahiri kwamba hawaelewi wanachofanya. Kujibebesha mizigo ya wachezaji wenye gharama kubwa wasio na tija kwa timu na kuwa chanzo cha mfarakano. Azam,African Lyon na wengineo wajitahidi katika kuleta ushindani wa soka la Tanzania.