Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsi Vuai Nahodha akiongea nasi muda mfupi uliopita. Kulia kwake ni Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema. Picha na John Bukuku
Serikali leo imependekeza pande zinazosigana katika siasia mkoani Arusha kukaa meza moja na kutafuta suluhu kwa mazungumzo na sio kwa vurugu.
Hayo yamesemwa mchana huu na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Shamsi Vuai Nahodha alipoongea nasi ofisini kwake jijini Dar, akiwa na Inspketa Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema, ikiwa ni siku moja baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa CHADEMA baada ya kufanya maandamano yanayodaiwa kuwa si halali. Inasemekana watu wawili wamepoteza maisha na sita wamejeruhiwa vibaya katika vurumai la jana.
Mh. Nahodha, ambaye kabla ya wadhifa wake wa sasa alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibra kwa muda mrefu na kuwa kiongozi mwenye uzoefu wa mambo hayo, amesema serikali imeamua kuingilia kati mgogoro huo kwa kuziweka meza moja pande mbili zinazokinzana ili kuleta amani mpya na kuidumisha jijini Arusha.
Pia Mh. Nahodha amesema askari polisi yeyote ambaye itathibitika alikwenda nje ya mipaka yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waliandamana jana jijini Arusha wakielekea uwanja wa NMC ambako walikuwa wana mkutano wa hadhara. IGP Mwema alikuwa ameshatoa tangazo jana yake (juzi) kwamba maandamano yamezuiwa na yakifanyika ni batili.
Juhudi za kumpata tena Mh. Nahodha kwa ufafanuzi zinaendelea, kwani kuna shauku ya kujua kwamba baada ya serikali kuingilia kati mgogoro huo unaotokana na sakata la uchaguzi wa Meya wa Arusha uliokwamba, je wana CHADEMA waliosomewa mashitaka leo watafutiwa kesi zao?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Too Late!!!!!!!!! Dr Slaa kama sikosei aliiomba serikali iingilie kati kabla ya 05/01/2011 serikali haikufanya hivyo imesubiri watu wafe na wajeruhiwe ndio wanasema wakae mezani watu wenye hasira, kweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu, shama la bibi

    ReplyDelete
  2. Ni nani anachakachua idadi ya waliokufa? Hivi ni kumi au wawili? Anayesema uongo kati ya hao ni nani na ana nia gani?

    ReplyDelete
  3. hongera sana mheshimiwa waziri na hongera uncle kwa kutupa hii habari muhimu kjapo uncle bado umekalia picha za tukio kuna watu wamekufa na damu imemwagika hiyo ni muhimu maana hao waliopelekwa mahakamani ni wazi watashinda maana hakuna maanadamano amamboyo ni batili kwa dunia ya sasa labda kama kuna fujo hako ni kama chezo tu ka jk kutmia dola vibaya
    mimi nachoweza kusema serikali kua watu sio vizuri haka kama wamekosa maandamano batili sio lakizi yatudhalimu damu
    juzi hapa london kulikuwa na maanadamano ya wanafunzi kupinga ongeeko la ada wanafunzi wakikuwa wanafanya funjo lakino hakuna mtu halikufu wala siraha za moto kutumika
    swali tanzania na uk ni nchi gani ina siraha nyingi za moto au nchi gani inaweza kumudu kuwa na siraha nyingi za moto
    plz jk do as a favour kama kweli una utu tusione damu plz not any more tnajua waliokufa sio ngudu zako lakini wengine inatuuma sana
    uncle tunaomba picha za tukio plz

    ReplyDelete
  4. Saidi Mwema Linanenepa tu, haukuwa hivyo wakati unatoka Nairobi. Inaonesha ni kiasi gani hufikirii ofisini.. Swala la arusha ni very simple, wala lisingefikia hapa tulipo. intelijesia ya wapi uliyoipata? ni ubabe wa kijinga kabisa.

    ReplyDelete
  5. Inasikitisha kwamba watu wamekufa lakini kumbe waliaambiwa kibali hakuna na wakiandamana ni batili!! Saizi yao, mkong'oto walioupata!!! Waliofariki Rest In Peace!!

    ReplyDelete
  6. lowasa alisema watu wakae meza moja,makamba likaibuka na kusema anamshangaa lowasa kwa kauli yake.sasa machafuko yametokea ndio mnataka kukaa meza moja.

    kibali mlitoa mda mrefu imekuaje mkaubiri siku moja kuzuia maandamano wakati watu wameshajiandaa na wengine wamesafiri kwenda arusha tayari?

    ReplyDelete
  7. Usitegemee Michuzi kutoa habari ambayo inapingana na kazi yake. Ukweli ni huu, Michuzi bado ni mfanyakazi wa serikali na habari ambazo anaona zitaweza kumletea matatizo hazitoi. Habari za Wikileak sijaziona ndani ya blog hii.

    ReplyDelete
  8. Kwani kuna makundi gani yanayogombana?, mbona HAYAPO? nani wazungumze? Madiwani 18 wa upinzani dhidi ya madiwani 13 wa CCM ili kumpata Meya? mbona CCM walishafanya uchaguzi na kumpata Meya baada ya tafsiri iliyotolewa na serikali? kitu gani serikali inataka wazungumze? Si Chadema walishapeleka malalamiko yao mahakamani au kwa waziri anayehisika sasa mazungumzo ya nini tena? naona IGP yupo katika kikao hicho, na yeye kweli ana sapoti hayo mazungumzo wakati alitekeleza wajibu wake wa ku-deal na wanaopinga maagizo ya serikali?
    Si tayari wahalifu wa tukio la jana wameshafikishwa mahakamani?

    PLEASE! BE SERIOUS AND DONT CONFUSE YOURSELVES AND THE PEOPLE.

    ReplyDelete
  9. Mzee lowassa si alisema hvi majuzi na Mzee makamba akamjia juu na kusema hivi na vile sasa leo imekuwaje tena?

    ReplyDelete
  10. President Kikwete please say something. You need to address Tanzanians and reassure them about their safety. That's what a leader does.

    ReplyDelete
  11. Wananchi wanaodai haki zao katika nchi zote za kidikteta huwa wanapoteza maisha. Nguvu ya watu haizuiliki. Kitajulikana kimoja! Zanzibar ilikuwa hivi hivi na sasa angalia serikali ilikaidi hadi wamekubali matakwa ya wananchi.
    February Mauzi

    ReplyDelete
  12. CCM HAIFAI KUONGOZA TENA...INARUHUSU FUJO NCHINI NA INAONEA MIKOA YA KASKAZINI.

    TUNAWANGOJA 2015, KAMA TULIKOSEA HATUTAKOSEA TENA.

    MDAU,
    ARUSHA

    ReplyDelete
  13. The goverment and CCM got bloody hands. No blood should be shed for this nonsense issue. CHADEMA is legally supposed to have mayor seat in Arusha. Numbers dont lie they have more seats than CCM. Its about time true democracy prevail in Tanzania than the sweet talk of the goverment is using to convince donor countries and the rest of the world that Tanzania is an island of peace. Truth walks bulshit walks and that real talk. Ibanie hii comment Bro Michuzi kwa udau wako.

    ReplyDelete
  14. kwanaza kabisa nakushukuru uncle kwa habari hizi. kusema ukweli ccm ipo cku moja watakuwa nje ya dola ata wakihiba kura vipi lakini ipo cku tu. wananchi ndiyo wanaochangua viogozi huyo jk mwenyewe ni rais kwa sababu ya wananchi kumpigia kura sio familia yake sasa kama serikari inauwa wananchi na kuwajeruhi vibaya eti maandamano si ya halali hili swala ni la kipumbavu wapi siku hizi dunia nzima akuna maandamano ya halali mimi sasa hivi hapa nipo mjini los angeles kuna maandamano ya aina mbili na polisi wapo wamesimama pempeni tu kuakikisha usalama wa wananchi sio kuhuwa wanachi. jambo hili limetuhuzi tena sana. asante

    ReplyDelete
  15. Jamani why why. si uTanzania huu. NI vigumu kuamini kuwa hii ndiyo Tanzania yangu hivi sasa. Kupiga na kuua wananchi wako siyo suluhu jamani. The government need to love her people jamani. Kama ni maandamano tu si ni kuwaacha tu waandamane na kuongea mpaka wachoke. Au waache wandamane mpaka watakapojisahau na kuanzisha vurugu wenyewe!!! hapo ndo serikali inaweza kudhibitisha kuwa CHADEMA wanachochea vurugu.
    Kikwete mbona anaonekana kama a kind and loving person. kwa nini lakini hawezi kuhurumia wananchi hata kama wanampinga. Ukiwapenda watu watajikosoa wenyewe kwa mapotofu wanyopanga. Loooo tukiendelea hivi don't be suprised tukaanza vurugu everywhere na sifa ya Tz kuishia motoni.

    ReplyDelete
  16. Somebody told me, Tanzania has the largest concentration of Animals in the world.

    No human being would beat and Kill others in cold blood

    ReplyDelete
  17. Wadau mkitaka comments zenu zisibaniwe na Michuzi andikeni kwa Kiingereza sababu Michu kiEnglish hakipandi kimeenda holiday. kwa hiyo anaona noma kumuita mkalimani atafsiri huwa anaziweka tu. lakini mkiandika kwa kiswahili na comment zenyewe zikiwa zinamnanga yeye au serikali wakati yeye ni mtu wa serikali hazitoki hata siku moja .
    mdau Paka la jikoni.

    ReplyDelete
  18. Waliambiwa:

    Mkutano ndio; kuandamana hapana!

    Si waende Bunge-ni? Bunge lina nini?

    Kama halina kitu, walifunge kabisa!

    Tuwe tunakutana chini ya vivuli vya miti, na kujadiliana hadi tukubaliane!

    ReplyDelete
  19. HIVI KUMBE KITI CHA UMEYA NI KIKUBWA KULIKO VITI VYA URAIS NA UBUNGE?

    MBONA CHADEMA HAWAKUANDAMANA PALE DR SLAA ALIPOSHINDWA UCHAGUZI? KUMBE ALISHINDWA KWELI? MAANA MPAKA LEO IMEINGIA 2011 HAKUNA USHAHIDI WALIOUTOA. HIYO WEKA PEMBENI KITI CHA RAIS KIDOGO, JE NA VITI VYA WABUNGE WALIOSHINDWA NA KESI ZAO ZIKO MAHAKAMANI IWEJE HAWA WABUNGE WASIFANYIWE MAANDAMANO LAKINI WAMEELEEKEZWA KUFUATA TARATIBU ZA KIMAHAKAMA KWA KUPELEKA KESI ZAO MAHAKAMANI LAKINI KITI CHA UMEYA ARUSHA WASHINDWE KUPELEKA KESI MAHAKAMANI?

    NA KAMA WALIPELEKA KESI MAHAKAMANI KWANINI WALIANDAMANA WASISUBIRI MAAMUZI YA KESI?

    ETI MEYA, MEYA, WACHA KATIBA MPYA IJE HUTU TUVYEO TUSIVYO NA KAZI VYOTE ISIPOKUWA NA MILANGO YA WIZI NA ULAJI TUTAVIFUTILIA MBALI, HAKUNA CHA MEYA WALA NINI, WALA SIONI HIZO KAZI ZA MAMEYA KWANZA MIJI YENYEWE MICHAFU, MAVUMBI NA MATAKATAKA KILA KONA, SIJUI HIZO COUNCIL ZINAFANYA KAZI GANI, HAPO KUNA WENYEVITI WA MITAA, MADIWANI SIJUI WENYEVITI WA NINI NDIO MAANA NCHI HAIENDELEI KILA MTU ANAJIONA BOSI ANACHEO NA KAMA HANA BASI ATAFANYA VURUGU APATE CHEO!

    Na nyie acheni sheria ifuate mkondo wake hakuna aliye juu ya sheria, mie sio mpenzi wa chama chochote lakini huyu babu atawaponza shauri yenu, utuuzima nao unakujaga kwa style nyingi, maana ukisikiliza hotuba yake yeye kila siku hajali cha sheria wala mahakama, sasa waacha mahakimu wafanye kazi yao, kwanza huko Arusha hakuna hata hakimu mmoja atakayemhukumu maana wote wako chini ya mamlaka yake, na hata wakati wa uchaguzi alikuwa anasemaga usalama wa Taifa wanaripoti kwake sasa nashangaa safari hii hawakumpa taarifa mapema kuwa kipondo kinakuja! Na hao mahakimu watawaachia yeye na wenziwe hamuoni kuwa kwenye kundi lao wamekwenda na gari lao la kawaida ina maana hawakulala mahabusu wametokea majumbani mwao wenzangu na mie walalahoi wanaofuata mkumbo wamelala rumande kwenye kunguni na mikojo na kupelekwa mahabusu ndani ya karandiga, ndio mtajua kuwa mwenye pesa sio mwenzio. Kama kweli wana solidarity na wote walilala rumande kwanini wao waje na karandiga hawa waletwe na magari yao ya kawaida na si la magereza wala la polisi. Wenzenu wanaenda kulala Mount Meru Hotel, nyie mwalala Polisi Motel! Kudadadeki hakuna mtu atakayenidanganya eti nivunje sheria kwa ajili yake!

    Mwendawazimu!

    Halafu nyie mnaoning'ining'ia kwenye screen zenu mnishukie na matusi kama kawaida yenu kama sijahack huto tu kompyuta twenu!

    ReplyDelete
  20. MGAMBO VIS A VIS POLISI NANI ZAIDII!

    Yaani Mbowe alivyokuwa anawapanga watu wake na magwanda ya mgambo utafikiri wanataka kucheza gwaride, mwe kumbe walikuwa wanakwenda kupambana na polisi. Na sijui kama kuna watu watarudia tena, ohoo nyie hivi vitu visikieni hivi hivi ukizingatia Moshi TCP ni hapo pua na mdomo ni kama vile kuwaita kuruta wa JKT waingie mtaani maana hao kuruta wa TPC walimalizia hasira yao yote ya adhabu za ukuruta kwa wanachadema! Lol! Si yakucheka lakini inabidi nicheke ka movie vile. Zamani tulivyokuwa wadogo tulikuwa tukiwaona polisi tunakimbilia ndani lakini watoto wa siku hizi wanakuwa wanacheza na polisi mtaani, tena polisi wa enzi zetu wengi walikuwa wakurya na wasukuma wamepanda juu kisawasawa!Enzi ya Mwalimu Freeman na wenziwe wangepelekwa vijijini kwao under escort wakakae huko bila kutoka kwa muda mreefu, huyo ndiye alikuwa Nyerere usingelimuona polisi anampiga wala kumkamata mtu lakini usingelikaa tena umsikie sijui Mbowe wala Slaa, yeye alikuwa anadeal na ringmasters or ringleaders, unapelekwa kijijini ukalale kwenye tembe lenu mjini unapasikia redioni!Bado hatuhitaji demokrasia Afrika inabidi turudi enzi za Mwalimu si ndio walikuwa wanaimba kwenye maandamano? Wanafikiri Mwalimu alikuwa wa kutania au kuchezea kama sasa?

    ReplyDelete
  21. Wataalam wa Utatuzi wa Migogoro/ soshiolojia
    Jana Waziri Shamsi alitoa "theory ya confict" katika mazungumzo yake na vyombo vya habari kwamba inasema "huwezi kujua seriousness ya mgogoro mpaka athari zitokee". Ndio maana Baada ya Mauaji na vurugu, serikalai inataka kupatanisha pande husika. Binafsi nina wasi wasi na hii theory kama ni ya kweli ama ametunga yeye tu, naomba ufafanuzi tafadhali!!!
    Mdau Zenj

    ReplyDelete
  22. SASA MMETUCHOKOZA WANANCHI WALIZOEA KUTUNYONYA 2015 MTALIJUA JIJI NA MATAA YAKE,KHAAAA KWANI WANGEANDAMANA INGEWAZUIA NINI NYIE SERIKALI??? MNGEWAACHA WAANDAMANE KAMA WANGELETA FUJO MNGEWASHUHULIKIA,MATOKEO YAKE WATU WAMEKUFA BILA HATIA WENGINE MAJERUHI,HII NCHI IMESHAHARIBIKA KABISAAAA ILA MWISHO WENU UMEFIKIA 2015 SIO MBALI,KUTUPANDISHIA KILA KITU BEI JUU MNATAKA HAYA MAISHA TUISHI AU???WE ULIESEMA ETI WAMEVAA MAGWANDA ULITAKA WAVAE KANGA AU BABA YAKO NI KIGOGO WA ..... NAONA UNAWATETEA SANA,YANI HATA MFANYE NINI WANANCHI TUNAPENDA CHADEMA PIGA UA TUPO TAYARI KWA LOLOTE KHAAAAAA TUMECHOKA MABILION MNAYATAFUNA SISI TUNALIA NA NJAA,SASA TUMEZINDUKA KAMA MALARIA HATUWATAKI TENA.

    ReplyDelete
  23. Serikali itaweza kuingilia vipi kupunguza watu wengine wasipoteze maisha yao wakati katika kila nchi duniani, askari polisi ni SERIKALI, ndio maana wanavaa magwanda yenye alama ya nchi na bendera ya nchi. Askari akikupiga ni sawa sawa na serikali imekupiga, isipokuwa katika nchi ambayo haiheshimu haki ya binadamu.

    ReplyDelete
  24. OOOH VAENI MAGWANDA YENU YA MGAMBO, NA WANAONDAMANA WOTE HAWANA KAZI ZA KUFANYA NA SHULE ZAO NDOGO!

    Eeh nimesema mnaandamana kwa sababu ya kukosa kazi ya kufanya mngekuwa mmeajiriwa maofisini mngelipata muda wa kwenda kufanya vurugu na kuandamana?

    Eti mmechokozwa wananchi wapi kutwa mwalia lia ooh polisi sijui wametufanyaje, wakati miaka ile CUF walipokuwa wanaandamana mnakumbuka maneno mliyokuwa mnayasema? Kuwa kipondo cha polisi ni sawa yao kwa sababu hamkuona kwanini wanaandamana ila ni udini na ukorofi tu wa waislamu. Na hata FFU walipoingia na buti misikitini na kuwapiga kinamama mlikaa kimya na kuchekelea kuwa ni size yao, hatukusikia cha TAMWA wala TAWLA kwatetea kina mama wale. kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu?

    Tena kila siku mkiona watu wanaandamana kazi kubeza ooh size yao wataandamanaje wakati wamekatazwa SASA NYIE MLIJIONA EXCEPTIONALS RAIA WA DARAJA LA KWANZA UNTOUCHABLES mtaweza tu kuandamana bila kibali na msipate kipondo cha polisi? HICHO KIPONDO SIZE YENU MAANA HATA JINSI UHURU WA NCHI HII ULIVYOPATIKANA HAMUJUI mlizoea kujibweteka na kutoa amri sijui nani kasema hivi na vile, na mimi nawapongeza jeshi la polisi kwa kutimiza wajibu wao bila kubagua kuwa hawa wakiandamana bila kibali wabondwe ila hawa waachiwe tu kwa kuwa ni malikia wa nyuki wakiumia tutakosa asali!

    ReplyDelete
  25. This is a beginning of a change...Tanzanians are tired of corrupt leaders and now they will come out in public to voice their frustrations. However, I wonder why did people continue to vote for CCM despite it's corrupt leaders??? When will that change??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...