WADAU NAOMBENI MSAADA WA MAWAZO AU KISHERIA

KAKA ANKAL, POLE NA MAJUKUMU

NI HIVI..KUNA JAMAA YANGU KAPATWA NA MATATIZO. ALIKWENDA KWENYE VYAMA VINAVYO WASAIDIA WANAWAKE KISHERIA, ALIKUWA NA TATIZO LA MZAZI MWENZIE KUMTELEKEZA BILA MATUNZO YA WATOTO WAO WAWILI. NDIPO ALIPOENDA KUOMBA MSAADA KISHERIA. NA YEYE KWA SASA YUPO NYUMBANI BAADA YA KIBARUA CHAKE KUOTA NYASI.

ALIFIKA KULE KWENYE HIVYO VYOMBA VYA KISHERIA WAMKAMPA BARUA YA KUPELEKA MAHAKAMANI( KINONDONI). KAFIKA, KILA KITU KIMEENDA SAWA. ILA ILIPO FIKA WAKATI WA KUPEWA BARUA YA KWENDA KUMKAMATA MTUHUMIWA, ALITAKIWA APELEKE KWENYE OFISI NYINGINE HAPO HAPO KWENYE MAJENGO YA MAHAKAMA NA ALIAMBIWA MUONE MTU FLANI(JINA KAPUNI). HAPO NDIPO TATIZO LILIPOANZIA.

YULE MTOA HUDUMA ALIPOKEA HIYO BARUA KUTOKA KWA WAKUU WAKE WA KAZI NA ALIPOISOMA TU ALIULIZA KWANI KWA MTUHUMIWA NI WAPI? AKAJIBIWA ILALA. AKAULIZA SASA TUTAWEZAJE KWENDA ? HUYU JAMAA YANGU AKAMWAMBIA MIMI NIPO TAYARI NIKAKUONYESHE....MTOA HUDUMA AKULIZA TUNAENDAJE NA AKAJIBIWA KWA DALADALA, MIMI NI NAYO NAULI HAPA NI TSH 2,000/= TU.

BASI BWANA, YULE MTOA HUDUMA AKIRUSHA BARUA PEMBENI NA KUMWAMBIA BILA ELFU 10 UNITOI HAPA. KWANZA NINA KAZI NYINGI SANA, PIA SINA MUDA, HUKU WAFANYAKAZI WALIOKUWEMO MLE NDANI WAKIRUKIA AT KULE MBALI WEWE... TOA HIYO HIYO ELFU 10 ILI AWEZE KUJA KUANDIKA RIPOTI VIZURI.

UKWELI NI KUWA HUYU JAMAA YANGU KWA SASA NI MWEZI WA PILI YUPO NYUMBANI BILA KAZI, HIVYO MOJA HAIKAI WALA MBILI HAIKAI. HATA HIYO 2000/- YENYEWE KWAKE NI KUBWA MNO KWANI MAISHA YAMEKUWA MAGUMU SANA KWAKE.

JE, NDUGU WADAU WA GLOBU YA JAMII, NI KWELI KISHERIA ALIPASWA KUTOA HIYO ELFU 10? AU NI KAZI YA MAHAKAMA? NA JE WASIO NA UWEZO WA KUWA NA EFLU 10 WATAPATA MSAADA KWELI? AU NI MIMI SIELEWI MAMBO YA MAHAKAMA? NAHITAJI USHAURI TOKA KWENU ILI NIWEZE KUMSAIDIA HUYU JAAMAA YANGU

ASANTE
MDAU ALIYELEMEWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamaa yangu wewe kweli toka Kinondoni mpaka Ilala ulitaka mtu anakwenda kumkama mtu aende na daladala? Wewe mwenyewe unajua foleni za magali na hasa daladala, ulitegemea mpaka aje kubadilisha magali angefika saa ngapi. Serikali yenyewe ndiyo hiyo, idara ya mahakama unaijua ukata ilio nao, akitoa hela yake mfukoni ili akufanyie kazi kuidai itamchukua miaka, mbona alikuonea huruma kwa shilingi 10,000/= mimi nilifikiri kaomba rushwa, kumbe ni nauli tu ya taxi kwenda na kurudi 5000 kila trip. Wakati mwingine tusikimbilie kusema watu wanakula rushwa tuangalie na ukweli

    ReplyDelete
  2. I thought he get paid for doing his job or just sitting in the office,
    put his/her name ili watu wamfahamu kama kazi yake ni kutaka rushwa tu.

    ReplyDelete
  3. Pamoja na kwamba kuna matatizo kama hayo lakini hakuna taratibu kama hizo za kufuata kwa hapa Tanzania,vinginevyo alikumbana na matapeli,nijuavyo mimi shauri likifikishwa mahakamani,mahakama inatoa barua(wito) wa kuitwa mahakamani aka samansi ambyao hupelekwa na mtu wa mahakama na kumkabidhi mshtakiwa mwenyewe kwa kusainishwa,siku ya kusikilizwa kesi mtuhumiwa asipokuwepo kesi husikilizwa kwa upande mmoja na hukumu hutolewa.kwa hiyo mdau takwimu ulizotoa hazijakaa sawa ili kuweza kumsaidia mhanga wako

    ReplyDelete
  4. hiyo ni rushwa na ndio mchezo wao kwasababu wanajua watu wengi hawajui sheria na haki zao hiyo ni kazi yake kwenda kumkamata na wewe utakiwa kutoa hiyo elfu kumi kwasababu yeye analipwa na serikali kwa kazi hiyo

    ReplyDelete
  5. Matatizo mengine ni ya kujitakia. Baada ya kuambiwa hivyo kwa nini hakurudisha hiyo barua huko ilikotoka? Ili wampatie mtu mwingine hiyo kazi na ili huyo aliyekataa hiyo kazi achukuliwe hatua. Mambo ya kulea wafanyakazi wa serikali yamezidi, huyo mtu hastahili kuwa na kazi. Roho mbaya, elfu kumi yeye alikuwa na gari ili adai hiyo pesa. Mengine tunayachochea sisi raia maana wengine wanatoa hizo elfu kumi bila hata kuuliza. Jamani rushwa Tanzania mpaka lini. Lait ningekuwa na nafasi ya kuwashughulikia, mgekiona cha moto.

    ReplyDelete
  6. Mkamatishe Takukuru! Opps, sijui nao watahitaji nauli ya kwenda huko Kinondoni!?

    ReplyDelete
  7. Mambo kama haya hayatakuwepo pale Taifa la 'Ruvuma' litakapozaliwa.

    Ruvuma ni nchi itakayokuwa ikiongozwa kwa misingi ya KATIBA na Haki za Binadamu. Wana-Ruvuma mnaombwa kutulia wakati wenye uchungu na nchi yetu iliyoneemeka (iliyo tekwa kwa hila kuanzia enzi za wakoloni weupe hadi hawa wa hivi sasa) wanafanyia kazi mambo kadhaa kabla ya kuanza rasmi harakati za ukombozi wa Kusini!

    Saa ya Ukombozi ni Sasa. Tukiendelea kulala, ni nani wa kumlaumu? Viongozi magoigoi tunaowachagua kila mara ambao hufanya makazi yao PWANI, na kuja kutudhihaki kila baada ya miaka mitano kwa vijizawadi vya chumvi na tisheti hawatufai.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...