Mzee Yussuf
NI rasmi sasa kuwa Mfalme wa taarab nchini Mzee Yussuf anarudi jukwaani na onyesho lake la kwanza kabisa ni katika mkesha wa Valentine Day, Jumapili 13/2/2011ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.

Mzee Yussuf aliyekuwa nje ya jukwaa kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia operesheni ya goti aliyofanyiwa katika hospitali ya Dk Baki huko Kibaha, atafanya makamuzi hayo na kundi lake la Jahazi Modern Taarab ambapo atatumia fursa hiyo kutambulisha vionjo vyake vipya.

Mkurugenzi wa fedha wa Jahazi, Seif Magwaru ameiambia Globu ya Jamii kwa email sasa hivi kwamba katika onyesho hilo mwimbaji mkongwe Bi Mwanaidi Shaaban atamsindikiza Mzee Yussuf na wimbo wake "Nitakufa kwa ahadi"

Aidha Magwaru ameongeza kuwa onyesho la pili la Mzee Yussuf litakuwa Jumatatu 14/2/2011 siku ya wapendanao katika ukumbi wa Bulyaga, Temeke.
"Mambo mengi yamezungumzwa juu ya afya ya Mzee Yussuf ikiwemo kuzushiwa kifo, lakini hakuna haja ya kuandikia mate, mashabiki waje kwa wingi katika maonyesho hayo mawili washuhudie wenyewe maendeleo ya mwimbaji wao kipenzi" alisema Magwaru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. we Mzee hiyo staili yako ya kubeba mifunguo kama bwana jela haipendezi,kuna siku sarawili itavuka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...