Naibu waziri wa habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara, akikagua gwaride rasmi la kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha JKT Mlale, Songea jana. Nyuma ya Naibu waziri ni Mkuu wa Kikosi hicho Major Abas Ahmed ambapo vijana 711 toka mikoa yote hapa nchini walihitimu mafunzo hayo ya Operesheni Uzalendo ikiwa ni ya 100 tangu jeshi hilo liundwe mwaka 1963.
Naibu waziri wa Habari Utamaduni vijana na Michezo, Dkt. Finella Mukangara akitoa maelezo kwa viongozi wa JKT Mlale-Songea, baada ya kukagua Shamba la uzalishaji Mbegu bora za Mahindi la Ekari 200 lijulikanalo kama Embakasi jana. (kulia) Mkuu wa kikosi hicho Major Abas Ahmed akifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri.
Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 842KJ, Major Abas Ahmed, akitoa maelezo ya kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi Operesheni Uzalendo kwa vijana 711 kwa mgeni rasmi, Naibu waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Dkt. Finella Mukangara aliyekaa kulia, kabla ya kuhutubia jana. (Aliyekaa kushoto) Mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenister Muhagama ameahidi kuchimba kisima cha maji ya kunywa kikosini hapo(Picha zote na mpiga picha wa mtandao huu Juma Nyumayo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hapa ndipo nilipofanya mafunzo yangu ya JKT, Ilikuwa ikiitwa operesheni miaka 30 ya uhuru. Mpo? wadau wa Lindipundipu, Lusonga, Magagula na Peramiho! namisi Ulanzi wa mitaa hiyo.

    ReplyDelete
  2. Mdau LondonJanuary 08, 2011

    OMG! Old memories nimepiga kwata kwenye kambi hii Enzi za Kanali Mtono tulipiga sana Miraba ya Embakasi,mraba unauona unapoanzia unapoishia huuoni duh!enzi za maafande Kijanga,Agrey,na Nguvu ya Nyani hapo ni Kombania B,hapo C unamkuta Pilato. Si mchezo Lakini watu tulikuwa tunajongo vilevile.
    Serikali idumishe JKT kwa kweli ni chombo kinachofunza sana maisha kwa Vijana.
    Mdau London

    ReplyDelete
  3. Nawaungeni mkono wadau hapa juu. JKT ilikuwa ni shule ya aina yake. Nilikuwa Mafinga, Operesheni Jikomboe, mwanzoni mwa mwaka 1973.

    Ilikuwa kazi kweli, chini ya maafande kama Ngonyani, Chacha (walikuwa Chacha wawili), Ndabagoye, Mungure, Halima, na Izunya. Tulikula mchakamchaka, "fang fang" na kichura kama hatuna akila nzuri. Sitawasahau makuruta fulani ambao walikuwa hawakomi kuwakorofisha maafande na kuishia kwenye suluba nzito.

    Ninashukuru kwa elimu niliyopata jeshini, ya masuala ya ukakamavu, masuala ya porini, silala mbali mbali na kufahamiana na watu kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania. Nyerere alifanya kazi nzuri sana ya kujenga utaifa kwa njia hiyo.

    Kwa mtazamo wangu, ingawa nimesoma shule na vyuo hadi kufikia kiwango cha juu kabisa, najivunia kwa namna ya pekee mafunzo ya JKT. Ningewakuta hao maafande wangu ningewaambia hivyo.

    ReplyDelete
  4. Shamba la Embakasi na mengine ya JKT yanatakiwa kuwa angalau ekari 20,000 ( elfu ishirini)kwa kutumia nyenzo za KILIMO KWANZA kama matrekta makubwa na JKT kuwa mfano wa kuwafundisha kilimo cha kisasa.

    Mambo ya ekari 200 karne hii ni kiduchu mno wenzetu utakuta mtu huko Guyana na ekari Milioni Moja kwa ajili ya ranchi ya mifugo ya kisasa ya familia yake.

    Mdau
    Aliyepitia JKT

    ReplyDelete
  5. kwanini wizaara ya habari na utamaduni? Wizara ya ulinzi wako wapi wao?

    ReplyDelete
  6. NIMEKUMBUKA ENZI ZANGU KWENNYE HII KAMBI,MDAU HAPA JUU UMENIKUMBUSHA ILE MIRABA YA EMBAKASI NA ZILE MBIO ZA MARATONI ASUBUHI KWENDA KUMWAGIA BUSTANI,ENZI YA MTONO, AKINA MAKARANGA PILATO,NA WENGINE.JKT JUUUUUUU.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  7. mdau wa USAJanuary 09, 2011

    nilikuwa nafikiria baada ya kufuta mambo ya form six kweanda JKT, Mlale ifungwa. Nakumbuka mambo ya lindipundipu, na afande Shaban compamia A, duu ilikuwa kali siyo mchezo. Mizigo ya kuni ilikuwa inaniua sana!!

    ReplyDelete
  8. Afante Shabani kombania A, na mambo ya lindipu mahindi ya kuchemsha kwenye debe, mizigo ya kini duu kweli JKT lazima iendelezwe nic chombo linachofunza maisha

    ReplyDelete
  9. Samahanini wana jamii, mimi ni kijana wa leo sasa haya mambo siyafahamu vizuri, ningepend kufahamu haya yafuatayo;-

    1.Haya mafunzo yanachukua muda gani?, mwezi 1,miezi 3,6,9,12 nk.

    2.Mkiwa huko mnalipwa au mnalipa na kiasi gani? au ndio sifa za kijinga "Operesheni Uzalendo"

    3. Nikitaka kujiunga natakiwa nifanye nini na niwe na sifa gani.

    4.Baada ya kumaliza hatua hii watajiunga JW ngazi fulani au hapo ndio mwisho wa reli kisha wanaingia mtaani wakajijue huko?

    5.Sehemu/kwenye mafunzo kama haya wafunzwa wa jinsia ya kike hua wanawakati mgumu aidha wajirahisishe kwa ngono au walazimishwe na wakufunzi kufanya hivyo, je huko hali ikoje kwenye hili swala.

    6. Labda kama nimeona vibaya, hiikambi ilikua ya wanaume tuu, au hazitakiwi kuchanganywa jinsi zote mbili?

    7.Naona wahitimu woooooote na huyu aliyeshika jambia wamekuja mikono ya sare/uniform zao, kwani hakuna sare za mikono mifupi kama ya huyo mkuu wa kikosi, au hio ndio sheria?


    Ni hayo tuu ningependa kufahamu, ni mimi kijana wa leo ambaye ningependa kwanda kuchangamsha mwili na akili huko. Aksante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...