Mpendwa mhariri,
Mimi napenda kushukuru kwa mabadiliko makubwa yaliyo tokea katika Ubalozi wetu wa Washington DC.Kwa sasa kuna uchapakazi wa hali ya juu kitu ambacho kimetufanya ata baadhi yetu kujisikia kuwa karibu na ubalozi wetu na kujituma katika kuitangaza nchi yetu kwa wageni.

Wakati nimepata nafasi ya kufundisha kuhusu Tanzania kwa wanafunzi wa maskout katika state ya ALABAMA-mji wa millbrook,nilipata ushirikiano mkubwa na mzuri kutoka katika ubalozi wetu kuanzia mweshimiwa balozi pamoja na maafisa wa hapo ubalozini.

Shukrani zangu zimwendee afisa anayeshughulikia mambo ya utalii aliyeweza kunitumia mabango ya kuitangaza nchi kwa njia ya fedex na yakanifikia katka muda wa siku mbili.

Afisa huyu amefanya kitu ambacho
watanzania waishio washington hawakukipata kabla.
Napenda kumshukuru saana.

Ndimi Projestus Rwegarulila
VIDEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Napenda nimshukuru sana ndugu yetu anayeitangaza Tanzania nje (USA). Hayo yaliyofanyika ni mambo mazuri sana, hasa kusaidia Wamarekani kuielewa Tanzania. Ninachoweza kusema ni hiki-
    1) Si wengi sana hapa Marekani wanajua mambo ya nje ya nchi yao, achilia tu Tanzania. Tukiwa nyumbani tunafikiri watu wanaijua sana Tanzania, la hasha. Kila siku unakutana na watu wanaoshangaa kwamba Tanzania ni nchi, maana hawajawahi kuisikia.

    2) Tukiwa nyumbani tuna mawazo kuwa tunajulikana sana. Si kweli. Tanzania tunaijua zaidi sisi, na wenzetu majirani wa Afrika, na zaidi Waingereza - watu wazima, sababu walitutawala.

    3) Naomba nipunguze makali kidogo yanayoonesha kuwa uongozi wa ubalozi uliopita haukufanya kitu sababu tu mtu mmoja aliyekuja jana amefanyiwa kitu fulani alichopendezwa nacho. Hata kama watu wa D.C wamesema hivyo, bado si kipimo tosha. Kwani hao wa D.C ni wangapi waliosema hivyo? Kulikuwa na mkutano wa Watanzania wote waishio pale? Ikumbukwe kuwa aliyekuwa balozi pale, mheshimiwa Ombeni Sefue, naye kuna mambo mazuri aliyafanya pia. Alitutembelea sisi wa majimbo ya mbali kabisa akitokea D.C, na sasa ameteuliwa na rais J.K kuwa mwakilishi wa kudumu (balozi) wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, USA.

    Asanteni nyote, na tubarikiwe na nchi yetu ya Tanzania!

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi sijawahi kuchafua hali ya hewa, wala kujeruhi hisia za watu wengine, nimekutumia email mara kibao uweke link za libeneke la tanzania katika skyscrapercity forum lakini wapi, mimi nilikua wa kwanza kuamini kuwa hii blog ya jamii haibagui, lakini mbona sasa nadhani inabagua? sitaki kurukia conclusion lakini bado naamini utaweka siku moja ili wadau wachangie na tupate forumers wengi katika libeneke la TZ
    zifuatazo ni link na wadau wote karibuni
    DAR ES SALAAM AND ZANZIBAR PHOTO GALLERY
    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430948

    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430948&page=38
    TANZANIA TOURISM
    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=803392

    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=803392&page=13
    TANZANIA GENERAL CONSTRUCTION
    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1135361
    TANZANIA ROADS HIGWAYS AND STREETS
    http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1265595

    ReplyDelete
  3. Sijaona tofauti ya english ya( Mpoki na Joti ) na mwalimu huyu.u know ze BIG big city Dar es salaam ...made my day

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 05:33:oo AM unanionea. Hebu bofya link hii uone mwenyewe.
    Si vyema kulaumu bila kufanya utafiti. Inakuwa noma. Hata hivyo hongera na ahsante kwa mchango wako muhimu. Tatizo letu watanzania ni wazito sana kuchangamkia mambo kama haya. Link yenyewe ni hii:


    http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=SKYSCRAPPER+CITY

    ReplyDelete
  5. Mwalimu kajitahidi lakini "amechemsha" anaposema mlima kilimanjaro umetokana na rift valley .... hapo kachemsha big time!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...