Pichani juu kulia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi Teknolojia, akikagua maendeleo ya ujenzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha. Aliyevaa tai ya njano ni Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. B. Mwamila akitoa maelezo kwa Waziri.
Prof. Makame Mbarawa, wa kwanza kulia, akipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya kupima mionzi kwenye maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania. Kazi ya Tume hiyo ni kukagua mitambo, migodi, hospitali na minara ya simu za mkononi ili kudhibiti na kuhakikisha kuwa kuna matumizi salama ya mionzi katika sehemu hizo. wa pili kulia ni Prof. Idd Mkilaha, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo na wa kwanza kushoto ni Prof. Kondoro, Mwenyekiti wa Bodi wa Tume hiyo. Tume hiyo ni moja ya Taasisi zilizo chini chini ya Wizara.
Prof. Mbarawa na wafanyakazi wa Taasisi, wa Wizara na wakandarasi wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya jengo la utawala la Taasisi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi hilo jina linatakiwa liwe MBAWALA AU MBAWARA???

    ReplyDelete
  2. Jamani hebu tuwe makini kidogo, huyo waziri anaitwa Mbawara, Mbarawa au Mbawala?

    ReplyDelete
  3. Jamani huyu waziri anaitwa Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na si vinginevyo! Waandishi wetu wa habari nchini tujaribu kuwa makini kwenye majina ya watu kama waandishi wa habari wa nchi zingine maana kukosea jina la mtu ni kumkosea sana na wakati mwingine inabidi kuomba msamaha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...