Kampuni yake kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea katika kambi ya Jeshi Gongolamboto Jijini Dares Salaam:Na hivyo kumfanya kuamua maamuzi ya haraka kama yafuatayo.
1. Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15599 kupitia mitandao yote.
Ujumbe huu utatozwa shilingi 1000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga. Red alert itawasha rasmi kesho ijumaa tarehe 18.
2. Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji kwa siku nzima ya ijumaa kwa wahanga zaidi ya 1000 waliopo Uwanja wa taifa ambao wengi wao ni watoto
3. Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga. Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika. Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 0767111403
4. Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi. Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu mbalimbali
If you can't feed a hundred people, then feed just one - Mother Teresa.
ReplyDeleteHONGERA KWA HATUA NZURI NA YA KUIGWA, MIMI NASHAURI PESA ZITAKAZO CHANGIWA AU CHANGWA KWA MFUKO HUU WA MAAFA ZISIPITE SERIKALINI, KWAKUWA NI NYINYI VODAFONE MLIOANZISHA MFUKO HUO KWANINI TENA MUIPATIE PESA SERIKALI, NYIE WENYEWE KAMA VODAFONE MKUSANYE PESA NA MFANYE MPANGO WA KUJUA WAHUSIKA NA KUWAPA KITAKACHOPATIKANA. WASIWASI KUNA WATU HUWA HAWANA HURUMA,HAWAJUHI WATU WAMEPOTEZA MAISHA AU MALI ZAO ZIMEHARIBIWA NA MILIPUKO HII, WATAKULA PESA JAMANI- KUFA KUFAANA, WATOA MISAADA WA NGO'S SIKU HIZI WANAKUJA MOJA KWA MOJA HAWAPITI SERIKALINI KWAKUWA WAMESHAJERUHIWA.
ReplyDeleteVILE VILE BADO HAMJATUAMBIA SISI TULIOKUWA MBALI NA TANZANIA JINSI GANI TUNAWEZA KUCHANGIA KWENYE MFUKO HUO WA MAAFA,
MDAU MPENDA HAKI.
Mimi napenda kuungana na anon wa Feb 17, 06:12:00
ReplyDeleteJAMANI INASIKITISHA SANA HEBU FANYA NDO UMEPIGIWA SIMU FAMILIA YAKO IMEANGAMIA NA BOMU NA HAWANA PA KULALA,HIZO ROHO ZA WATU ZINATEKETEA MALI,JIRANI ZANGU NYUMBA ZAO KWISHA KABISA MAGARI YAMETEKETEA MOTO,JIRANI MWINGINE FAMILIA NZIMA KWISHA. NINI KIFANYIKE ILI TATIZO HILI SIJIRUDIE.
ReplyDeleteWADAU MKO WAPI.
Mwamvita na Uongozi wote wa Vodacom Foundation, mnaonyesha nia ya kutaka kusaidia watanzania wenzetu waliokumbwa na maafa. Lakini chonde chonde hichio kinachopatikana (hela) fanyeni mpango mwingine tofauti kabisa wa kuwasaidia wahanga na msaada huo na sio kuupitishia serikalini.wallahi hazitawafikia walengwa. tafadhali sana endeleeni na moyo huo huo wa kuwaonea imani wenzetu na tusaidiane katika kuwafariji lakini sio kwa kupitia serikali.
ReplyDelete