Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amefanya ziara ya ghafla Moghadishu Somalia. Akiwa nchini humo amekutana na Rais Sheikh Sharifu Ahmed na waziri mkuu wa nchi hiyo. wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo usalama, tatizo la ukame, misaada na ulinzi, lakini kikubwa zaidi ni mkakati mpya uliowekwa na serikali ya Somalia kumaliza uasi nchini humo na kuleta amani ya kudumua baada ya zaidi ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Je ni mkakati gani huo tegea sikio mahojiano haya kati ya mkuu wa Idhaa ya redio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha na Balozi Mahiga anayeanza kwa kufafania kwa nini kaenda Somalia ghafla.

Ili kuyasikiliza bonyeza link hii
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/
au http://www.facebook.com/UNRadioKis
http://twitter.com/redioyaum

au moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/119523.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...