Mgeni Rasmi OCD CID wa wilaya ya
Rungwe Afande Seifu akimwaga cheche tukioni

Kamati ya ufundi ya Laxmi Darts Club ya
Tukuyu ikipanga mikakati na listi ya wachezaji
Wachezaji wa Polisi Mbeya wakiwasilana na
'babu' yao wa kamati ya ufundi ili kujua mapema kama kitaeleweka

kulia ni mdau Gidion wa Laxmi akipongezwa na Thomas baada ya kushinda mchezo mmoja, hata hivyo Gidion hakufua dafu katika seti aliyocheza na Mbegalo wa Polisi Mbeya
Afande Adelade akitoa mishale kimiani
Matokeo ya mchezo hayakuwa mazuri kwa Wanyambala wa Tukuyu kwani walichezea kichapo cha jumla ya mabao 22:10 kwa 10:2 kama inavyooneshwa katika score board. Inasemekana walimuendea 'babu' kudai chao baada ya kushindwa wakati aliwaahidi mambo leo ni mswano...

Aslaam aleikhum Mjomba Michuzi,

Pokea salaam toka Tukuyu, Rungwe Mbeya.
Jana ilkuwa ni siku ya pilikapilika siku nzima hapa Tukuyu wakati Laxim Darts Club ilipowakaribisha Maafande wa Kituo cha kati Mbeya Mjini katika mchezo wa Darts wa kirafiki katika kuukaribisha mwaka 2011

Matokeo ya mchezo hayakuwa mazuri kwa Wanyambala wa Tukuyu kwani walichezea kichapo cha jumla ya mabao 22:10 kwa 10:2 kama inavyooneshwa kwa score board.

Wachezaji wa Poilisi Mbeya walionesha umahili na viwango vya hali ya juu sana katika singles na doubles pia. Afande Adelade wa Polisi ndie alikuwa bora katika mchezo wa jana. Mchezaji pekee wa kike toka Polisi Anna Mwakabonga alifungwa kwa taaaabu na Mussa wa Laxmi 1:2 kwa 2:1

Mara baada ya kumalizika mtanange Mwenyekiti wa Laxmi Darts Club Bw. Gidion Mwakalundwa aliwapongeza maafande wa Mbeya kwa mchezo mzuri waliouonesha na hatimaye kuibuka na ushindi. Lakini aliwatetea Wanyambala wa Laxmi kwa kufanya kwao vibaya akidai kilitokana na maandalizi mabovu, kukosa vifaa vya mazoezi na hata zana za kuchezea wakati wa mashindano ikiwa ni paoja na Mishale (Darts arrows) kwani wachezaji wake walikuwa wanaazimana mishale na hata wengine kuchezea mishale isiyolingana uzito. Alitoa wito kwa wana Rungwe popote pale walipo na wapenda michezo kwa ujumla kutoa msaada wa hali na mali kwa ndugu zao ili waweze kushiriki vyema.

Naye Mgeni rasmi katika mchezo huo OCD CID Rungwe afande Seifu alihimiza swala la michezo katika jamii na hasa kwa vijana ili kujiepusha na vitendo viovu na hata mambo ambayo ni hatari kwa afya zao kama Ngono. Pia alihimiza zana ya Polisi Jamii na Polisi shirikishi, kwa kupitia Laxmi Darts Club aliwapongeza wana Tukuyu na Wilaya ya Rungwe kwa ujumla kwa kuwa na mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi kwani wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kufichua maovu, hali ambayo imefanya Rungwe na mji mdogo wa Tukuyu kuwa tulivu.

Kauli mbiu ilikuwa “Darts – New Friends” = “Vishale – Rafiki Mpya”

Kwa wasamalia wema wanaotaka kuwasaidi Wanyambala wa Tukuyu (Laxmi Darts Clubu) kwa vifaa na kadhalika wawasiliane na Mwenyekiti Charles Mwakatobe simu +255 787 087 955,

e-mail: laxmidarts.club@gmail.com
Anuani ya Posta:
LAXMI DARTS CLUB
S. L. P. 63
TUKUYU, Tanzania

Na mdau Mjomba Juma






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. good to see luxmn club, I suppose luxmn bar is the home of this club, father make sure unakarabati vyoo vya hiyo bar yako.

    ReplyDelete
  2. Mjomba "Anonymous" yaelekea hujafika miaka mingi Tukuyu, Karibu sana utembelee, Hali ya Laxmi Bar sio ile ya miaka ya 1947 sasa ni pazuri sana. Umefanyika ukarabati wa hali ya juu, Karibu sana nyumbani Tukuyu

    ReplyDelete
  3. mbona sehemu chafu lakini

    ReplyDelete
  4. Kweli sehemu inaonekana chafu,

    ReplyDelete
  5. wewe mnaosema laxmi pachafu nafkiri hamjafika tukuyu muda mrefu

    pamekarabatiwa ile mbaya, na ile hotel ya ghorofa la laxmi imeishakamilishwa
    pazuri kwa kweli
    hongera fadher na dada anna karadia chibba kwa juhudi zenu
    mdau wa dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...