Wanafunzi wa Kampala International University (K I U) wakiwa katika mlango wa kuingilia Ikulu Dar es Salaam upande wa Ofisi za Waziri Mkuu baada ya kuandamana jana ili kuishinikiza Serikali ikitambue Chuo hicho ili wapate Mikopo. Hata hivyo hawakufanikwia kuonana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda ambaye hakuwepo ofisiniw huo, na maafisa waliokuwepo waliwataka wachaguane wanafunzi watano waingie kufikisha malalamiko yao. Watano hao walipoingia na kutoka walisema wameambiwa warudi kesho saa tano.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwanini inaitwa KIU na sio TIU.Kutoa mkopo ni kazi.

    ReplyDelete
  2. Hang on! nimetatizwa hapa, naomba muongozo.

    1. Hiki chuo kipo nchini na kina kibali halali cha kutoa elimu kwa kiwango cha university lakini serikali haikitambui?

    2. Wanafunzi wanaosoma hapo hawakujua kama chuo hiki hakitambuliki? je wanajua kwa maana hiyo hata shahada zao hazitatambulika? kwa nini wakajiunga na chuo wakijua hayo?

    ReplyDelete
  3. Kwikwiiii....hahaaaa....mbavu zangu jamani!

    ReplyDelete
  4. Hiki chuo hakistahili na wala hakina sifa kabisa ya kuitwa chuo kikuu, nashangaa hawa wabongo Nyumbani kuna vyuo kibao kama mna vigezo kwanini mlikimbilia huko,na smijisumbue waziri mkuu hawezi fanya lolote

    Mgeenda TCU walau tungewaelewa,,Mgesoma hata Chuo Kikuu Huria shida zote za nini?

    ReplyDelete
  5. Mdau nafikiri hujaelewa unayesema NYUMBANI KUNA VYUO KIBAO KWANINI WANAKIMBILIA HUKO? hiki Chuo Cha Kampala nafikiri kipo Nchini Tanzania kule GONGOLAMBOTO. Tatizo tu sijui kama kimesajiliwa.

    ReplyDelete
  6. Kimeshatoa wahitimu mara ngapi? Je kilianza lini kutoa shahada zake hapa Tanzania?

    ReplyDelete
  7. hiki chuo sio chuo kikuu kinachotambuliwa kimataifa thats why serikali inashindwa kuwasaidia kiliishakuwa hakitambuliwa kwa muda mrefu sasa kwa sababu hakifuati system ya universities na wanafunzi wake weng ni zile four za form six na form four wale wote walioshindwa kuingia vyuo vya kawaida vya bongo ndio wanakimbilia huko ambao hawana qualification za kuingia university wao wanasomba as long a unafedha za kuwalipa sio chuo ni mamluki ni business oriented so big up serikali nyie mlio hapo rudieni mitihani ya form six mjiunge na vyuo vinavyojulikana acheni upuzi wenu ndio maana hamjui hata wapi kwa kwenda kufatilia ili chuo kiwe registered sio kwa waziri mkuu wapuuzi nendeni tcu ndio watambuzi wa vyuo

    ReplyDelete
  8. Wadau hiki chuo kinatambulika na kimasajiliwa Tz kwa taratibu zote. Na pia wanaoponda ni wale wanaofikiria tu kwamba ni wahapa hapa. Wenzetu wameshaona mbali na kuliteka soko la Africa Mashariki mapema. Kipo Uganda tawi Kenya na Tz. Sasa wako kwenye mchakato wa Rwanda na Burundi. Tubadilike jamani
    This is a list of universities in Tanzania.

    Ardhi University, established in 2007[1]
    Hubert Kairuki Memorial University (HKMU), established 1997[2]
    International Medical and Technological University (IMTU), established 1995
    Moshi University College of Cooperative and Business Studies
    Mount Meru University
    Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)
    Muslim University of Morogoro (MUM)
    Mzumbe University (MU)
    Open University of Tanzania (OUT)
    Ruaha University College (RUCO)
    St. Augustine University of Tanzania (SAUT)
    St. John University of Tanzania (SJUT)
    Sokoine University of Agriculture (SUA)
    State University of Zanzibar
    Theophile Kisanji University
    Tumaini University (TU)
    University of Bukoba
    University of Dar es Salaam (UDSM), established in 1970 from the split of the University of East Africa
    University of Dodoma, established in 2007[3]
    Zanzibar University (ZU)
    Kampala International University (KIU) Established in 2008 as a distant learning institution.
    [edit] References

    ReplyDelete
  9. KIU, wasanii. Nilienda kuomba kazi hapo baada ya interview nikaambiwa hapa bwana unoko wako wa UDSM HATUUTAKI SI UNAJUA WANAFUNZI WETU TUNAWALEALEA, HIVYO ADOADO.....
    Nikaamua kuki google nikakuta hata huko kwao Uganda hakitambuliki kihivyo... nikasepa.

    ReplyDelete
  10. HIKI CHUO NI FEKI SANA AISEE YAANI KIPO KIBIASHARA ZAIDI, UKIWA MGENI NASIKIA UNATOZWA DOLARI NA WAZAWA WAO WANATOZWA MADAFU YA KIGANDA. KIUKWELI KILA MWANACHUO ALIEMALIZA HAPO ANALALAMIKA HAJAWAHI KUPEWA ORIGINAL CERTIFICATE....KAAZI KWELIKWELI, KWELI HUKO NYUMBANI NI DAMPO

    ReplyDelete
  11. Mdau wa Thu Jan 06, 08:11:00 AM amepotosha ukweli. KIU haijasajiliwa Tanzania. Imesajiliwa Uganda tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...