Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka mkoani Dodoma,ilaripoti kwamba,waadhili na wafanyakazi wa chuo kikuu cha UDOM,wamegoma kuingia kazini leo na kuushinikiza uongozi wa chuo hicho chini ya Prof. Mlacha na Prof. Kihula,ili wapatiwe ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo:-
- kwa nini mishahara yao inayotoka wizarani haiwafikii kama wizara ilivyopanga??
- je asilimia hiyo iliyokuwa ikipotea ilikuwa inaenda wapi na kwanini??
- kwa nini mpaka sasa hawajalipwa malimbikizo yao ya pesa walizosimamia field??
Pia Wanafunzi wa kitivo cha elimu cha Ng'ong'ona nao asubuhi ya leo waliandamana wakitaka kurudishiwa pesa zao za malazi baada ya chuo kufupisha muda wa kuishi chuoni hapo kwa semista hii ya kwanza.
Wanafuunzi hao walitawanyishwa kwa mabomu ya machozi,mijeredi na maji a kuwasha kutoka kwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi chake cha kutuliza ghasia,mpaka sasa wapo mbioni wakihofia usalama wao
hali ya mazingira kwa upande wa ualimu sio shwari sana sababu polisi bado wametanda,kila kona ya mlima wa kitivo cha elimu.
Ripota wa Globu ya Jamii yupo katika eneo hilo la tukio na sasa anatutaarifu kwamba wakuu wote wa chuo wameingia katika mkutano wa dharula na atatufahamisha zaidi yale yoote yaliyojiri katika kikao hicho hapo baadae kitakapomalizika kikao hicho,hivyo tuvute subira kidogo.
hapa ndo tumefika after 50 yrs
ReplyDeleteKabla ya kuripoti ni muhimu mkasoma mfumo wa utawala wa chuo....msikariri, UDOM haina mfumo wa vitivo, orgazization structure yake ni CHUO KIKUU (UDOM), VYUO (viko 6 kikiwemo elimu) skuli (ziko ndani ya VYUO na Idara ziko ndani ya skuli...hata hivyo nawapongeza sana kwa kutuhabarisha wananchi
ReplyDeletemambo haya mpaka lini jamani??
ReplyDeletesafi
ReplyDeleteCHUO CHENYEWE KIMEFUNGULIWA JUZI TU,TAYARI MATATIZO YAMEANZA,UKIFUATILIA UTAKUTA LAZIMA KUNA UBADHIRIFU HASA UKISABABISHWA NA UONGOZI,JAMANI MAMBO HAYA TANZANIA HADI LINI ???NDIYO MAANA WATANZANIA WENGI HUAMUA KUKIMBIA NCHI BADALA YA KUWA TUKILALAMIKA NA HAKUNA SOLUTION,
ReplyDeleteMTOA MAONI,KAMPALA,UG.
KULINGANA NA MAELEZO YA VIONGOZI WAKUU WA UDOM,SIONI KAMA KULIKUA NA SABAB YA MSINGI YA KUANDAMANA.INAVYONEKANA KUNA SHINIKIZO LA KISIASA KUTOKA KWA WANASIASA.LENGO KUBWA IKIWA NI KUICHAFUA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI.WATANZANIA JAMANI TUJIFUNZE PIA NA KUONA JITIHADA ZA RAISI WETU.CHUKI ZA KISIASA ZIKOMESHWE TUSIENDESHWE NA MATUKIO.NA CHUKI ZISIZOKWISHA.TUIJENGE NCHI YETU CHANGA KWA PAMOJA.
ReplyDeleteANAESEMA HAKUKUWA NA SABABU YA KUANDAMANA HAIJUWI UDOMU TATIZO LA UDOM NI MLACHA KAMA YY NDIYE ANAE TUMIKA KISIASA BASI ACHUNGUZWE
ReplyDeleteHIVI WEWE UNAEKUBALIANA NA WALIOYASEMA UONGOZI WA CHUO NA KUWAONA WAFANYAKAZI WA UDOM WAJINGA UNATUMIA AKILI AU MAKAMASI??? ULITEGEMEA WAKUBALI DAT WAMEBORONGA??? ILI IWEJE???? SIASA ZIMEINGIAJE HAPO ILIHALI NI CHUO CHENU MAFISADI??? NA WASIWASI UTAKUA UNAUNGANA NA HAO WAJINGA WENZAKO WA UDOM KUSABABISHA FUJO ZISIZOKUWA ZA LAZMA KWA KUWAIBIA HOA WAFANYAKAZI WA UDOM. NINAKUSHAURI FUATILIA HILO SWALA KWA UMAKINI NA UTAJUE UKWELI SIO KUKURUPUKA KAMA KIHIYO..................
ReplyDelete