Home
Unlabelled
mpunga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wali mwingi, ndizi moja, kiazi kimoja, nyama 2: sasa nani atakula na nani ataacha? kwanza hapo hygiene pia ni tatizo, meza ina kutu si mchezo, si ajabu hata yayo masinia yana kutu pia. kingine cha ajabu ni kuwa kuna masinia yamewekwa juu ya mengine, lo! nina uhakika chini ya haho masinia sio kusafi, sasa hamuoni ni kuchafua chakula kilicho ndani ya masinia yaliyo chini? kwanza kwanini mpakue kwenye masinia? mbona hayo mambo yamepitwa na wakati? kila mtu awe na sahani yake jamani, huo ndio ustaarab
ReplyDeleteAhh Ahh kitu cha UBWECHE hicho... Uchafu!!! wewe mtoa maoni hapo juu utakuwa mtoto wa KISHUA na haukupitia haya mambo ya kwetu USWAZI. Tena nahisi ulikuwa unakatazwa kula kwa watu. pole for not having those OLD GOLD MOMENT in your life time. Ila nahisi kama bado haujachelewa vile...
ReplyDeletewewe madau hapo juu acha uzushi kupitwa na wakati ndiyo nn?? haya mambo ya pwani bwana kwa watani zangu wa jadi(wazaramo). Hata mm sikuhizi napenda hii kitu(pilau), si unajua kule kwetu(TBR) ni Ugali na mrenda wee acha tu!!
ReplyDeleteMdau DSM TZ
Huitwa pia shaba. Tuliokulia Kariakoo, Ilala, Jangwani, Gerezani, Migomigo na Tandale twaijua raha ya hii kitu. Huyo anayesagia kaja mjini ukubwani (na Mwenge?) hivyo tumsamehe wajameni. Babu yangu nakumbuka zamani alikuwa ananichukuaga kwenda kwenye shughuli ya ziara Mlingotini, Bagamoyo. Basi kuna siku niliona mpunga umepakuliwa bado kutiwa kwenye masinia. Ulikuwa mkubwa kama volkswagen beetle. Yaani hadi leo nakumbuka, Dah!
ReplyDeleteDah, naona hili beche la ushuani sinia mtu 3.
ReplyDeleteMdau wa kwanza ana problem kubwa sana ya matatizo! Tumpe pole jamani!
ReplyDeleteWamatumbi bwana!sasa wewe mdau wa hapo juu umeona kuwa kula kwenye sahani kwa pamoja sio ustaarabu ukaona eti kula kwenye sahani peke yako ndio ustaarabu, hizo ni falsafale za kimagharibi kule kwetu hivyo ndivyo tunavyo kula na kwa kweli jamii zetu zinazidi kupendana.Na huu umasikini wa kiroho umefanya watu kuanza kujenga dining rooms ati kuwekwe meza na kila mtu na sahani yake,zamani watu walikuwa wanatandika mikeka nje na kula atakae bahatika kupita basi anakaribishwa,those were the good old days.Sasa hivi kila mtu mzungu.Msinielewe vibaya siko against maendeleo, lakini mtu anapouita utamaduni wa kwao kuwa hauna ustaarabu hapo kido mimi simfahamu.
ReplyDeleteHiyo ndo uswahilini matala kwetu Bongo sio kila mmoja anaenda hotelini wengi wetu tunaudhuria uswahili iwe harusi vilio na hitma kisomo kama hapo juu,ndi makuzi yetu!wewe mdau hapo juu unavya ulofa,hasaa huwo ni ulimbukeni,sasa unafikiri nafasi ya kuweka masinia ipatikane wapi na ndizi mbona zinatosha tu na nyama ndo kiasi cha pesa acha ushamba wewe!hata kama umezaliwa Masaki matembezi yako Ikulu kisha unapanda ndege unashuka UK au Amerika sina uhakika kweli,huna ndugu au rafiki kariakoo temeke au mbagala,au hata ulosoma nao,zamani,,,,,Eee mshamba jamaa mdharau kwao mtumwa sio wewe tu wako wengi malimbukeni wenye vya ulofa kama wewe,,,Pole sana... Hanny
ReplyDeletehuyo mdau wa kwanza hapo juu mshamba sana yani. au ni kipofu, yani yeye haoni hapo kama kila sahani ndizi 3 na maana yake ni watatu watatu. inabidi akafanyiwe uparesheni ya macho.
ReplyDeleteraha ya MPUNGA WA SHUGHURI muule mzunguko, yaani watoto mtandazo na wakubwa vidole kuzama sasa we mtoto wa kishua hapo juu nenda kale kwenu kwenye sahani za udongo tuache sisi washughulini tujinonofoe na kitu cha beche au wanauita wali mchafu. kingine cha ukweli kuhusu hili beche wamelifanyia modification maana kuna kitu cha ndizi juu!!! zamani tulikuwa tunakuja nazo wenyewe na pilipili mfukoni..PILAU JUUUU.
ReplyDeletewenye tabia za kichoyo utawajuwa tu... hapo juu kabisa Mungu hupenda upamoja na lazima wanadamu wajikumbuke kwa pamoja kwa kila zuri. Wewe susa wenzako Twala.
ReplyDeletewe acha tu hivi vitu vina raha yake bana ....imiss this....
ReplyDeletesasa sijui mimi nimgonjwa?? Maana nilivyoiona tu hii picha harufu ya pilau ikanijia puani waziwazi. jamani, heeee....!
ReplyDeleteYaani hakuna mtu aliyetaja kachumbari?? Tena lina pili pili!!
ReplyDeleteKuna mtu kasema nyama chache? Hahahaha, mbona ziko bwelele tu, sio mpaka ufukue mchele...
Huyo wa juu angejua tu, sehemu hizi wajanja huwa wanaenda na ndizi zao. Sasa ukikuta ndizi mbili/tatu kwenye sinia lako, ujue hapo mambo supa!
Halafu wazee wa Ujiji hapo wanakuvalia kanzu iliyotoboka, ili watoto mnakalia kushangaa "vitunguu" wakati mzee anafukia ubeche.
ReplyDeletehaya ndio mambo ya nyumbani KILA NYAMA TIA SHINYANGO NA MCHUZI ROVIROVI KOMBE LIWE SAHANI aaaaaaaa nakumbuka kwetuuuuu
ReplyDeleteHapa sio butiama pale magomeni mapipa? maana pilau la pale asikuambie mtu... unaweza kununua sahani mbili...
ReplyDeleteHamna atakaebisha pilau la shughuli si mchezo. Na raha yake inakuja unapoitafuta nyama halafu unaipata
ReplyDeleteKuna sinia moja hapo mbele lina mfupa mkubwa kama paja la bata ...kaaa!!! ningelipata hilo ...mmhhhh!!! mate yananitoka
ReplyDeleteNAUAKIKA UKITOKA HAPO LAZIMA UJITIBU NA ZAIDI YA SHILINGI 20,000/= KWA FAIDA YA KULA CHAKULA KISICHOZIDI GHARAMA YA 1000/= ETI KWA KUPENDA PILAU HATA KAMA NI USHAMBA WA PWANI BASI NA IWE.
ReplyDeleteHuyu jamaa wa juu ni mjinga na hana malezi. Tabia ya kila mtu kula sahani yake ni dalili ya uchoyo na roho mbaya. Mpunga kama huu wa pamoja ndio unaoleta upendo na mashirikiano katika jamii. Yeye anasema nyama ni kidogo. Hata kama hakuna nyama huo ndio uwezo wake alojaaliwa na mungu. Lakini kama mimi ningelikuwepo naona inatosha hiyo TONGE NYAMA
ReplyDeleteMdau wa juu huyu haelewi uswazi, katoka kwao kili, kafika dar anakaa kwa mushi, kapewa paper ya mtihani na kwetu kumoja, baadae kapewa scholarship ya UK na mjomba slaa. Sasa anatubeza walala hoi kwenye shughuli yetu.
ReplyDelete