Nimekua nikifanya utafiti sasa kwa miaka kumi juu ya vyombo vya usafirishaji katika miji yetu mbali mbali Tanzania. Nimefanya utafiti huu kwa kuzingatia malalamiko yanayotolewa na abiria,kufuatiliakwa ukaribu utoaji wa Laisensi kwa ajili ya kufanya biashara ya usafirishaji wa abiria pia kwa kuzingatia swali muhimu la kwa nini kumekua na Mabasi madogo madogo mengi maarufu kwa jina la vipanya kuongezeka kila siku katika miji yetu hasa Jijini Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na mikoa mingine.

Serikari yetu hasa katika sekta inayo husika na swala zima la usafirishaji imekua inalegeza sana masharti yake ya itoaji wa leseni, hii imesababisha kua kila mfanya biashara anaejisikia kumiliki vyombo hivi vya biashara ya usafirishaji kufanya hivyo, ongezeko hili limekua si kero tuu kwa abiria lakin pia limekua kero kwa serikari yenyewe ambapo sasa wanashindwa kabisa hata kuvisimamia kwa ukaribu. Mfano mzuri kumekuwa na tatizo la vibaka katika vituo mbali mbali vya mabasi ambao maarufu kwa jina la wapiga debe.

Inaonesha kuwa vyombo hivi vya usafiri wa mjini vingi vinamilikiwa na washika barabara wenyewe ambao ni wafanyakazi ndani ya sekta hiyo data zinaonesha kua kila mji asilimia zaidi ya 40% ya vyombo vyote hivyo vinamilikiwa na wao,si vibaya ni biashara lakin kibaya zaidi ni kua hata mapato hawalipiii kutokana na kujuana.

Katika mkoa wa Mbeya paka mwaka 1999 kulikua na vyombo vichache sana vya usafirishaji mjin lakini muda ulipo zidi kwenda miaka ya karibuni ambapo Serikari ya jamuhuri ya muungano ilitangaza kua hakuna kuwa tena vipanya kati kati ya jiji yani kuelekea Posta, hii iliathiri sana ambapo ilifanya wafanya biashara wengi wa Vipanya kuhamishia biashara zao mikoani na Mbeya iliathirika kabisa na kusababisha biashara ya Costa ambazo zilikua zikifanya biashara za kusafirisha abiria kufa kabisa, hii haikuwaathiri abiria na wamiliki wa mabasi hayo makubwa lakin pia iliathiri taifa kwa ujumla kwa ongezeko la ajali kutoka asilimia chache miaka ya 1999 paka kua asilimia mala dufu paka kufikia 2010

Tatizo hili la vyombo vya usafirishaji kuongezeka halijaathiri wananchi ambo wanategemea vyombo hivyo tuu, lakin pia limeathiri kwa kiasi kikubwa ongezeko la msongamano wa magari katika miji mbali mbali hasa Jijini Dar es salaam, Dodoma, Arusha na kwa sasa Jijini Mbeya.

Msongamano huu pia umesababisha mambo baadhi kujitokeza la kwanza kumekua na ongezeko la omba omba katika Jiji la Dar es salaam kwa kuchukua upenyo huo wakati magari yanangoja foleni basi wanakua wanaomba omba. Sasa maeneo yote ya jiji Omba Omba wamekua kwa asilimia kubwa na kero.

Pili katika tatizo la foleni imesababisha ongezeko la wafanya biashara wadogo wadogo kuuza bizaa zao mbali mbali kama Ice Cream, maji ya kopo pia hata yale ya plastic,pipi biscuit na hata mahindi,mayai na vingine vingi.

Hii imeonesha kua wafanya biashara hawa wameongeza kasi kubwa la uchafuzi wa jiji na mazingira kwa ujumla kwa sababu mteja akila kitu chochote hana pa kutupia taka zake hivyo atatupia nje ya Gari kutokana na kuwa katika vyombo hivyo vya usafiri hakuna vifaa maalum kwa jili ya kuhifadhia taka kukusekana.

Sababu ya tatu ni kwamba vyombo ongezeko hili na kuwa na foleni kumeleta vibaka wengi ndani na nje ya jiji,mala magari yasimamapo yanawapa upenyo vibaka kuwaibia watu ammbao hawana hata hatia.

Pia sasa imeonekana mida ya asubuhi watu wanapo enda kazini na jioni wanaporudi kutoka maofisini kunakua na msongamano ambapo hata traffic light zetu zinakua hazina kazi na kulazimisha wana usalama wa barabarani kusimamia jambo hilo swala ambalo ni hatari na linasababisha ajari nyingi hasa maeneo ya Morocco, Ubungo, na Mwenge.

Na mwisho msongamano wa vyombo vya usafiri vimesababisha watu wengi kulazimika kuamka asubuhi na mapema si kwa kupenda lakin ni kwa sababu hawana jinsi inabidi wawahi folen hili tatizo si kwa Jiji la Dar es salaam tuu hata miji mingine nchini limekua ni tatizo sana.

Nini basi kifanyike ili kupunguza tatizo hili la msongamano wa vyombo hivi vya usafirishaji?

Naishauri serikari hasa katika hii sekta wanayo husika na usafirishaji wa abiria watazame tena muundo wao kwa ukaribu. Na pia kuwe na idadi ya magari maarumu ya biashara hii na kuondoa kabisa hivi vipanya maana havikuundwa kwa nia ya kuwa kibiashara lakin viliundwa kwa nia ya kuwa vyombo vya kusafiria wanafamilia na pia kwa wateja maeneo ya hotelini na sehemu kama hizo.

Kwa kuzingatia hili na kutokana na sababu ya kua Tanzania bado ni Nchi ambayo inaendelea na hatujafikia kile kiwango cha kuweza kua na vyombo vya kasi vya kusafirisha abiria kama Treni na na mabasi ya kisasa, Serikari isisitize zaidi utumiaji wa mabasi makubwa na kama UDA na si Costa njia hii itapunguza sana kero kwa wanachi,pia itapunguza kwa kiasi kikubwa zaidi swala zima la msongamano wa magari katika miji yetu husika. Asanteni sana.

Naomba kutoa hoja

Njeje Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sorry Nje ya mada: BREAKING NEWS: Steve Clarke joins Liverpool as first-team coach

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...