KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE, WANACHAMA WA CHADEMA TAWI LA RED DEER, ALBERTA - CANADA WANATOA SALAMU ZAO ZA RAMBIRAMBI NA POLE NYINGI KWA WATANZANIA WENZETU WALIOGUSWA NA TUKIO LA KULIPUKA KWA MABOMU HUKO GONGO LA MBOTO MJINI DAR ES SALAAM. HABARI HIZI ZIMEPOKELEWA KWA MASIKITIKO MAKUBWA NA ZIMEMGUSA KILA MMOJA WETU KWA NJIA MOJA AU NYINGINE. TUNAWAOMBEA WOTE WALIOPOTEZA MAISHA, NA PIA KUWAPA POLE NA KUWATAKIA KUPONA HARAKA WALE WOTE WALIO JERUHIWA NA MLIPUKO HUO. HALI KADHALKA, TUNAWAPA POLE PIA WALE WOTE WALIOPOTEZA MALI ZAO NYINGI NA ZA THAMANI.
NI MATARAJIO YETU KUWA SERIKALI ITAWAANGALIA KWA KARIBU WALE WOTE WALIOGUSWA NA JANGA HILI. HATA HIVYO, WANACHADEMA WA RED DEER WANASHAURI KUUNDWE MFUKO MAALUMU AMBAO UTAWEZESHA WATANZANIA NA MARAFIKI ZETU KUUCHANGIA ILI KUWEZA KUWASAIDIA NDUGU ZETU WALIOATHIRIKA VIBAYA NA JANGA HILI.
NI USHAURI WETU PIA KWA JESHI LETU KUANGALIA UPYA JINSI YA UHIFADHI WA SILAHA KALI ZA KIVITA NA KWAMBA ZITAHAMISHWA KUTOKA MAENEO YA KIRAIA ILI KUWEZA KUZUIA JANGA KAMA HILI LISIJIRUDIE TENA, KWA MARA YA TATU. TUNATEGEMEA PIA SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA KALI NA KUWAWAJIBISHA WALE WOTE WALIOZEMBEA NA KUSABABISHA KUTOKEA KWA MAAFA HAYA.
MUNGU AZILAZE PEMA PEPONI ROHO ZA WALE WOTE WALIOTWALIWA KWA MAAFA HAYA, AMEN.

CHADEMA - RED DEER - ALBERTA, CANADA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa kweli inasikitisha sana jamani,Tunamuomba Mungu awape nafuu haraka wale wote waliojeruhiwa.Mwenyenzi Mungu awalaze mahali pema peponi wale wote waliopoteza maisha yao.
    Mdau Calgary.

    ReplyDelete
  2. Ankle pole na kazi..
    Mimi pia naungana na watanzania wenzangu popote walipo duniani kuwapa pole wenzetu waliokumbwa na majanga ya mabomu..
    lakini nataka kuuliza je hizi rambirambi toka Erading,Italia Canada na kwingineko je zinaambatana na misaada au ni maneno tu ilimradi tujionyeshe kuwa tuna uchungu wa ndugu zetu..hivi vyama vinapaswa kuchangishana na kupeleka misaada japo uhakika wa misaada yenyewe kuwafikia walengwa nao una utata manake nchi yetu hii nayo haivumi lakini imo..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...