Na Mwandishi Maalum
New York-Kasoro kadhaa zikiwamo za upotoshaji mkubwa wa takwimu zilizomo katika Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani ya Mwaka 2010( Human Development Report) kumewafanya Wakurugenzi Wakuu wa Takwimu kutoka nchi za Umoja wa Mataifa kugeuka mbogo na kuzijia juu Taasisi zilizoandaa taarifa hiyo.
Wakuu wa maswala ya takwimu walikutana hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakihudhuria mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya UM ( UNSD). Mkutano huo wa siku nne, uliomalizika ijumaa, ulijadili ajenda mbalimbali zikiwamo hiyo ya Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani ya mwaka 2010.
Kwa ujumla hali katika chumba cha mkutano wa Kamisheni hiyo, ilikuwa ya sintofahamu, huku kila mjumbe aliyechangia taarifa hiyo, akishindwa kudhibiti hasira, uchungu na masikitiko ya waziwazi ya kutoridhishwa na namna taarifa hiyo ilivyoandaliwa huku ikiwa na mapungufu yasiyo yakawaida.
Licha ya kwamba takwimu zilikuwa ama zimekosewa ama zimepotoshwa nchi kadhaa hazikutokea kabisa kwenye taarifa hiyo.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ulijumuisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa, Bw. Mohamed Hafidhi Mtakwimu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Bi. Radegunda Maro Mkurugenzi wa Idara ya Operesheni za Takwimu.
Akichangia mjadala wa Taarifa hiyo, Dkt. Albina Chuwa anasema.“ Serikali yangu inaungana na wasemaji waliotangulia, kuhusu upotoshwaji mkubwa wa takwimu zilizoonyeshwa kwenye taarifa hiyo zikiwamo za nchi yangu Tanzania, sijui UNDP wamezitoa wapi takwimu hizi , sisi kama wenye dhamana na masuala yote yahusuyo takwimu, hatukushirikishwa ni wazi kwamba UNDP wametumia takwimu ambazo sisi hatukuziridhia na wala hazina baraka ya ofisi yangu.
Akiongea kwa hisia kali, Dkt. Chuwa amesema . “Ni wazi kwamba zoezi zima la maandalizi ya taarifa hiyo yameishia katika ukiukwaji wa kanuni na taratibu zilizokubalika kimataifa za uchambuzi na usambazaji wa taarifa za takwimu za nchi wanachama”.
Akasema kuwa Tanzania ingependa kuona, Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (UNSD) ikizifanyia kazi hoja zilitotolewa na nchi wanachama kuhusu mapungufu yaliyomo katika Taarifa hiyo ambayo ilizinduliwa mwaka uliopita.
Wajumbe wa Kamisheni hiyo wameeleza na kusisitiza kwamba, wakati wanatambua umuhimu wa Taarifa ya Maendeleo ya Binadamu kama nyenzo muhimu katika uendeshaji wa mijadala ihusuyo maendeleo ya watu kitaifa na kimataifa. Lakini wamelazimika kuelezea masikitiko yao kuhusu vyanzo vya takwimu na mbinu zilizotumiwa kuaanda taarifa hiyo.
Watakwimu Wakuu kutoka Serikali za Afrika ya Kusini, na Suriname na ambao majina yao hayakupatikana mara moja. Pamoja na kuelezea masikitiko yao juu ya taarifa hiyo. Wametaka masikitiko na maelezo yaliyotolewa na wajumbe ya kutoridhishwa na taarifa hiyo, maelezo na malalamiko hayo yajitokeze kama yalivyoelezwa na wajumbe katika majumuisho ya mwisho ya mkutano huo.
“ Ujumbe wangu unasisitiza kwamba hisia zilizoonyeshwa na wajumbe wa mkutano huu, za kutoridhishwa na taarifa hii, zijitokeze kwenye taarifa ya mwisho ya mkutano huu kama zilivyotolewa, sisi ni wataalam wa takwimu na si wanadiplomasia hakuna kupindisha lugha hapa” akasisitiza Mjumbe huyo wa Suriname. Kauli iliyoungwa mkono na wajumbe wengi.
Wajumbe wameipa miezi mitatu Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, kutoa taarifa yenye majibu ya hoja zilizotolewa na wajumbe kuhusu kasoro za taatia hiyo.
Aidha katika mambo mengine yaliyolalamikiwa na wajumbe katika taarifa hiyo ni pamoja kutoridhishwa na matumizi ya takwimu ambazo hazikuwa rasmi na ambazo zimepatika kutoka vyanzo visivyo rasmi.
Kwa sababu hiyo wamesisitiza kuwa pale ambapo takwimu rasmi zinakosekana, basi matumizi ya takwimu zisizo rasmi razima yapate ridhaa ya nchi husika.
Halikadharika washiriki wa mkutano huo, pia wameelezea masikitiko yao kuhusu utofauti na upishanaji mkubwa wa taarifa za kitakwimu kati ya Taasisi moja na nyingine ndani ya Umoja wa Mataifa. Na wakatoa wito wa kutaka kurekebishwa kwa tofauti hizo haraka.
Vile vile Watakwimu hao wamezitaka taasisi zinazoandaa taarifa hiyo ya maendeleo ya binadamu duniani, kuwasiliana na wataalamu wa takwimu wa kila nchi kabla ya kutoa hadharani taarifa hiyo ili kuepusha kujirudia kwa matatizo na makosa yaliyojitokeza katika taarifa ya mwaka jana.
Taarifa ya Maendeleo ya Watu Duniani huandaliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuzishirikiana na taasisi nyingine za kimataifa na kwa kufanya kazi kwa karibu na nchi husika kupitia Idara za Takwimu. Lakini katika hali ya kushangaza, taarifa zinaonyesha kuwa taarifa ya mwaka jana, utaratibu huo haukuzingatiwa hasa eneo la ushirikishwaji nchi husika.
Wakati huo huo, Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu, imetoa taarifa kwamba, sensa ya idadi ya watu na makazi itafanyika mwakani (2012).
Katika hatua nyingine Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe katika Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa ikiwakilisha Bara la Afrika. Tanzania itakuwa mjumbe wa Kamisheni hiyo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwakani 2012.

Hata UNDP wanachakachua taarifa za nchi! Tumekwisha.
ReplyDeleteLakini na sisi kama nchi jee tunazo hizo taarifa zinazohitajika?
Kwa mfano, kuna kipindi nilikuwa naandika ripoti fulani na nikahitaji taarifa za uzalishaji mazao kwa nchi. Ilikuwa ni kichekesho kwamba taarifa zinatoka katika Wizara moja lakini zilikuwa na tofauti kubwa sana.