ANKAL,
JANA NILIFIKA OFISI ZA TANESCO KINONDONI MAJIRA YA SAA 2 KAMA AMBAVYO NILIAGIZWA NA DADA WA RECEPTION KWA AJILI YA KUPATIWA ‘SURVEYOR’ WA KWENDA NAE KUFANYA TATHMINI YA NJIA YA UMEME NYUMBANI KWANGU. BAADA YA KUMPA KADI YANGU ALINIAMBIA NISUBIRI KAMA WENZANGU NILIOWAKUTA. BAADA YA MUDA TAKRIBAN DK 20 DADA HUYO KWA UKARIMU ALITUAMBIA KWAMBA MAJINA YETU YAMEGAWANYWA MAKUNDI MAWILI KWA HIYO MTU ATAKAEKUJA ‘SURVEYOR’ NA KUITA NDIO KILA MMOJA ANAMFUATE.

KWELI BAADA YA MUDA ALIKUJA DADA MWINGINE AKAITA MAJINA NA KUONDOKA NA KUNDI LAKE HATIMAE AKAJA KIJANA AKAITA MAJINA YA KUNDI LILILOBAKIA TUKAWA WATU 10. AKASEMA OFISI HAINA GARI HIVYO TUNAPASWA KUKODISHA GARI KWA KUCHANGIA WENYEWE; GAFLA AKAJA JAMAA WA GARI AKASEMA KWA KUWA RUTI INAANZIA TANGIA BOVU, TEGETA ,MADALE , BOKO, BUNJU NA MBWENI KILA MMOJA ATATOA SHILINGI ELFU 9,000/= MARA WATU 10 NI SHS. 90,000/=! KILA MMOJA ALISHIKWA NA BUTWAA.
HII INAONEKANA NI UTARATIBU WAKAWAIDA KABISA NA PICK UP ZINAZOPAKI NJE NI MRADI WA WATU WAFANYAKAZI WA TANESCO.JE, NI KWELI TANESCO HAWANA MAGARI NA HAYO TUNAYOYAONA YANAFANYA KAZI GANI? KWA UTARATIBU HUU NI WATU WANGAPI WATAMUDU KUWEKA UMEME? ITAKUWEJE BAADA YA TANESCO KUONGEZA GHARAMA ZA KUWEKEKEWA UMEME;
WADU MNASEMAJE?
-MDAU ALIYELIZWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Bleeding a leech to fatten a heifer!

    Watatukamua mpaka watumalize!

    Watanzania tuamke ikiwezekana hata kwa maandamano!!!

    ReplyDelete
  2. Hivi tutaendelea kweli Tanzania, wenye nacho wanataka kuchuma kwa masikini. Tutatumia vibatari mpaka lini.Inaudhi

    ReplyDelete
  3. Pole habari hii inaonesha uozo uliopo sio tu TANESCO bali katika kila sekta nchi. Watu wameaznisha desturi za kuishi kijanjajanja na ukipinga desturi hizi unaonekana mkorofi.

    Tunapaswa kujua taratibu na kuwalazimasha wafuate taratibu hizo, na hiyo ni kazi kwani kuna watu wanapenda mambo ya kijanjajanja na ndiyo wanawapa kichwa Tanesco.

    ReplyDelete
  4. this is too much watanzania! Kwanza ni kwa nini unatakiwa kwenda ofisini kumchukuwa surveyor? ingelikuwa rahisi zaidi kama surveyor anapewa list yake na usafiri wake kwenda katika sehemu husika. Hii ni kazi yao na ni wajibu wao kufika kunakohusika na sio wajibu wa client.

    Lakini tanzania tushazoea na hatutobadilika, polisi hafiki kukamata mwizi kwa sababu hana gari au gari halina petroli.

    si muda basi na wakusanya taka itabdi tukawachukue ofisini ili wakafanye kazi zao!!!!

    ReplyDelete
  5. tafadhali naomba mnisaidie kujaza 'survey' hii.

    bonyeza hapa

    http://www.eSurveysPro.com/Survey.aspx?id=9428fa04-ee10-4519-abdb-dcf3f95b135b

    shukrani sana kwa muda wako.

    ReplyDelete
  6. Tafadhali naomba utumie dakika chache kujaza hii 'survey'. Inahusiana na huduma za TANESCO kwa wateja.

    bonyeza hii link hapa chini.

    http://www.eSurveysPro.com/Survey.aspx?id=9428fa04-ee10-4519-abdb-dcf3f95b135b

    Shukrani sana kwa muda wako

    ReplyDelete
  7. HII KITU NI KAWAIDA KWA JAMAA WA TANESCO IPO ZAIDI YA MIAKA 15 TANGU WALIPOKUWA OFISI ZAO ZA ZAMANI PALE NYUMA YA USALAMA WA TAIFA !

    ReplyDelete
  8. Du wizi wa mchana wa jua kali. Kaka ulietuma huu ujumbe, ingekuwa vyema sana wakati mkitajiwa hiyo plan ya uchangishaji wote mngekataa na badala yake wote mngeomba kuonana na mkuu wa huyo mtumishi ama hata MKURUGENZI wa tanesco kuzungumza nae juu ya huo uozo, hiyo ndio njia pekee ya kukomesha wizi wa hao wanaTanesco. Ama wakikataa basi wawaandikie risiti za hiyo transportation ikiwa na saini ya mtu wa tanesco ili muweze kufuatilia hilo jambo kunakohusika, ikiwezekana hiyo risiti ipostiwe kwenye hili jamvi la michuzi ama gazeti lolote kubwa la hapo mjini. Msikubali kuburuzwa kama mbuzi.

    ReplyDelete
  9. muusika aliyotuma habari hii tungeomba uwataje hao surveyors ili wajulikane na jamii.

    ReplyDelete
  10. Hawa Tanesco wanabebwa sana na serikali yenyewe mi nashangaa kwanini tunakampuni moja tu ya umeme ime-monopolose market ndo maana wanafanya mambo ya ajabu. kama watanzania ni lazima ifike mahali tutafute njia ya kutatua hili. kwana umeme wenyewe wanatuwashi utafikira trafic lights! wanazima na kuwasha bila taarif as if hawatambui kuwa mamia ya wananchi mali zao zimeharibika kwa kukatiwa umeme mara kwa mara tena bila notice.

    ReplyDelete
  11. HAWA'SURVEYORS' NI WAFANYAKAZI WATANESCO WALIOKUWA ZAMU TAREHE 4/01/11. NI RAHISI KUPATA MAJINA YAO PALE FRONT DESK KWANI MPANGO MZIMA HUANZIA PALE

    ReplyDelete
  12. Tanesco = CCM = Ubababe = wataendelea kutesa madarakani forever.

    Solution:
    1. Tumieni mtu wa TARUKUKU kwenda kama mteja ili kunasa hao wahuni.

    2. Mwananchi mmoja tu akae nje ya jengo na camera mkononi akiwa amejificha kidizaini pindi hao wahuni wakitoka nje na kuchukua wateja tayari kuwapandisha kwenye teksi bubu basi wapigwe picha ikiwezekana videos kisha zibandikwe kwenye huu mtandao ili waumbuke.

    Tatizo litakuwa kwishney.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...