Ankal,
Naomba unitangazie kwa wadau kwamba gari hili aina ya Nissan Caravan Hiace yenye namba za usajili T202 BNQ limebwa January 21, 2011 nilipokuwa nimeegesha pale Hongera Bar jijini Dar es salaam. Yaani nimechanganyikiwa. Tumeshatoa taarifa Polisi Mabatini Kijitonyama kwa RB NO: 497/11 Atakayeliona please naomba atoe taarifa kituo chochote cha karibu cha polisi ama anipigie simu namba
+255 718 099 963
.
Zawadi Nono Itatolewa kwa atakaye fanikisha kupatikana kwa gari hili.

Mie niko Mwenge, Dar es salaam. Chonde chonde naomba msaada wadau wa Globu ya Jamii.THE PLATE NUMBER IS T202 BNQ,

kwa ndani linaonekana hivi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Du, pole mdau mwenzetu, hii inasikitisha sana.Afadhali kama Documents zote bado unazo na hukuziacha kwenye hilo gari maana hiyo Hiace inaenakana haina hata plate Number. Jamaa hao hawawezi fika mbali watakuwa wamo mitaa ya jijini Dar mpaka watafute namna ya kuweka namba za badia ili waweze kuchomokea mikoani, hivyo kuwa makini sana. Mungu mkubwa utapata gari yako.

    ReplyDelete
  2. Kwanza pole sana mdau,mwizi atakuwa ni watu wanaofahamika hapo arround,jaribu jaribu kusikilizia lizia maeneo ya karibu unaweza ukapata fununu zozote.
    pili,ni swali la kiuzushi hiyo gari ulikuwa na mpango wa kuifanya Ambulanse nini,mambo ya vitanda ya nini tena?Au ndio nyinyi munaoleta "mobile guest house",Haraam,Laana tu LLah,utapata tabu sana kuipata,Astaghfirullah
    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  3. Wadau - hili gari halijaibiwa - mwenyewe anafanya advataiz tu hapa -- "nayegambisiliza" -- nimepata hii idea baada ya kupitia hii blog kwa mara ya tatu. Kama ni gari liloibiwa tusingeonyeshwa ndani mkao wake n.k. Halafu bar za Bongo si wanywaji na magari yao wote wanakuwa nje jamani??? Sasa ulevi gani mtu umenunua gari "jipya" kama hili halafu unalewa mpaka unakuja shtuka limetoweka!! Uzushi huu. Niko zangu hapa TX napata vinywaji pia, kuna uzuri wa "kuchemsha" kichwa sometimes unapata revelations kama hizi. Hili gari halijaibiwa wala nini. Sielewi kwa nini anko wetu hakushtuka hapa

    ReplyDelete
  4. Kweli. Mimi pia sidhani kama limeibiwa. Hajataja namba za usajili. Ukiangalia picha kwa makini gari inaelekea lipo yard (kama za autorec ukiwa unatafuta gari mtandaoni)

    ReplyDelete
  5. duh, mbona hajataja hata plate number zake? hii inachanganya anyway POLE!

    ReplyDelete
  6. Inawezekana kweli imeibwa ila hakuwa na picha ya gari baada ya kuinunua, labda ndo mana ameona ni bora aweke picha za zamani ili watu wajue ilivyo ndani. Kutokuwa na viti ndani ya gari si hoja,Bongo mafundi wapo wanaunga kila kitu,kwa hiyo tusimsemee vibaya ila tumsaidie na kumpa pole.

    ReplyDelete
  7. MH, jamani duniani kuna mambo, hii gari inavyoonekana ndani,ni kwamba nyuma kuna vioo,lakini kwa ndani hivyo vioo vimezibwa na sponji nzito,inamaana wa ndani hawaoni nje na wa nje hawaoni ndani,du! sijui mwenyewe alitaka kutoa msaada hospitalini? Pole sana,utaipata tu jaribu kuulizia maana blogu hizi watumiaji wengi wapo nje ya nchi,hivyo fanya jitihada huko huko bongo.

    ReplyDelete
  8. mkuu inabidi utoe pia na zawadi hakuna mtu atakayehatarisha maisha yake bure.

    ReplyDelete
  9. pia pole sana mungu atakusaidia.

    ReplyDelete
  10. Pole sana. Sasa mbona ulienda kulianika katika b aa?

    ReplyDelete
  11. Nyie hamjui kusoma au vipofu?
    Namba ya kusajili ameiweka bayana kabisa... T202 BNQ au hauioni?

    ReplyDelete
  12. Duh kweli kuna wabongo wazito kuelewa. Yaani ukisoma baadhi ya comments hapo juu unabaki kujiuliza hao walioziandika wanajua kusoma na kuelewa ama la.

    ReplyDelete
  13. hili gari ni la kusex nini ? lina bed 6x6

    ReplyDelete
  14. picha kwenya tradecarview, really nice.ni uongo tu hapo

    ReplyDelete
  15. Hii gari ni kwa ajili ya Funeral Directors (Wasafirishaji miili ya Marehemu kwa staili ya kisasa).

    Sasa jamaa waliokupua hii gari ya mazishi walikuwa wanafikiria nini, pia mwenye gari alikuwa anasubiri nini Hongera Bar na gari ya mazishi?!

    ReplyDelete
  16. napingana na wote wanaosema kuwa gari hii imeibiwa,
    muongo mkubwa, hii gari ameizimikia, ndio maana ameamua kuirusha hewani asikilizie watu nao wataisifia kiasi gani.
    hakuna dalili zozote kama imeibiwa.inaonekana ipo yard ( kwa wale wa japan mtakubaliana nami).mimi nahisi ungesema kuwa unachanganyikiwa ulipoiona,uliitamani tu. picha zaidi zinaonyesha kuwa gari HAINA PLATE NUMBER,IPO YARD KAMA SIO BANDARINI(hapa ni JPN).
    but all in all, its nice choice,real wealth to buy... ila umedanganya umma.tuma gari nyingine watu washangae!!

    ReplyDelete
  17. Watu wengine bwana! Mwenzenu kasema ameibiwa, nyinyi mnabisha, yaani mmezoea ubishi tuu. Ametoa RB No, ametoa number za gari, amejaribu kutoa picha za gari alizonazo wakati analiagiza, bado hamuamini??? Kama huwezi kumsaidia kaa kimya, usibishie......

    ReplyDelete
  18. Nadhani baadhi ya wachangiaji hawako makini hawajasoma vizuri maelezo wanakurupuka kuchangia. Picha alizotoa jamaa ni zile alizopata wakati anaagiza gari yake ili ziweze kusaidia kulitambua gari lenyewe. Namba za usajili katoa ambazo ni T 202 BNQ. sasa mlitaka afanye nini. Kumbukeni gari inaweza kuibwa popote pale hata kama umepaki ndani ya uzio wako. cha msingi ni kumsaidia jamaa kwa atakayebahatika kuliona ili afanikiwe kupata gari yake na si kutoa maneno ya dharau.

    ReplyDelete
  19. Watu bwana! Kwani ni lazima uongee/uandike? Kama huna la maana la kusema kaa kimya.. Anon wa Mon Jan 24, 10:11:00 AM 2011 pamoja sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...