Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakizungumzia mustakabali wa kambi ya upinzani Bungeni katika kipindi cha asubuhi cha TBC 1 leo katika kufafanua kilichojiri jana wakati wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya ukumbi wa bunge kwa muda kupinga upigaji wa kura kuidhinisha marekebisho ya kanuni kinyume na matakwa yao.
Home
Unlabelled
mwenyekiti wa chadema na naibu spika waongelea mstakabali wa kambi ya upinzani bungeni leo (part 1)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ipo haja nafasi ya Uspika wa bunge la Muungano Tanzania kushikiliwa na chama kikubwa cha upinzani. Ila nafasi ya naibu spika ndiyo iende kwa chama tawala kinachoendesha serikali.
ReplyDeleteNinasema hivyo, kwani hapa Naibu Spika anaongea kishabiki zaidi kwa vile anatoka chama tawala chenye wabunge wengi. Hivyo basi ili bunge liwe huru na spika mkuu kufanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa na kwa kufuata sheria na taratibu za bunge ni vyema spika mkuu awe wa chama kikubwa cha upinzani mfano CHADEMA.
Spika toka chama kikubwa cha upinzani akiendesha bunge kimabavu na kutofuata kanuni na sheria za bunge atakuwa anabanwa na wabunge wa chama tawala, hivyo kwa utaratibu huu Spika wa Bunge la Muungano kutoka chama cha upinzani atakuwa makini.
Hii clip inaonyesha dhahiri jinsi Naibu spika Ndugai (CCM) anavyojivunia wingi wao bungeni na kuwa tayari kukibeba chama tawala kutokana na wingi wao.
CHADEMA wanajua kutumia kipengele cha kupigia kura CCM wanaweza kupitisha chochote kile ili mradi kina manufaa kwa CCM na siyo kwa manufaa ya kukuza demokrasia itakayozaa mijadala yenye manufaa kwa taifa.
Mdau
Mwananchi Makini
In my humble opinion, I think Chadema DO have a point.
ReplyDeleteMdau London.
hoja yangu kubwa kuhusu mjadala huu nikuwa KWANINI SWALA LA UPINZANI LIJADILIWE NA CHAMA TAWALA? KAMABI YA UPINZANI NI SWALA LA VYAMA VYA UPINZANI. dunia nzima inalielewa hili, wabunge wa chama tawala hawasishwi kwenye mijadala hasa ya uongozi wa kambi ya upinzani bungeni. unapo wapa chama tawala fursa ya ya kujadili swala la upinzani bungeni nikuwa funika kimamlaka upinzani.
ReplyDeletenimalize na swali NIWAPI UMEONA CHAMA CHA WABUNGE WACHACHE KIKIONGOZA KAMBI YA UPINZANI, AU CHAMA TAWALA KUWA NA MAMLAKA YA KUTUNGA SHERIA JUU YA UPINZANI. hii sio demokrasia
Mhe. Dr. Ndugai, kwanza ushauri mdogo tu: pamoja na kwamba wewe ni mwanachama na mbunge wa CCM lakini angaa jaribu kuji-pritend kuwa impatial mbele ya umma unapokuwa unazungumza kama NAIBU SPIKA!!!
ReplyDeletePili, Ni lini CCM ilitambua kuwa umma unahitaji katiba mpya? Kama kweli CCM ilikuwa inatambua haja ya mabadiliko ya Katiba, mbona haikuiingiza katika Ilani yake ya uchaguzi wa mwaka jana wala mgombea wake wa urais kugusia hoja hiyo wakati wa kampeni? Lakini mwezi mmoja baada ya uchaguzi, ndio Mhe Dr. JK akatangaza kukubaliana na madai ya umma kuhusu mabadiliko ya katiba. Kwa hiyo tunaweza kukubaliana na Mh. Mbowe kuwa ukitaka CCM wakusikilize inabidi kufanya 'nguvu ya ziada'!! Ninawapongeza CHADEMA kwa kuibana CCM na serikali yake na pia ninampongeza Mhe. Dr. JK kwa kupata 'ujumbe' na kuonyesha nia ya kuufanyia kazi hata ka
Watanzania tuna safari ndefu sana kufikia demokrasia ya kweli..
ReplyDeleteHuyu Mh naibu spika mbona haongei kama kiongozi wa bunge. Nilidhania ukishakuwa spika au naibu spika, then hapo unakuwa unalitumikia bunge na sio chama cha siasa tena. Nafikiri Mh Mbowe yuko right kabisa kuwa hadi hivi sasa bado kuna wabunge ambao bado ni waoga sana kusema kitu chochote bungeni kinachoenda kinyume na matakwa na chama chake.
ReplyDelete