Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe (pili kulia), Katibu mkuu wa Chama hicho,Dr. Willbroad Slaa (kati) pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini,Mh. Philemone Ndesamburo wakiwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha leo kusomewa mashtaka ya kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano yaliyofanyika jana mkoani humo.
Viongozi wa CHADEMA Wakimsikiliza wakili wao walipokuwa katika Mahakama ya Arusha leo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Willbroad Slaa akipena mikona na baadhi wa wanachama wa chama hicho waliofika Mahakamani hapo kusikiliza hamta ya kesi ya viongozi wao.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, katibu mkuu wa chama hicho Mh. Wilbroad Slaa na wabunge wa Moshi Mjini na Arusha mjini Mh. Philemon Ndesamburo na Goodluck Mrema wamefikishwa mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomewa mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano.
Timu ya Jamii iliyoko eneo la tukio inaeleza kwammba wah. Mbowe, Slaa na Ndesamburo walifika mahakamani hapo kwa pamoja katika gari la kawaida, wakati watuhumiwa wengine wote walifikishwa kwa karandinga.
Hivi tunavyoongea mchakato wa kuwawekea dhamana unaendelea na tutafahamishana kadri habari na picha zitavyokuja toka Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Naapa. Ipo Siku watanzania hawatakaa na kuangalia tu mafisadi wakitafuna nchi kama ni ya kwao. Wataibuka watu kama Dr.Slaa wengi ambao watawaamsha watanzania na kuleta mapinduzi na kuwaweka mafisadi rumande wasote huko mpa waoze. Mungui Ibariki Tanzania! Bado sijapata jibu kuhusu jengo nyuma ya umoja wa vijana ambayo imejengwa kweneye eneo wazi ni ya fisadi au?

    ReplyDelete
  2. Natoa Pole Kwa Viongozi wote wa Chadema Kwa mateso waliyoyapata. Pia Natoa pole kwa Marehemu Waliouwa Kinyama na Polisi. (RIP).

    JUST REMEMBER THIS CHADEMA YOU WILL NOT WALK ALONE.

    USA.

    ReplyDelete
  3. Jamani nchi zote unahitaji kibali kuandamana, sasa kama kibali walinyimwa kwanini walienda kufanya hayo maandamano,sheria ziliwekwa ili zifuatwe. Kosa ni la hao waliondelea na hayo maandamano sasa watu wamepoteza maisha mnaanza kulalamika haya yangu macho. You won't see me out there doing maandamano will be looking through my window. Kwa wale wote wanaongebea uongozi kwa nguvu huwa hawana nia njema. Pole kwa watu waliopigwa na waliofariki sometimes police have to use all measures in there power when doing there jop.

    ReplyDelete
  4. Chadema you have my full support!! Sina chama lakini hii imenifanya nipate mwamko wakujiunga na ninyi. Inauma sana mtu akikunyima haki kwakweli.

    ReplyDelete
  5. kwakweli nimesikitika sana na uongozi wa viongozi wetu maandamano ni ya amani kwa nini wamewadhalilisha hivyo na kuwaumiza jamani ipo siku m mungu atasikia kilo chetu kwa mafisadi hawa wa njii hiii watatoka madarakani na wenye kujua kuongoza kwa amani wataongoza shame on u ccm

    poleni sana chadema na watu wote mliopata heka heka kuweni na roho ya kijasiri ipo siku tutafika tu

    siomwanasiasa

    ReplyDelete
  6. POLENI SANA VIONGOZI WETU WA CHADEMA,ILA SASA WANANCHI TUMEFUNGUKA MACHO HATUWATAKI HAWA MAFISADI WA CCM TENA MWISHO WAO UMEFIKA,YANI HATA UTUELEZE NINI CHADEMA TUNAWAPENDA HABARI NDIO HIYOOOOOOOOO,CHADEMA OYEEEEEEEE 2015 TUNAINGIA IKULU,MMEOTA MAVITAMBI YENU SASA VITAISHA KABISA EPA,RICHOMND NA DOWANS MTAVISIKIA KWENYE BOMBA MMETUULIA WANANCHI WETU SUBIRINI MWISHO WAKE MTAUONA SIO MIAKA MINGI

    ReplyDelete
  7. 1) Mnaodai kwanini Chadema ilikaidi amri ya kutoandamani, mnajua kuwa serkali imetoa kauli za kukingamana toka kwa watu 2 tofauti wote wenye mamlaka? Mbona hamsemi wawajibishweje?

    2) Okay, mnasema Chadema walikaidi amri halali. Je, polisi wamefundishwa kupambana na vitu vidogo kama hivyo kwa mtindo wa vita vya majimaji?

    3) Kuna siku nyie mnajifanya hamwoni madhambi ya CCM mtahalalisha hata wanafunzi wetu wanaogoma kudai haki zao toka kwa serkali ya CCM wauawe ilimradi tu maanadamano yatakuwa yamekataliwa na CCM na serikali yake.

    4) Wengine hatuna CCM wala CHADEMA, alakini hatukubali serikali ituburuze inayotaka. Nasi tuna haki ya sauti kama wananchi.

    5) Sauti nyingi ambazo hazikosoi serkali ya CCM kwa namna 1 ay nyingine ni wale wenye mirija ndani ya CCM au familia zao zinaishi kutegemea chama hicho na kutuibia sisi Watanzania.

    Na bado, mimi nataka siku 1 waniue tu hao askari limradi mbegu ya mapinduzi itakuwa imepandwa. CCM jueni haturudi nyuma, mtaua hadi mtumalize, potelea mbali.

    ReplyDelete
  8. One upon a time Martin Luther king said "A MAN WHO WON'T DIE FOR SOMETHING IS NOT WORTHY TO LIVE" and again he once commented that "RIGHT CAN NOT BE GIVEN FREELY BY THE OPPRESSOR BUT CAN BE DEMANDED BY THE OPPRESSED"

    PLOSI FANYENI KAZI YENU,ILA KAMA KWELI MNAJUA KWAMBA MNAISHI KWA KODI ZETU NA KUTUUA KWA SILAHA ZILIZONUNULIWA KWA KODI ZETU NA BADALA YA KULINDA RAIA NA MALI ZETU MNALINDA MAFINSADI NA MALI WALIZOTUIBIA-SIKU SI NYINGI TUMEAMKA-WAKENYA NI MFANO MZURI.MTATUUA ILA IPO SIKU NANYI MTAKUFA.
    MUNGU BARIKI MY MOTHER LAND-WALAANI VIONGOZI WANAFIKI WA CCM.NAJUA WAPO WASAFI ILA HAWAZIDI WATANO-TULISHUHUDIA WOTE KULA ZA MAONI-ASIYE NA PESAALIKOROGWA--RUSHWANI BABA NA MAMA WA CCM-HIYO HIANA SIRI NI WAZI KWEUPEEEE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...