MAREHEMU GEORGE A. SENERWA

Leo tarehe 10/02 /2011 umetimiza mwaka mmoja tangu ulipo tutoka kipenzi chetu George A Senerwa. Hakika umetuacha na simanzi kubwa, umetuacha na majonzi ewe mpendwa uliyekuwa kiungo na kila kitu katika familia. Unakumbukwa sana na marafiki zako,wafanya kazi wenzako,ndugu zako na zaidi mtoto wako wa pekee Abigail George.
Tutaendelea kukupenda,kukumbuka na kukuombe zaidi ya sana

Fortunata Getele- Mkeo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Rest in peace George, niliposikia habari ya kifo hiki nilisikitika sana, alikua na moyo wa upendo na kusaidia pia. Fotu, Mungu akupe nguvu, amani na ujasiri, maombi ndo silaha yako, usiache kuomba. Abigail, Mungu ni baba wa wote, atakulea.
    Tulikua wote shimiwi 2008

    ReplyDelete
  2. Pumzika kwa amani George. Sote tu njia moja, umetutangulia, tutafuata. Jipe moyo Fortu mdogo wangu, yote ni mipango ya Mungu. Mungu akujaalie hekima na busara ya kumlea Abigail vema. Tuombeane daima. Mimi dada yako Veronica Simba.

    ReplyDelete
  3. mungu alikuchukua wakati ulikua msaada mkubwa sana kwetu hasa ulivyokuwa mcheshi kwa kila mtu na ulipenda sana kujituma kwa kila jambo kwakweli niliposikia nilistuka sana mungu akulaze pepa peponi na shem kaza moyo mungu akutie nguvu na ujasiri kwa kila jambo unalofanya kimwili auko nae hila kiroho anakuongoza george.
    -makwinya india

    ReplyDelete
  4. Poleni sana na msiba. Mungu wa faraja azidi kuwafariji.Naomba kuuliza kama marehemu alikuwa Kibaha secondary mwanzoni mwa miaka ya 1990.Kama ni yeye;alikuwa mwanafunzi mwenzangu.Nasikitika kusema imepita mwaka sasa ila mi ndio najua leo kwamba hatuko naye tena, pole sana shemeji na mwenetu Abigail.
    RIP wajina!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...