SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA WATANZANIA WENZETU WALIOATHIRIKA NA MABOMU GONGO LA MBOTO
Jumuiya ya Watanzania United Arab Emirates (TAE) kwa masikitiko na huzuni kubwa inatoa SALAM ZA RAMBIRAMBI kwa wafiwa wote ambao wamepoteza NDUGU, WAZAZI, WATOTO, WENZA WA MAISHA, JAMAA NA MARAFIKI kwa msiba mkubwa uliowafika. Pia inatoa pole kwa majeruhi wote.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ahueni ya haraka majeruhi wote.
Kwa masikitiko makubwa, pamoja na kutambua kuwa hii ni miongoni mwa ajali za aina mbalimbali zinazoweza kumfika mwanadamu kutokana na vyombo na zana alizojitengenezea yeye mwenyewe. Kwa kuwa ajali imetokana na zana za kisayansi basi ni wazi kuwa kipo chanzo cha kisayansi kilicho sababisha ajali hii. Ni imani yetu kuwa hatua za haraka zitachukuliwa kuzitambua sababu hizo na suluhisho la kudumu litapatikana ile kuliepusha Taifa na majanga yanayoepukika.
Mwisho tunarejea tena kuwaombea marehemu wote, tunawatakia ahueni ya haraka majeruhi na kuwaomba viongozi waliokuwa na dhamana mbalimbali kutimiza dhamana zao kwa umakini wa hali ya juu kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa kiusalama.
Jumuiya ya Watanzania UAE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...