Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi Uingereza , Shina la CCM Reading na vitongoji vyake, tunapenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa, kutoa rambirambi zetu kwa familia za wananchi waliopoteza wapendwa waokatika ajali ya mabomu yaliyolipuka katika kambi ya jeshi eneo la Gongo La Mboto, Dar-es- Salaam , Tanzania .
Tunawaombea wote waliopoteza maisha yao Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani;tunawatakia majeruhi waugue pole, wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao zakila siku. Vilevile, tunawatakia wote waliopotezana na ndugu zao hususan watotowaliopotezana na wazazi wao waweze kupatikana na kukutana tena.
Tumesikitishwa na taarifa za maafa hayo na kuhuzunishwa kuona kwamba ni mara ya pili tukio kama hili linatokea nchini kwetu. Wengi watakumbuka janga kama hili lilitokea kule Mbagala. Tunapenda kuuomba uongozi wa jeshi uangalie upya namna silaha kali zinavyohifadhiwa; katika utaratibu wa kuhifadhi mabomu, tunapendekeza yafanyike marekebisho yatakayozingatia usalama wa raia.
Katika kuhitimisha, tunalisisitizia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lichukue hatua madhubuti na za haraka katika kuhakikisha majanga yanayoweza kuepukika kama haya hayatokei tena.
Mungu Ibariki Tanzania .

SHINA LA READING MPO SAFI KABISA,VIONGOZI WENU TUMEWAPENDA HASA ANAYETUPA UPDATE .JE TAWI WANA SHIDA GANI?LIMEKUFA?
ReplyDelete