Marehemu Swetu Fundukira

Ni mwaka mmoja tokea ndugu yetu, kaka yetu, mpendwa wetu Swetu Fundikira alipouwawa kikatili. Globu ya Jamii inaungana na familia ya marehemu katika kumkumbuka Swetu ambaye japo kimwili katutoka, lakini kamwe kumbukumbu yake kuwepo nasi wakati wa uhai wake itadumu milelel nyoyoni mwetu.

Leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inategemewa kuitaja tena kesi hiyo na hatimaye, kwa vile haina mamlaka ya kusikiliza na kuendesha kesi ya mauaji, itaipeleka Mahakama kuu tayari kwa kuanza rasmi na watuhumiwa wawili waliokamatwa kufikishwa kizimbani kujibu mashitaka. Ni matumaini yetu kwamba haki itatendeka, japokuwa kwa kufanya hivyo hakutamrejesha duniani Swetu wetu....


Mola na ailaze pema Roho ya Marehemu

-AMINA


Kwa kumbukumbu ya matukio ya kifo cha Swetu Fundikira
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Eheee! Hivi hii Kesi ya wanajeshi waliomuua FUNDIKIRA iliishia wapi wadau hebu tukumbushane basi. Au yamefanyika mambo kama ya DOWANS.

    ReplyDelete
  2. Si ajabu Faili limeshachomwa moto na watuhumiwa wanatembea mitaani kama vile wao ndio waliofanyiziwa.Bongo tambarare. Sheria za bongo zipo ktk madaftari lakini hazifanyi kazi yoyote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...