Makamu wa Rais Mhe.Dr.Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) bwana Abrahamu Shamumoyo mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano huo ambao ulimchagua Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Didas Masaburi kuwa Mwenyekiti mpya wa Taifa wa ALAT, nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mheshimiwa Diwani Daniel Okona.
Mwenyekiti mpya wa ALAT Taifa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Didas Masaburi akipongezwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza bwana Wilson Kabwe, Mstahiki Meya Masaburi aliwashinda wagombea wengine wawili kwa kupata jumla ya kura 217 kati ya kura 278 zilizopigwa.
Mke wa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mheshimiwa Janeth Masaburi akisalimiana kwa furaha na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia ELIMU Mhe.Kassim Majaliwa mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za uenyekiti wa Taifa wa ALAT ambapo Mstahiki Meya Masaburi alishinda kwa kishindo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Eliakim Chacha Maswi akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma James Msekela. Anayesikiliza kwa makini mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI bibi Maimuna Tarishi, kabla Makamu wa Rais hajaufungua rasmi Mkutano wa uchaguzi wa ALAT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...