Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi na baadhi ya wabunge wa chama hicho, walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama Jumapili hii.
Mama Maria Nyerere akiteta jambo na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati viongozi wa Chama hicho na baadhi ya wabunge, walipomtembelea nyumbani kwake Butiama.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.Picha zote na mdau Joseph Senga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hawa nao wanahangaika! waone na magwanda yao! Ona mama maria amewatilia CCm ha ha ha!

    ReplyDelete
  2. hongereni sana kwa kutambua mchango wa baba wa taifa katika taifa hili sasa likiwa kijana na pia hongera mama maria kwa kusonga mbele ki umri na kuendelea kutukuka pia najua utakua umewapa somo vijana wako juu ya siasa za mwalimu nafikiri hipo siku nawe mama maria utavaa hizo granda za chadema sio mbaya leo ukavaa hizo za kijani

    ReplyDelete
  3. Pamoja na Kuwaheshimu Ndugu zetu wq CHADEMA, naomba niwape ushauri wapunguze siasa kidogo waanze kufanya kazi walizotumwa na wananchi waliowachagua, Miaka mitani si mbali sana watakuja jutia muda walioupoteza

    ReplyDelete
  4. kufanya kazi za Umma kama Ubunge na Uwaziri, si kuvaa suti na kukaa Dar es saalam, au mijini kweye viyoyozi.ni kuangalia mazingira husika na kushirikiana na wananchi walio kuchagua ili ujue kinachowasibu na ukipatie ufumbuzi yakinifu. kwahiyo kuvaa magwanda si kosa bali ni kuonesha wapo kikazi zaidi.

    ReplyDelete
  5. Kazi gani wanayoifanya sasa zaidi ya kuvaa magwanda na kuandamana? Huko kuandamana ndio kutatua kero za wananchi zilizoko majimboni mwao? Mbona siwaelewi? Kama jimboni kwetu kuna tatizo la maji, kuandamana kutatuletea maji? Kama kuna tatizo la shule, vyumba vya madarasa au makazi duni kuandamana kutaondoa hayo matatizo?

    Nyie CCM na wabunge wake sikilizeni niwape ushauri wa bure, yale majimbo yaliyochukuliwa na Chadema mkiyataka mtayapata kirahisi wakati wao wanazurura kula hela ya Sabodo nyie nendeni mkafanye kazi za jamii kwenye hayo maeneo, fanyeni kazi huko kwa kutumia pesa kutoka kwenye serikali yenu iliyoko madarakani na hata kwa miradi mnayoweza kuivumbua pamoja na wananchi na mkapata ufadhili kwenye mashirika na NGO za kimataifa. Piga mzigo kwa kwenda mbele, wakistuka ni 2015 hawana pa kushika. Ila kwa jimbo la Zitto Kabwe sidhani kama inawezekana the guy is using the above strategy!

    ReplyDelete
  6. Mama Maria kweli wewe ni kiboko yaani umewavalia kabisa sare ya CCM? Watu wenye akili zao wanaelewa ulikuwa unawaambia nini hao vijana, maana wewe hao kina Mbowe unawafahamu vizuri sana tangu enzi ya Mzee wao, imani yao na kwako ni vitu viwili tofauti hao ni mabepari na wewe ni mjamaa! Waache wavae sare zao za mabepari. Walitaka kukutumia kama mtaji kwenye maandamano yao lakini umewawahi!lol!

    ReplyDelete
  7. hakuna shida kuvaa magwanda. hata hivyo hawakuenda kumbadilisha mama maria itikadi. hiyo nguo ni ya kijani na haijaandikwa CCM.ajabu leo michuzi umetupa kitu hiki. tutaanza kukutembelea tena.

    ReplyDelete
  8. hongera chedema kwa kuthamini mchango wa baba wa taifa, wengine wamesahau mchangao wake wanafanya wanavyotaka

    ReplyDelete
  9. kuvaa magwanda si kosa, ni alama yao ya utambulisho wameamua kuchagua, kama wengine walivyochagua kofia, fimbo, nk,chadema chapa mwendo ule ule, kazi tunaiona, kwenye habari ya leo tunamuona Lema Arusha anafanya mambo, na kwa kumtembelea Mzee Nyerere, natumaini naye ametambua na anaikubali kazi yenu huko huko aliko!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...