Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mama Chiku Shomari akimshukuru Mungu ofisini kwake baada ya kustaafu rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Mzee Shomari akimzawadia mkewe mama Chiku Shomari kwa kumaliza na kustaafu salama kazi kwenye mlango wa Ofisi ya Utamaduni wakati anaondoka rasmi leo jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Itenda -Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera mama Chiku.Nakukumbuka sana kwa busara na nasaha zako nilipokuwa nawe darasa moja pale Institute of social work darasa la 2000-2003.Mtukuze mwenyeenzi Mungu kwa kukujalia afya njema hadi unapotimiza ngwe hiyo ulioibeba miaka mingi ukilitumikia Taifa.

    Nakutakia maisha bora ya kustaafu Mungu akujaalie afya njema unapopumzika.

    Mchungaji

    ReplyDelete
  2. sikujua ameolewa na muarabu mama Shomari,hongera sana umelitumikia taifa kwa muda mrefu toka ukiwa wilayani temeke,ualimu, chaneta mpaka wizarani nakutakia retirement njema.

    mwana netiboli.

    ReplyDelete
  3. Mama NyanzoMarch 01, 2011

    Wifi,
    Nakupongeza sana. Sio mchezo maana Mtu unapostaafu unamshukuru Allah kwani huku makazini kuna a lot of challenges.
    Nakuombea Mwenyezi Mungu akupe kila la kheri katika maisha yako mapya.

    Wifi Sande

    ReplyDelete
  4. Mtu ukitaja CHANETA basi una maana Mama Chiku Shomari aliyeijenga, kuilea na kuikuza CHANETA. Auntie Chiku tunakutakia kila kla heri wewe na familia yako. Mdau wa michezo.

    ReplyDelete
  5. Basi hilo ndio tatizo lenu "wabara" sio wote baadhi, hivi ulishawaona au kuwasikia wabondei, na warangi hawa warangi ni waarabu kabisa. Tatizo lenu ni kanzu na kofia yale yale na ni ule ule udini unozungumzwa. PREJUDICE AND IGNORANCE, itatupeleka mahala pabaya. Siku moja nilikwenda CCBRT kupima macho, basi kila daktari akiniuliza namwambia naona vivuli eti alikata tamaa akaanza kuzungumza na daktari mwenzake problem zangu kwa english. Mimi nikamwambia "talk to me, I am the patient here" alishtuka, yote kwa sababu nimevaa mtandio. Huyu ni Daktari sasa wa mtaani sijui itakuwaje. Huu ni ujinga mkubwa sana. Nawaonea huruma.

    ReplyDelete
  6. Inahusu nini kuolewa na mwarabu na hii picha! as the lady upstairs mentioned ni kwa sababu ya kanzu sio? siku hizi Kanzu nazo zimesoma kwa taarifa tu fupi! msione watu wamevaa kanzu au mitandio mkawadharau mtaumia!!!!...ipo siku TUTASHINDA KWA UWEZO WA ALLAH SWT....

    ReplyDelete
  7. labda mdau ameandika hivyo kwa sababu ya rangi ya mzee Shomari kwani he looks lighter kwa kweli na si lazima sababu iwe kanzu,(ingawa weupe pia si uarabu)kanzu ni kivazi tu yeyote anavaa.

    Issue at hand, hongera mama Shomari kwa kustaafu nakutakia kila la heri katika maisha mapya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...