Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiangalia Ramani inayoonesha maeneo yote ya Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti, alipowasili kwenye kituo kidogo cha Hifadhi ya Taifa Serengeti Mkoani Mara leo, Makamu wa Rais yupo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa ajili ya Mapumziko mafupi. Wa pili kushoto Mke wa Makamu wa Rais Mama Aisha Bilal na kushoto Mkuu wa kituo cha Hifadhi ya Taifa Serengeti Mtango G.G. Mtahiko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal kulia, akizungumza na Mmiliki Mkuu wa Mahoteli ya Kempinski Bw. Al-Bwardy Ali mwenye Makao yake Nchini Dubai, alipokutana nae leo kwenye Hoteli ya Bilila Lodge Kempinski iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti. Makamu wa Rais yupo katika Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti kwa ajili ya mapumziko mafupi. Picha na mdau Amour Nassor wa VPO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. KAMA KAWAIDA NAONA NAE ANAANGALIA WAPI AJIMEGEE ILI KESHO ASHUSHE BONGE LA HOTELI AU LODGE. NDIO TANZANIA YETU LAZIMA UCHUKUE CHAKO MAPEMAAA

    ReplyDelete
  2. hizi pozi nyingine.Kama vile VP anajua kinachoendelea ktk hiyo ramani.Have a good vacation anyway.

    ReplyDelete
  3. Duh
    Kajamaa kapokapo tu! hata saa hakana..lakini kanasumbua big time!

    ReplyDelete
  4. Waswahili wanasema "Raha jipe mwenyewe","Baada ya ziki Faraja","Mchumia juani Hula kivulini" MH.kazi kwako baada ya kukosa kuongaza Zanzibar umepata kuwa Makamu wa Rais kazi kwako nakutakia mapumziko mema lakini kumbuka mnamadeni na wananchi wa Tanzania, mmezunguka nchi mzima kunadi sera zenu MH. Pumzika lakini watanzania wote wanawaangalia na wanaimani MH.Rais pamoja na MH.Makamu wa Rais Kila la heri katika mapumziko yako kazi bado ipo mbele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...