MAISHAMEMA TANZANIA.

SHINDANO LA UCHORAJI.

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya MAISHAMEMA TANZANIA, kupitia mradi wa Sexuality Education & Awareness Project ( SEA Project ) , inatangaza tangazo la uchoraji kwa watu wote wenye uwezo wa kuchora.

Michoro ibebe ujumbe ulio katika moja wapo kati ya mada zifuatazo.

1. LESBIANISM IN HIGHER LEARNING INSTITUTIONS OF TANZANIA.



2. LESBIANISM IN SECONDARY SCHOOLS OF TANZANIA.



3. LESBIANISM IN PRISONS OF TANZANIA.



4. LESBIANISM AND HIV/AIDS; A CASE OF TANZANIA.



5. LESBIANISM IN TANZANIA.



Michoro iambatane na maandishi na iwe yenye kuchukua kuanzia kurasa hamsini ( 50 ) na kuendelea. Maandishi yanaweza kuwa katika lugha ya kiingereza ama Kiswahili.

Washindi kumi watakao chora michoro bora watapewa zawadi pesa taslimu, shilingi laki tatu za kitanzania ( Tshs 300,000) pamoja na LAPTOP.

Washindi watatu wa kwanza watapewa mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa wachoraji wa kazi zote za taasisi.

Michoro yote itumwe kabla ya tarehe 1 February 2011. Michoro itakayo tumwa kabla ya tarehe 1 February 2010, haitafanyiwa kazi.

Michoro itumwe kwa

COORDINATOR,

Sexuality Education & Awareness Project.

P.O.BOX 35967,

DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Please weka anwani ya simu au email kwa mawasiliano zaidi.

    Hilo box office haliruhusu mawasiliano ya haraka.

    Pia ni vizuri kuweka jina la huyo Coordinator na ofisi zenu ziliko. Hii kitu kama Genuine, kwanini kunakuwa na usiri mwingi?


    NB: Nadhani kuna makosa yamefanyika katika kuweka deadline. Kuna haja gani ya kusema michoro itakayotumwa kabla ya tarehe 1 February 2010 haitafanyiwa kazi. Vitu vidogo kama hivi vinaweza kuwafanya watu washushe credibility ya hilo shindano na waandaji wake.

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa walinichekesha kweli, eti wanataka michoro isiyopungua kurasa hamsini zawadi laptop na laki tatu kisha mkataba. Kwanza ilibidi watambue michoro hamsini ni mingi sana kuliko hizo zawadi walizotaja. Jamani, tunathamini kazi za watu. Mimi ni mchoraji lakini mashindano ya namna hii kamwe siwezi kushiriki!Michoro hamsini!? Ingawa nimechelewa kuchangia lakini nadhani kupitia mtandao huu ujumbe umefika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...