Afisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha Nyota moja wa jijini Mwanza ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake,akizungumza na madereva na makondakta wa daladala waliogoma kufanya kazi leo wakishinikiza kupandishwa kwa nauli kutoka sh. 250 mpaka 300 kutokana na gharama za mafuta kupanda sana.hii imetokea leo hii katika viwanja vya Furaha maeneo ya Kirumba.hali hiyo imewalazimu wakazi wengi wa jiji hili kutembea kwa miguu au kutumia usafiri wa pikipiki maarufu kama boda boda huku wengine wakilazimika kushushwa katika daladala zilizokuwa zimepuuza mgomo huo.
Madereva na Makondakta wa daladala hizo zilizogoma wakimsikiliza kwa makini jamaa mmoja aliejitambulisha kuwa yeye ni afisa wa serikali lakini hakutana jina lake wala idara anayotokea,na baada ya kugundua kuwa hakuwa na kitambulisho walimpuuza na kumtaka aondoke eneo hilo kwani hawezi kuwasaidia lolote.
Wazee wa kazi walifika eneo la tukio na kusikilizia kama kuna lolote wanaloweza kukabiliana nalo,lakini haikuwa hivyo na baadae wakaondoka zao.
Madaladala yakiwa yamepaki katika uwanja wa Furaha maeneo ya Kirumba,jijini Mwanza leo
hapa hakieleweki kitu mpaka hatma yao ipatikane huku mama na watoto zake wakipita katika eneo hilo la mgomo.
hapa hawataki kusikia la yeyote,mpaka serikali iwape hatma yao.
Hapa wakilizua moja ya daladala lililokuwa likipakia abiria na kumuamuru dereva kuweka gari yake uwanjani.
Vikao vya hapa na pale vikiendelea.
Wakazi wa Mwanza wakitembea.
Wanafunzi pia wakitembea.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...