Mkali wa mashairi nchini,Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akiimba moja ya mashairi yake usiku huu katika kiota cha Mzalendo pub akiwa sambamba na bendi yake ya Mjomba Band ambayo itakuwa ikifanya mambo yake katika kiota hicho kila siku za Alhamisi kuanzia leo hii.
Aliekuwa mshiriki wa Tusker Project Fame,Aneth Kushaba ambaye sasa yuko na bendi ya Mjomba akiimba kwa hisia kali moja ya nyimbo za bendi hiyo katika ukumbi wa Mzalendo pub usiku huu.
Wapenzi wa muziki wakiyarudi magoma.
Supa staa Steven Kanumba akilisakata kisawasawa wakati bendi ya Mjomba ikifanya vitu yake usiku huu katika ukumbi wa Mzalendo pub.
Ray nae akiwakilisha na shairi lake huku Mjomba Mpoto akiachia bonge la tabasamu kuona kwamba vipaji vipo vya kutosha kwa upande wa mashairi.
Safu ya Ushambuliaji ikiwajibika.
Wadau kibao waliohudhulia katika ukumbi wa Mzalendo pub kuipa tafu Mjomba Band ambayo inafanya vizuri katika tasnia hiyo ya muziki wa laivu.wapo katika kiota hicho kila siku ya Alhamis,hivyo jitahidi alhamisi ijayo usiukose uhondo huu.

kwa picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mjomba ni msanii wakeli apewi sifazake kwa sababu ana u ccm !!
    mdau paris

    ReplyDelete
  2. looking nice Kanumba!!

    ReplyDelete
  3. bora kabadili mavazi..nalia pia na kaka zangu kanumba na ray, ur good looking lakini mnajiharibu kwa kuachia sana miili na kutumia chemicals katika nyuso zenu. zinawaharibu.

    Mama ushauri.

    ReplyDelete
  4. Ingekuwa vema endapo bwana michuzi ungetutangazi a day before ili tuweze kuhudhuria sasa utaonyesha leo wakati mambo yalishafanyika jana maana yake nini (DOOORI DORI DOORI SAMWELA)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...