Mcheza gofu wa siku nyingi na mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Chris Kamuzora amefariki dunia jioni hii baada ya kuangukiwa na mti akiwa mchezoni kwenye viwanja vya gofu vya klabu ya Gymkhana jijini Dar.
Taarifa toka Gymkhana zinasema marehemu alikuwa mchezoni na rafikiye wa karibu Profesa Mohabe Nyirabu, pamoja na wachezaji wengine Ally Hamisi, Michael Makala na Athumani Chiundu kabla ya mti katika ya miti mingi uwanjani hapo kuwaangukia.
Habari zinasema Profesa Kamuzora alikuwa amebanwa vibaya sehemu ya kichwa na alikimbizwa hospitali akiwa mahututi. Baadaye kidogo taarifa ya kufariki dunia zikaja.
POLENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI. KATIKA WAKATI HUU MGUMU. MUNGU AMSAMEHE KWA MABAYA ALIYOTENDA NA AMBARIKI NA HAMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMINA. NAWAPA POLE SANA MIMI MWANGAJAMII KUSHIRIKIANA NA ISSAMICHUZI. KWA KWANI MUNGU ALITWAA NA WMECHUKUA KILICHO CHAKE.
ReplyDeleteR.I.P Prof Kamuzora tutakukumbuka sana kwa ujuzi wako, Huyu ni mwalimu wangu pale UDSM Bcom 2008. Alitufundisha Statistics na nakumbuka alikuwa anatuambia katika field yake yuko peke yake East & Central Africa. Dah tumepoteza lulu.
ReplyDeleteMungu awape faraja ndugu na jamaa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Amen
wana kanyigo poleni mke watoto wa marehemu na watanzania kwa jumla pamoja na wanafunzi waliopitia kwake pale mlimani.tukubali mapenzi ya mungu ni zaidi.
ReplyDeleteRest in peace dear Prof Kamuzora! Sitaweza kusahau mbinu zako za ufundishaji ukitumia laptop yako ambayo enzi hizo ilikuwa rare item. You knew your stuff and wondered why we could not grasp easily your stuff. But you had a funny side too in class, which made us laugh instead of being stressed out, even in difficult situations. I really remember those days and could picture you in your chair in front of our class with your laptop showing us population pyramids and so on. We surely will always miss you my dear Prof..
ReplyDeleteNi mimi mwanafunzi wako wa Demography mwaka wa BSc Gen 1992-95.
Jamani kweli kifo hakina huruma,Marehemu Ongala aliimba, yaani mti hauaungiki hadi umsubiri Prof.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
RIP Prof nami ulinifundisha Mlimani enzi hizo 2005.
ReplyDeleteThis is terrible...rest in peace Prof...we will always remember you at those times at UDSM..Mh this is hard to believe. RIP
ReplyDeleteOoohh..Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu. Amina. So sad jamani, mwalimu wangu wa Demography... He was so lovely man. duh! yaani im speechless..kifo kweli hakina huruma. Moshiro, M
ReplyDeletePole sana professor, mimi mwanafunzi wako nimeshindwa kujizuia machozi yamenitoka, nipo ughaibuni nakula nondozz ya PhD ila bila wewe na walimu wenzako nafiri wengine tusingefika huku.
ReplyDeleteYou will always be missed, RIP prof
Asante kaka michuzi kweli hii ni blog ya jamii kwa breaking news mpo juu
ameacha ombwe kubwa katika fani ambayo kwa kweli ni watanzania wachache kama sio yeye peke yake aliyebobea! Mungu amlaze mahali pema peponi.
ReplyDeleteKaka michuzi ombi, huyu professor ametufundisha wengi ambao tupo ughaibuni sehemu mbali mbali naomba hii posti uhiweke hapo juu kwa siku nyingine moja ili wadau waendelee kutoa salamu za rambi rambi, nitawajulisha UDASA waje kwako wazichuke waweke kwenye kitabu cha maombolezo cha kumbukumbu.
ReplyDeleteMwalimu wangu RIP
Asante blog ya jamii mbarikiwe
MUNGU AWAFARIJI WAFIWA WOTE,JAMAA NA MARAFIKI,NINAMKUMBUKA PROFFESOR ALITUFUNDISHA STATISTICS KWENYE MIAKA YA 1990,ALIKUWA MCHESHI,NA ALIKUWA MWALIMU AMBAYE KWA KWELI HUWEZI KUCHOKA KIPINDI CHAKE ANAPOINGIA LECTURE ROOM.
ReplyDelete