Taasisi ya hisani ya DYCCC ni chombo cha hapahapa nchini chenye kujishughulisha sana katika kusaidia jamii hususan katika nyanja ya Afya, Elimu na Ustawi wa jamii kwa ujumla.
Ajali ya milipuko katika kambi ya jeshi ya gongo la Mboto usiku wa tarehe 16 Februari 2011 imewaathiri raia wengi waishio maeneo ya jirani na kambi hiyo na kwingineko. Kwa bahati mbaya watu kadhaa wamepoteza maisha na wengi zaidi kujeruhiwa na wengine kupoteza makazi na mali zao.
Leo asubuhi tarehe 18 Februari 2011, Katibu Mtendaji wa DYCCC, Ahmed Saggaf alikabidhi bidhaa kadhaa kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Mecky Sadick kama msaada wao kwa waathirika wenye thamani ya jumla ya shilingi milioni thelathini na sita, kama ifuatavyo;
- Robota 60 nguo
- Mashuka 400
- Mito 100
- Tani 3.5 mchele
- Katoni 250 (za Kilo 12) tende
Makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya Sabasaba na kuhudhuriwa na Wakuu wa Wilaya wote watatu wa DSM, Wabunge wa DSM Mussa Zungu, Dr Ndugulile, Abbas Mtemvu, Zarina Madabida, Mariam Kisanga, Makongoro Mahanga, RPC Kova na madiwani kadhaa wa DSM. Ujumbe wa DYCCC uliwajumuisha pia wajumbe wa Kamati ya Zakaa na Sadaka, Saleh Akrabi, Aziz Al Hassan na Salum Al Jabry.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...