Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya bima ya Real Insurance Tanzania Bw. Joe Mcheheku akikaribisha wageni na wafanyakazi wa kampuni katika mkia wa jogoo (cocktail) maalumu ya kumuaga afisa mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni hiyo na kumkaribisha mpya katika ukumbi wa Kibo Hall wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar usiku huu
Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Real Insurance Tanzania Bw. Stephen Okundi akiongea katika mkia wa jogoo huo wa kumkaribisha rasmi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Real Insurance Tanzania Bw. George Sithole akiongea katika mkia wa jogoo huo wa kumuaga. Bw. Sithole anahamia Msumbiji ambako Real Insurance wamefungua tawi
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba alikuwa miongoni wa wageni mashuhuri kwenye mkia wa jogooo huo. Kulia ni mkewe Mama Everlyn Warioba na wengine ni wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo kubwa ya bima
Mwenyekiti wa bodi ya Real Insurance Tanzania Bw. Joe Mcheheku (kati) akiwa na CEO mpya George Okundi (shoto) na CEO anayeondoka Bw. George Sithole
Mapaparazi wakiwa wamemvamia Bw. Stephen Okundi kutaka kujua nini mikakati yake anayokuja nayo kama bosi mpya wa Real Insurance Tanzania. Kwa picha zaidi za mkia huu wa jogoo BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...