ANKAL ANKAL MICHUZI.. (please usiweke email nitapewa talaka)

YAANI MADA ZA MKURUGENZI WA WABEBA BOX ZIMENIGUSA SAAAANAAA. NIMECHANGANYIKIWA NAOMBA MSAADA KUTOKA KWA WADAU NIFANYEJE


Michuzi kua mkakamavu, blog yako imeaza kuwaka moto!! Mambo yameiva.. Tulikua tunasoma mambo ya fashion basi tu.. mada za mbeba boksi zimegusa na comments zina prove.

NINA TATIZO NA NAOMBA USHAURI KWA WADADU

Mimi nimeolewa january siwezi kutaja siku kwani mume wangu anapenda kusoma blog yako. (Habari ndio hiyo Michuzi)

SASA hivi hayupo nyumbani.. toka asubuhi atoke yeye hajarudi. Sasa hatasimu yake huwa apokei kisa kelele nyingi bar eti Kuna mechi.
Huyu mtu wangu hakai ndani ya nyumba.. yaani katoka kila saa
Mara mechi, mara meeting mpaka saa tisa usiku.
Mwanaume gani au business gani mpaka saa tisa na pombe wakati wewe unafanya kazi ya serikali.
Mimi najua saa nyingine hapokei simu kwa sababu yupo na kichangudoa.. (It's so lame)
Kinachoshagaza ni hili.. hapa kwetu nimeweka dstv na beer zipo kwenye friji. Lakini yeye anasema lazima awe na marafiki zake..

Najuta sana hii ndoa sijui kama tutafika.. naogopa kila siku tukifanya mapenzi atanipa ukimwi.

Mungu wangu Mungu wangu sijui nifanye nini?????

Mada hii imenifanya nitoe machozi kabisa maana hili ndilo jambo linanitesa sana kwenye ndoa yetu.

MIMI NI MSICHANA MZURI, SINA MTOTO, NIMESOMA NA NINA MASTERS NA KAZI SAFI..

KWA MWEZI NAPATA MILIONI 5 MSHAHARA .. Lakini sina mtu anayenituliza kimapenzi.

Mume wangu nae anahela zake na sizitaki.. ila sipati nachohitaji moyoni.
Nifanye nini? Nafikiria sana niachane nae lakini familia itaona mimi kichaa.. Hasa baba na mama yangu..

Nao vilevile ni matajiri.. lakini baba yangu mambo yake yaleyale..

Wanaume badilikeni.


Kuna rafiki yangu wa zamani yupo marekani.. huwa tuna chat sana online.. yeye yupo tafauti na maneno yake ni matamu wakati wote. (HATA SASA NIPO NAYE SKYPE..)
Natamani sana ni cheat lakini mimi ni mke mwema.

Mwenzi ujao naenda marekani kusomea mambo fulani kwa kampuni nayofanyia kazi(kwa muda) nafirikiri NITATOKA NA MBEBA MOBKSI WANGU WA NEWYORK.

NAOGOPA SANA LAKINI SINA NJIA, WOTE TUTAKUWEPO KARIBU NA NAJUA TU NITALAINIKA. MAANA WIKI ZINAPITA MIMI MKAVU.

Mume wangu tayari kitambi kimetoka na tayari yuko hoi dakika mbili uwanjani.
Mbeba boksi wangu yeye ni gym kila siku na yupo fit.
I love that. mwa..

Mada safi michuzi. Asante kwa kuwa hodari.. nikikuona Regency au Nyumbani Lounge drinks on me

WADAU, KAKA ZANGU, DADA ZANGU NIFANYEJE?


Wenu Miss KV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. nenda kwa babu wa loliondo.
    P.S:Michuzi,blog yako matangazo mengi,inachosha kuscroll down,na inatia uvivu kuitembelea

    ReplyDelete
  2. Inawezekana kuna kitu unamkera bila ya wewe kujijua,jaribu kujichunguza wewe mwenyewe kwanza

    ReplyDelete
  3. jamani huyu dada yupo fresh inaelekea.. sijui yupo kampuni gani
    Michuzi naomba email yake tafadhali!!!! Mimi nipo dar na nimetulia.
    siendi bar wala nini. sina kitambi na nipo fresh.
    Michuzi mimi nataka mke kama huyu. Sasa nimemaliza chuo na nina kazi poa hapa mjini.
    Naomba sana michuzi uweke email yake.
    Inaelekea bonge la toto..wa kishua haswa.. na wazazi matajiri??
    Mimi nipo tayari.. tuwe pamoja na sita kwenda bar wala wapi..

    Huyu jamaa ni mjinga.. Ajui mke kama wake ni vigumu sana kupata dar..

    Dada wewe mwache huyo jamaa. Weka email yako mimi nitakutafuta.
    Naomba ujibu Miss KV

    Mimi Costa Mushi
    Mungu Akubariki

    ReplyDelete
  4. huyu naona ana nyege njingi

    ReplyDelete
  5. Kwanza dada yangu naomba utulize boli... hapa umemwaga mtama kwenye kuku wengi.

    Angalia usije ukavuka mkojo ukaangukia kwenye kinyesi. Mwanzo kabisa ningependa kukusihi uzungumze na mumeo muweke mambo sawa.

    Wewe kumfananisha mume wako na wanaume wengine (Wabebaboksi) inakupa nafasi ya kukuza tamaa yako na kukupunguzia uwezo wa kumudu mahusiano yako. Punde utakapoanza kumfananisha mpezi wako na watu wengine utakosa kufurahia upekee wake ambao huwezi kufananisha na mtu yeyote yule.

    Wengi hapa unaozungumza nao pengine wanamatatizo kama yako au hata zaidi. Hivyo ni bora kuwa makini.

    Usiri na uaminifu katika ndoa ni kinga ambayo hupotea punde unapoanika mambo yako hadharani kwa watu... Kila mtu ana shida na hata pengine wengi huweza kuficha mambo yao japo kwa ndani wanajua kinachowaumiza mioyoni.

    Ukimshirikisha mume wako na kumueleza kwa uwazi unavyojisikia bila kumlinganisha na mtu mwingine naamini mtaweza kupata suluhu. Ukiruhusu ndoa yenu iweze kutumika kama mfano wa shida katika ndoa pasipo wahusika wenyewe kuwepo kumbuka kwamba umetoa idhini watu kuingilia mahusiano yenu.

    Wahusika wakuu ni nyie wawili - WEWE na mume wako.

    MAMBO YA KUJIULIZA:

    Jiulize alianza lini tabia hiyo? Je, alikuwa hivyo zamani? Je, kuna uwezekano kwamba unasababisha yeye kuchelewa kuja nyumbani? Je, anaelewa kwamba haupendi tabia yake ya kuja nyumbani amechelewa au akija amechelewa wewe haumuelezi au unanuna?

    Ukiweza kutambua hayo unaweza kushangaa mabadiliko yatakayotokea...

    Jaribu akija nyumbani kumkaribisha kwa furaha hata kama atakuwa amechelewa... kisha kwa siku nyingine panga muda maalum wa kuzungumza kwa upendo na kujali... kumueleza wasiwasi wako na kutathimini ndoa yenu... naamini mtapata muelekeo mzuri na anaweza kugundua makosa yake ukimuelewesha kwa upendo na kujali.

    Kama unampenda basi hauna sababu ya kumuacha. Pia usisahau kwamba "MBEBA BOKSI" anaweza akawa anavutia kwa mbali lakini pindi ukishakua naye yawezekana naye pia anamapungufu japo siyo kama ya mume wako. Watu hawafanani hivyo kumlinganisha mume wako na mwanamme mwingine haisaidii... mkubali kama alivyo na utaweza kuridhika naye na kukubali mapungufu yake na mazuri yake pia.

    Suleiman

    ReplyDelete
  6. Pumba za mbeba boxi, kakosa kazi anachangamsha mada yake. Anaandika na kujijibu mwenyewe...!!Demu gani mwenye hicho kisomo na anaelipwa huo mshahara anaandika pumba kama hizi. Hela hizo men wapo kibao bongo kuna haja gani kusubiri kwenda huko Marekani! Na kitambi kinahusika vipi? Pumba tupu!

    ReplyDelete
  7. Wewe uliyeandika mada hii ni YULE YULE anayejiita mkurugenzi wa wabeba box. Kinachofanyika ni kubadili email address yako. Kwa wenye akili zetu za haraka za kung’amua watu washamba kama wewe tumekustukia. Ni kwamba mtiririko wa ulichoandika hapa na ule ulioandika pale mwanzo katika mada yako ya kwanza ni sawa kabisa.
    Kikubwa zaidi ulichojichanganya ni kuwa hapo umeandika UNATAMANI SANA ucheat lakini wewe unajiita ni MKE MWEMA. Hapo chini umesema mumeo ana kitambi dakika mbili yuko hoi uwanjani. MBEBA BOX WAKO YEYE NI GYM KILA SIKU NA YUKO FIT. Tushike lipi? Umesha cheat tayari au bado? Kibaya zaidi na maneno kama haya haya yametumika katika mada ya kwanza. Nadhan ujipange urudi kivingine na utumie muda wako vizuri kwa manufaa yako na ushamba wako.

    Mwanaume asiyependa mpira naye utamwita mwanaume? Kacheze mduara/tarabu/kombolela.
    Michuzi mada zingine uwe unazitupia kapuni maana hazina mshiko. Kuna mambo mengi sana ya kuifanyia Tanzania.

    Mdau Brussels- Belgium

    ReplyDelete
  8. Huyu Sulemani ana akili sana. Mimi nasema Miss KV achana na huyo mume wako. Ni mjinga sana.
    Duh, safari ndio hio ya marekani..another one bite to dust.
    MUME AMECHELEWA HAPA @SULEIMAN ADVICE REPLY.

    HUYU DADA ATAPATA SINDANO YA KUTOA MAUMIVU KUTOKA KWA HUYO MBEBA BOKSI WAKE WA NEW YORK. MABISHOO SANA WALE..

    Lakini mimi nasema jamaa mwache kwani tayari huwezi kufanya hawe mume mwema.


    MIMI NIKASIRIKA SANA WATU WANAPATA MKE MZURI HALAFU HAWAJUI KUMTUZA.

    Vijana au wanaume kama hawa hawasitahili kuwa na wewe kabisa. Tupo sisi wanaume wa shoka.. kina nanihii na tutaweza kukuheshimu na vilevile kama kutoka tutatoka wote.

    JAMANI MIMI NIPO DAR LAKINI SINA KITAMBI NA NAPIGA TIZI NA NAJIPENDA KIMAVAZI NA AKILI KAMA WABEBA BOKSI WA MAREKANI AU ULAYA.

    SASA UKIRUDI SAFARI NAOMBA NITUTAFUTATE

    MIMI NIPO SINGLE, NINA DEGREE NA PIA NA KAZI NZURI TUU..

    SIPATI HELA NYINGI KAMA WEWE LAKINI NIKO KWENYE 2 MILLION KWA MWENZI.

    Michuzi Naomba email ya huyu DADA!

    PLEASE WEKA EMAIL YAKE AU KAMA UNA NUMBER YAKE..

    MIMI MCHAGA HALISI RIWA

    ReplyDelete
  9. Wewe uliye kuja na mada hii ni hayawani na wala si mwanamke unataka kufanya watu wapumbavu,wadau wala mziumize kichwa najitolea kupoteza muda wangu kumjibu mpumbavu huyu ili nanyi msipoteze muda wenu kama mimi. Mimi ni mwanaume na ninaomba mwanaume mwenzangu kama kweli unatabia ya kupoteza muda mwingi kwenye bar ama bila ya kukaa na familia yako hiyo ni mbaya na inaweza hataridha ndoa yako, vilevile angalau tuwe na utaratibu wa kufanya mazoezi, na naamini sote tunafahamu kama hujitolei muda kwa mpenzi wako ama hauko fiti hiyo ni hatari sana kwa uhusiano wako. Mimi niko marekani kimasomo na kabla ya hapo nilikuwa na kazi yangu nzuri tu hapo bongo, na fara yoyote hawezi kunibadilisha eti nibaki hapa, kwa sababu ni kupoteza muda kama wajinga wengine wanavyopoteza muda hapa, so siku nikila gamba langu, napiga mwaka mmoja wa kukusanya vijisenti napanda pipa, narudi minazini kwetu. Mimi kabla sijaja hapa, mtazamo wangu juu ya hawa ndugu zangu wanaojiita wanaishi hapa, niliwaona ni watu wa maana sana kwa sababu sikujua hali halisi ya hapa, na sasa najua watu wengi hatusemi ukweli wa maisha ya hapa tunapopaongelea marekani, sijui kwingineko kwa sababu sijafika. Kwanza hilo jina wabeba maboksi inabidi liongezewe jina liwe "wabeba maboksi na wafuta kinyesi." Ngoja niwaambieni ukweli wa mambo kwa ambao hamjafika hapa. Ni watanzania wachache sana wanaofanya kazi za maana hapa, tuliowengi, tunafanya "nursing homes," ama kwa machizi ambapo kukutana na kinyesi ni kitu cha kawaida saaaana. Hata mimi mwenyewe hapa kwa sasa nafanya kazi hiyo, na kinyesi kwangu ni kama vile baa medi kumwagikiwa na bia, ni kitu ambacho bongo kwa kweli nisingefanya but utafanyaje na upo nchi ya watu na sisi tunaonekana ni manyani tu, hata usome vipi jamaa kukuamini lazima uwe "extraordinary" kwa wamarekani period, hata ndugu zetu Africa-American wanalia nacho ni kwa sababu tu ni minority, and that is the fact. Msibabaike na mpumbavu yoyote anayekuja kutoka huku, unaweza wewe ukawa wa maana mara elfu kumi miatano na mbili nukta tisa tisa.... Kuna jamaa wapo more than 10 years hapa wakiongea kiingereza ni kama cha kwangu nilicho jifunzia kwenye shule za halmashauri kuanzia msingi, sekondari, a-level na mpaka udsm, tena kuna wakati nashindwa elewa inawezekana vipi ikawa hivyo. Sasa wewe fara najua ni mtu uliye nje na unataka kulazimisha watu wa nje waonekane ni wajanja saaana ama wa maana sana. Nashukuru sana Mh January Makamba aliweka wazi alikuwa anafanya kwa machizi wakati yupo hapa and I am very sure ameshika sana mavi ya machizi ama vizee na kubadilisha diapers, na nani wewe fara ka-kwambia kuna mtu anaweza poteza pesa kulipia gym hapa, kwa mshahara gani wa $ 9,10,11, 15...au kwa muda upi atakaokwenda gym. Kwa taarifa yako vitambi vipo kibao hapa, nyani wewe Ukifika tu hapa wanakwambia eti soma CNA kwa sababu kazi ni rahisi. Asikwambie mtu, tembea uyaone na always "home sweet home" na nikila tu nondo yangu nakwea pipa narudi zangu bongo nikale maisha yasiyo na stress. Eti niki-chat nae anaongea vizuri malaya mkubwa wewe, nyoooooooooo! njoo uone anavyo pelekeshwa na Wanugu (African-Americans), ama mibonge yanya yenye minyama-minyama ya kizungu kisa makaratasi. Vijana wenzangu wabongo (mliokwenda na msiokwenda shule) mwenzenu narudi tuendeleze uchapa kazi na maendeleo yetu binafsi maana ya nchi nayo kuyafikiria ni kuumiza kichwa. Wakija bongo tuwe tunawapeleka kwenye vibanda vyetu tunavyo miliki sisi wenyewe vya vigae, kuwaonesha mashamba yetu, mifugo yetu na ma-investment yetu huku maisha yanakwenda taratibu. Msibabike na picha zetu za bloguni tunapiga baada ya kutaabika sana na kushika mavi.
    Msema Ukweli!

    ReplyDelete
  10. Mimi ni mume wako, nimesoma hayo yote uliyoandika na nimejua ni mimi kabisa. Maana ni kweli tumefunga ndoa january, ni kweli una masters, mshahara wako kweli naufahamu ni milioni 5, na wazazi wako wanauwezo. Na ni kweli huwa naenda kutazama mpira kwenye mabar ingawaje kweli nyumbani kuna dstv na bia zipo.Umekuja kuyaongelea hapa kwenye blog umesahau ule wosia ulipewa ukiwa ukumbini siku ya sherehe ya ndoa yetu?Unakumbuka uliambiwa ukiwa na tatizo unatakiwa umwambie nani?Sasa utanikoma nikurudi nyumbani.

    Mumeo

    ReplyDelete
  11. JAMANI NI MIMI MISS KV
    Nasoma majibu lakini mbona mnataka email yangu?

    Mhmm naona kuna wanaume wenye akili hapa Bongo.. asante suleiman..

    Lakini naona amechelewa..sasa navyoandika saa nane ndio amekuja.

    Kaenda chumbani kulala mimi nipo living room. Anafikiri nafanya kazi kumbe basi tu.. niko bored kichizi

    Sio napenda wabeba boksi, mimi ni mwanamke ambaye nimejaliwa baraka na Mungu. Kazi ninayo, hela ninazo na wazazi hawahitaji hela zangu.

    Muda kidogo uloyopita Baba yangu ameninunulia gari safi sana. (Zaidi ya milion 40) .. siwezi kukwambia gari gani sasa

    LAKINI MIMI NATAFUTA MWANAUME ANAYENIPENDA.. SITAKI PESA BALI MUDA WAKE..

    NDIO NAONA MBEBA MABOKSI YUPO FRESH NA ANAVUTIA

    Miss KV

    ReplyDelete
  12. Mambo ya mapenzi ni magumu kuyafahamu. Lazima kuwepo na sababu ya mapenzi ndio watu wanapendane. Wengine wanapenda warembo kwa sura, wengine wanapenda warembo kwa elimu au mali, wengine ucheshi, wengine afya ya mtu yaani watu wa gym, umaridadi, urefu au ufupi wa mtu, rangi n.k. Nakumbuka wakati ninasoma kuna wasichana walikuwa wanawapenda wavulana wanaofanya vizuri darasani katika masomo yao. Kila mtu anakigezo chake cha mpenzi anayemtaka. Lakini mbali ya hayo kuna vigezo vinavyowekwa na vyombo vya habari. Hivi sasa bongo kuna vigezo vya mamiss au mamodel. Sasa watu wengi wanapokuwa wamechagua bila ya kutafakari vizuri au kulazimishwa na familia hapo ndio matatizo yanapoanza. Inaonyesha wewe huna tatizo la fedha, umeamua kumfata mbeba boksi kwa sababu ya vigezo vyako vipya, na mumeo nae ameamua kuwa na nyumba ndogo kwa vigezo vyake vipya. Kuna kesi imetokea hapa ninapoishi kuna mwanamke mrembo sana kwa sura na anaasili ya kiasia, mumewe naye ni muasia ambae ameweka nyumba ndogo na mwanamke wa kiafrika mweusi hata weusi wenyewe wanamuhisabu kuwa ana sura mbaya. Nafikiri watu wazingatie mapema nini wanachokitaka kabla ya kufanya ndoa. Hivyo basi nakubaliana na mdau ayeuliza je nyinyi wenyewe wawili mmeshazungumza nini mkitakacho kwenye mapenzi yenu?

    ReplyDelete
  13. Anko hii mada inatugusa wengi sana ,ndio maana ina wachangiaaji wengi.
    Nipo ndani ya ndoa miaka 6 sasa,hudumu kamili nahisikia kwenye bomba tu, mume wangu dakika 2 amejitahiidi sana,kisingizio amechoka , kila siku anashind Bar,sasa si kuuwana huku,

    ReplyDelete
  14. dada kwanza kabisa pole sana ila inanisikitisha sana kwa kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri kiasi hiki ,, kwa msomi wa masters hukutakiwa kuweka jambo hili katika mtazamo ulioweka hapo juu kwenye mada yako, nina uhakika asilimia 70% mumeo kama ni mpenzi wa blog hii atagundua ni yeye anaongelewa(kwa sababu ya dondoo ulizoweka wazi) na unaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye ndoa yenu,tafadhali siku nyingine tumia utaratibu wa tofauti.

    USHAURI;
    kama unaipenda ndoa yako kwanza fuatilia ushauri wa suleiman hapo juu...
    pili usiweke akili yako kwamba mbeba maboksi atakufurahisha kumbuka hizo ni tamaa za muda na hasira ndio zinakupelekea wewe kufikiri hivyo, kumbuka mtu ambaye umeamua kuolewa nae ni hatua kubwa hiyo umechukua, labda kama ulifanya makosa katika hili kwamba hukuwa tayari kuolewa nae na sasa ndio mambo hayo yanalipuka, ila cha muhimu zaidi kwa sasa ni kuongea na mumeo mwambie kinagaubaga aelewe nini kinakusumbua na yeye akwambie kwa nini anafanya hicho , i hope anafahamu kwamba anakosea hiyo si kama ni bahati mbaya he does that on purpose, kuwa makini sana na marafiki wanakushauri kucheat kwani hiyo sio solution ya kudumu na unazidisha mzigo ktk mahusiano yako, kwani ni ngumu sana kuhudumia mabwana wawili hata biblia imeandika hili. kuwa makini unapofanya mapenzi na mume wako ni kweli anaweza kukuletea magonjwa so liangalieni hilo pia. Tatu, jichunguze wewe mwenyewe jaribu kukumbuka nini ulikuwa unamfanyia kipindi hicho he was high on mountain in love with you, jaribu kurudisha hizo ladha na angalia ni tabia gani unazo mwenzako hazipendi kutambua hili jaribu kukumbuka mmegombana kwa sababu zipi mara nyingi? au amekukataza tabia fulani fulani mara ngapi? nne, usiongee kwa ukali ukiwa unataka kuongea nae kuwa umerelax, na mtegee kipindi ana furaha. try this i hope it will work out,,,all the best mungu akututie nguvu sana.

    malichiki (ukrn)

    ReplyDelete
  15. Nahisi na wewe pia unamapungufu ila cha kufanya ni kukaa na kuzungumza na MUMEO na kutafuta njia ya KUYATATUA MTATIZO yenu,MITIHANI ktk maisha ya NDOA ni kitu cha kawaida, uamuzi wa kwenda kufanya MACHAFU na MMBEBA box si UAMUZI wa busara.Kazi nzuri na kuwa na pesa ndio tatizo lenu kwani kuwa na FEDHA nyingi na kutokuwa na FEDHA vyote hivyo ni vyanzo vya kusambaratika kwa NDOA nyingi,DADA yangu tumia BUSARA utaiona raha ya NDOA.Kwanza hebu fikiria ulivyotaja una kazi nzuri na una elimu ya kutosha tayari watu wanakugombea kama mpira wa kona yote ni FEDHA,Shangaroro(USA.

    ReplyDelete
  16. Mwamini MUNGU aliyehai aliyeziumba Mbingu na Nchi na hayo yote utazidishiwa..

    ReplyDelete
  17. oyaa sista du nicheki kwenye mail viporoporo@gmail.com

    Mdau Shambani(Karachi)
    Pakistan.

    ReplyDelete
  18. Mimi natofautiana na wachangiaji mliotangilia. Sina hakika kama miss KV ana exist kweli,maana kwa maelezo na mipango yote hiyo hata yeye mwenyewe anajua kabisa mumewe atamgundua. Na katika akili za kawaida tu, kama kweli yupo asingethubutu kusema kwamba anaenda Marekani na atatoka kimapenzi na mtu fulani. Hiyo sio kweli, sio kweli hata kidogo

    Ninachokiona hapa ni kwamba, ni huyo huyo Mkurugenzi wa wabeba maboksi au kijana wake (mbeba maboksi) ndiye aliyeandika hii kitu ili ku-justify alichoandika mwanzo (au alichoandika bosi wake). Hakuna miss KV hapo.

    Kwa sisi tunaoendaga huko mara kwa mara, tunajua maisha ya wabeba maboksi na wasambaza gazeti bwana. Wanadhiki na ni matapeli wakubwa. Wanaotesa kidogo ni wanafunzi wenye scholarships na wale kazi za kueleweka (formal jobs sio kucheza na maboksi). Akina "miss KV" kama mpo msidanganyike mtaenda kubeba maboski na nyie

    La mwisho, mbeba boksi harudi nyumbani bwana, atafikia wapi?

    Naomba kuwasilisha Mh Ankal

    ReplyDelete
  19. Miss kv kama wewe ni mkristu basi pata ujumbe huu na msawali haya ukiweza kujibu utakuwa slama na mwenye furaha.
    Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

    1. Je, ninajenga nyumba yangu au naibomoa?
    2. Je, ninawekeza kwenye ndoa yangu? Natumia uwezo wangu kuiboresha?
    3. Je, naonyesha kumthamini na kumjali mume wangu?
    4. Je, natumia nguvu zangu na uwezo wangu kwa ajili ya familia yangu?
    5. Je, natengeneza mazingira kwa maneno na matendo yangu yakumfanya mume wangu afurahie na kupenda kuwa nyumbani?
    6. Je, naridhika na kuihudumia familia yangu?
    7. Je, hisia zangu na upendo wangu ni kwa ajili ya mume wangu au mtu mwingine? Je, muonekano wangu, maneno mazuri na ushawishi mwema ni kwa ajili ya mume wangu au watu wengine?
    8. Je, natimiza mahitaji ya mume wangu?
    9. Je, ni mwaminifu kwa mume wangu? Nina uhusiano wowote wa siri ambao sitaki mume wangu ajue?
    10. Je, mume wangu yupo huru kuwa muwazi kabisa kwangu hata kunikosoa?
    11. Je, ninaruhusu mawazo ambayo siyo safi kuwa ndani yangu kupitia redio, televisheni au vitabu?
    12. Je, nimekuwa kimbilio na faraja kwa mwanaume ambaye ndoa yake ina matatizo?
    13. Je, natafuta ushauri na faraja kutoka kwa mwanaume mwingine (mchungaji, kiongozi wa kanisa, mshauri, mfanyakazi mwenzangu) na sio mume wangu kwanza?
    14. Je, ninauhusiano wa karibu zaidi na mwanaume mwingine kuliko nilivyo na mume wangu?
    15. Je, nimekuwa mkali na mwenye maneno yasiyo ya upole au ni mwenye maneno mazuri na yenye upole na unyenyekevu?
    16. Je, naonekanaa rahisi rahisi kwa wanaume wengine au naonekana ni mtu mwenye msimamo? Je, naruhusu mizaha isiyofaa na watu wengine?
    17. Je, kuna kitu katika mavazi yangu, muonekano au maongezi ambacho kinaweza kuwa kichocheo kwa wanaume kuwa na tamaa?
    18. Je, ninavyoongea na wanaume kazini au popote naonyesha kuwa mimi ni mwanamke wa kristo au nakuwa nawaonyesha upendo na ukaribu wa kupitilizia ambao unapaswa uonyeshwe na wake zao?
    19. Je, nimeweka mipaka katika mahusiano yangu na watu wa jinsia ya kiume? Ni mipaka gani hiyo?
    20. Je, kuna mausiano niliyonayo ambayo yanaweza kuleta utata kwa watu?
    21. Je, mume wangu na watu wengine wanao nifahamu wanaweza kusema kuwa mimi ni mwanamke mwenye busara na anayejiheshimu?
    22. Je, nimeazimia moyoni mwangu kuwa safi mbele za Mungu? Je, ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine wanaoishi maisha ya kumfuata Mungu?

    Mithali 31:10 Mke mwema, ni nani awezaye kumuona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
    Nakutakieni kwaresma njema.

    ReplyDelete
  20. we umeolewa lakini bado haujakua hakuna such a thing like perfect ndoa kila ndoa inamapungufu yake its up to your na huyo husband wako kuweza kuyakpunguza means kujadiliana na pia kucomplomize sana katika ndoa na sio kuja kuanika mambo yako hapa huku ulaya huwa tunakua na maneno matamu kwa wanawake wa bongo kutoka na uhaba wa wanawake au mtu kutokuwa na mpenzi kwa muda mrefu au kutokufanya sex kwa muda mrefu thats why tunakua na maneno matamu lakini think in long tem utakuta huyo jamaa akaja kuwa ndio anamakubwa zaidi ambayo utakuja kutuletea tena huku kwenye blog ya michuzi cos hauna akili timamu na wewe unakazi ya ziada at least rekebisha upande wako as umesema na baba yako nae haeleweki mpango wake so wwe jaribu kuvunja hio tabia ambayo inaonekana ipo kwenye ukoo wenu cos sisi wenzio at least tunasehem ya kukop in case mambo yakienda vibaya wazazi wetu wako safi sasa ninacho kushauri anza kuitibu hio ndoa yako ili usirudie makosa ya baba yako ok na wewe michuzi hebu acha kutuchosha na topic ambazo hazikuhusu hizi zilitakiwa ziwe kwa akina dinahicious@blogspot na sio wewe michuzi we vipi bana

    ReplyDelete
  21. Dada umenena ila ningekuwa wewe nisingesema mambo yote sababu, atajua utakwenda nje karibuni na atajua una mshikaji huko.

    Swali langu ni kama pale juu, je mlipochumbiana alikuwaje? je imewachukua muda gani mpaka kuoana? Kumbuka pesa si kila kitu. Umeona mamilionea wanaooa na kuacha kila siku hii inaonyesha kuwa mapenzi hayana pesa. Ndo maana wanaume wanaawaacha wake zao na kutembea na wafanyakazi wa ndani.

    Je ukitoka kazini unakuwa mke au unakuwa mamsapu wa kutuma na kuita kama wahindi? je, huwa uanweka mbali mawazo ya kuwa una kazi nzuri na unatoka familia tajiri unapokuwa na mmeo na kujifanya wewe ni chini ya mme? Si kwa kila jambo uwe chini lakini kuna wakati inabidi tujiweke chini kidogo ili mme asikike.

    Achana na huyo mbeba maboksi halafu mpeleke mmeo ajiunge na gym na wewe uwe naye hii itampunguzia nguvu za kwenda bar.

    ReplyDelete
  22. Dada pole sana kwa hayo makubwa yanayokusibu, dah kweli sasa nimeamini kitambi si dili kwa kweli, mimi nlikuwa na kitambi hapo siku za nyuma na nlikuwa nadhani ni dili, nilipokuja ulaya na kuona watu hawafagilii kitambi na mimi nikaakiondoa haraka sana, wabongo mnaotaka kuja ulaya jamani kama mna vitambi mjue hapa patupu, hakuna msichana atakayekukubali na kitambi chako. Sasa sina kitambi na naona mambo fulani yamekuwa murua sana.

    Suala la msingi dada yangu ni kujiuliza kuwa mume wako alianza lini hiyo tabia? je mlishawahi kuzungumza na wewe ukamwambia kuwa hupendi hiyo tabia? unajua kucheat hakuna mwisho, usifikiri ukicheat US basi tabia itakoma pale airport ukiwa unarudi, hiyo ndo itakuwa mwanzo wa tabia mbaya ambayo pengine itakuwa vigumu sana kuiacha. Tafuta wasaa muafaka kaa china na zungumza na mwenzio lakini kamwe usijaribu kuonja issue ya nje hutoacha.

    Mungu atakusaidia kufanya jambo lenye busara, jaribu pia kupunguza mawasiliano na wanaume mana ujiulize kama huyo jamaa anakupenda, mbona hajakuoa???????

    ReplyDelete
  23. Nakwambia mwaka huu wanaume wengi wataachwa kwenye mataa wasipojirekebisha hizo tabia zao. Hebu angalia huyo mwali mdogo hata ndoa haijajibu kilichokufanya wewe kaka umuoe kisha umfunganye ndani ni kitu gani? Wivu au ukware? Maana tungesema mmekaa miaka 10, 15 mmeshachokana na nyumbani kuna makelele ya ndugu na watoto hapo sawa, lakini ndio kwanza ndoa hata miezi mitatu haijaisha, mwanaume badala ya kujenga mapenzi na kujenga nyumba yake kutwa vijiani kama kuku wa kienyeji au mbwa koko hivi hiyo ndoa kweli unaijua maana yake au unaisikia?

    Jamani eeh mimi niko tayari kuanzisha vitcheni party vya wanaume, maana inaonekana hapa kuna mapungufu yanayotokana na kukosekana kwa mafunzo ya jando na unyago. Zamani jandoni vijana wa kiume walikuwa wanapewa kozi ya jinsi ya kuishi na mke, kwani wazee wetu walijua kuishi wawili ni kazi maana wote mmetoka kwenye malezi tofauti sasa kuna vitu vingi hapo. Na tena zamani kesi kama hii ikipelekwa kwa wazee wenu utachekwa kijiji/mtaa mzima na tena utaonekana labda jongoo lako halipandi mtungi kwani haiwezekani mwali mbichi umuache alale kitandani peke yake wewe ukanywe pombe au kuangalia mechi kama sio tatizo la jogoo kukosa kuwika.

    Sisemi bi dada uvunje ndoa yako lakini huyo bwana nenda kamshitaki kwa mshenga wako au kiongozi wako wa kiimani maana hayo mambo kadri unavyoyaachia mwisho wake sio mzuri. Sasa kama yeye tatizo lake ni jogoo hawiki mbona hilo ni tatizo dogo lakini kama ni kiburi tu cha udume wake (Wanaume wengi hawakubali makosa hata kama utamkuta hana nguo kitandani na mwanamke mwengine atakwambia sio mimi yule au nilibakwa) basi wazee au hao viongozi wa imani watakusaidia. Kwa sababu hicho kilichokupeleka kwa mume lazima utimiziwe na kama hawezi kutimiza akae pembeni waje wengine wakutimizie hukufuata ugali humo ndani maana hata kwenu ugali upo! Ebooh! Hii aibu gani sasa nyie wanaume mnaleta?

    ReplyDelete
  24. ha haaaaaaa jamani yaani kama watu humu wanaakili basi watagundua kwamba mtoa mada ni yule yule hapa kaja kivingine

    ReplyDelete
  25. Mungu wangu, mungu hakupi vyote!!!!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  26. Dada yangu mpendwa...Sisi wanaume wengi..au karibu wote tuna - mature at the age of 40..Jiulize kwanza huyo jamaa yangu ana umri gani? kama amefika 40 au anakaribia 40 na mambo yale yale..anza kuwa na plan B ya maisha.. lakini kama bado yuko chini ya 40..basi kuwa nae "baneti kwa baneti" kama afande wangu kule Makutupora alivyokuwa anasema...

    ReplyDelete
  27. Lugha iliyotumika huyu anajidai ni mke wa mtu ni Muongo! Anaonekana ni Gay huyu! Anachachafya blog ya Michuzi!

    ReplyDelete
  28. this is the same guy who posted the otherone, hapa anajifanya dem.

    ReplyDelete
  29. MRS KIOKOTEMarch 24, 2011

    WEWE NI MALAYA HUNA LOLOTE UMEOLEWA JANUARY HII NI MARCH HATA MIEZI MITATU HAIJAISHA UNASEMA ETI MBEBA BOX WANGU NEW YORK , USHACHEAT DADA NA MUNGU ANAKUONA, MNAWASIFIA WAMAREKANI SABABU HUKU WATU WAKO BUSY MNO, NA PARTY NI ZA KUOKOTEZA, NDIO MAANA HAWATOKI SANA ,LAKINI BNONGO KUNA VIKAO VYA HARUSI, MARA BAR KUNYWA NA WASHIKAJI , LAKINI CHA MUHIMU NI KUWAKUMBUSHA TUU KAA NAE KIKAO MWAMBIE EEH BWANA KUMBUKA UMEOA INABIDI UBADILIKE PUNGUZA OUTINGS ZISIZO NA MAANA, HATA WANAWAKE PIA , KWA SISI TULIOKO AMERICA TUNATOKA SANA WAKATI WA SUMMER LAKINI BONGO KUNA PARTY KILA WEEK , NATENA UKITAKA MONDAY TO SUNDAY KUJIRUSHA, NA BADO MAKITCHEN PARTY, HARUSI, KIPAIMARA , BIRTHDAY , BASI ILIMRADI WAMEKULA MIGUU YA KUKU, HAHAHA. JAMANI WE DADA KUMBUKA NDOA NI MAWASILIANO(COMMUNICATION)AT LEAST UNGETUAMBIA KUWA ULIKAA NAYE MKAONGEA HAKUBADILIKA , NDO UKAANZA KUSKYPE NA HUYO MNUGU,,,, WATCH OUT UTAKOSA VYOTE HUYO WA NEW YORK UKIKAA NAYE KWA MUDA UTAONA UDHAIFU WAKE PIA
    BARIKIWA, NI MIMIMSHAURI MRS KIOKOTE

    ReplyDelete
  30. Wanaume wa kitanzania kama mapacha. nasoma hii habari nafikiria kuwa najisoma mimi. Sio huko Tanzania tu mimi hapa niliko ughaibuni ni hivyo hivyo. hakai nyumbani na ukipiga simu yake hapokei. Kitambi hana wala nini ila ni tabia tu ya kupenda sijui kuangalia huko nje vichupi. Mimi nimesoma na ninachong'ang'ania kukaa naye sijui ni nini. Kwa vile sasa hivi ni kama roomate vile tunalipa tu mortgage pamoja na kutunza mtoto.

    Sijawaza kucheat kwa vile mimi nimesema nikiona imetosha basi nitafunga virago nibebe mwanangu nikiondoka ndio nitaanza kujua lipi la kufanya na wala sitajeuka nyuma kutanzama.

    Alikua tofauti sana kabla hatujaoana, tumeoana alikua the best husband nilivyopata mtoto tu basi ndio hivyo...na sio kuwa nimebadilia ..Mimi nina gym nyumbani na nina gym membership hivyo hata weight yangu ni ndigo sasa hivi kuliko nilivyoolewa lakini ni basi tu. Nyumbani anaona kelele za mtoto basi muda wote ni kuenda kuangalia ngumi, mara sijui wana vijimikutano vya kitanzania, mara wanaanda soka ya summer kila siku sababu...

    To hell with them I can do much better by myself ni heshima tu ya watanzania naona tukiachana itakuaje lakini nafikiria maisha yangu yote hivi? Mbona itakua kazi sana kwa vile nafikiria yeye ni mdogo kuliko rafiki zake lakini yeye ndio aliyeanza kuoa. Ila kuna wengine wawili wameona pia ila bado wana hang around na wale singles pia na ukisema wanakuekea ile sauti ya yule mwanamke anayeongea kama mkenya anayetaka mumewew amfukuze kazi secretary wake...Wanasema wanawake tumezidi.. Sometimes I wanna be a lesbian labda mwanamke mwenzangu ataelewa wha I want...

    ReplyDelete
  31. duh suleiman nimekukubali..umeandika all sense!!

    ReplyDelete
  32. "Mnywaji", hajui nyumbani akitoka kazini, hapokei simu. Sidhani kama wewe dada umesoma kweli, kwa sababu ungekuwa umeshafunga virago siku nyingi, wakina dada usipoteze muda wako, kuolewa siyo kudhalilishwa, na siyo kuvumilia ujinga. Wewe upo sawa na mwanmume kama hakujali na wewe usimjali, hata kama huna pesa isiwe kigezo cha kuishi na wajinga. Life is good. Good luck. Michuzi usibanie hii.

    ReplyDelete
  33. We suleiman nimekupenda sanaaaaaa! Una mawazi mazuri...Lakini kuna wanaume wengine bwana hata kukaa nao muda mfupi huwa ni kero...huwa wana vitabia fulani hivi..hasa ukiolewa na mwanaume ambaye hataki maendeleo yako.kwa vile yeye anaona hawezi basi anataka na wewe mfanane.
    Lakini pia na huyu mwana mama namuonea huruma . kuna wanaume wa namna hiyo na hawezi kubadirika hata mkikaa chini. Sana sana wanaume wa namna hii huwa wana dharau sana wake zao. Na kama anaona mkewe ana pesa ndo kabisa anataka kumuonyesha kuwa pamoja na pesa zake hababaiki.

    Huyo mme hana lolote .wala wewe mama usifikiri anaenda kwa machangu. Ni basi tuu kwa kuwa amekuona una pesa anataka akunyanyase na pesa zako. Huyo ana inferiority complex. wala usijali. Mpe vitu tu uzae watoto wako basi . Wala asikutie presha. Mie nina mme wangu yuko hivyo hivyo. Nami nilichukua muda mrefu kumsoma.Mke ukiwa na pesa, na mme akahisi kuwa huitaji pesa zake , hapo shida za namna hiyo huanza.

    TUKO WENGI USIJALI, MWAGA VITU...rosalinda@yahoo.com

    ReplyDelete
  34. Mi hata sikupi pole wala hongera, maana ndoa ni wewe na mumeo na sio wadau au hukufundwa nini? Uzuri, hela, elimu zote zipotelee mbali kwani havihusiani na mapenzi na mwanamke wa kweli wa kitanzania mwenye miezi 2 katika ndoa hawezi akamuanika mwili/ubavu wake namna hii.Wapiga box wa ughaibuni wako busy na mabox yao ila wana ile lugha na sauti ya kienglish oh sorry love, ooh love ya much,excuse me and so on ila ndo hao hao wabongo au nawe ukikukuruka unakumbuka Marekani unashidwa? Tumia nyama ya ulimi kumvuta mpenzi wako kwani mapenzi ni hapa hapa duniani ukiwa naye furahi even kwa that moment. Usione wanawake wenzako wakijengewa kaghorofa ukadhani kamzizi no nyama ya ulimi na hata ukienda kwa marekani ukatoka nje ya ndoa twajua uliplan kufanya hivyo vile uliweka kwa hadhari. Punguza mapepe

    ReplyDelete
  35. Yaani Miss KV- pole sana .

    Nimeshangaa matatizo uliyo nayo kwenye ndoa yako-Ndiyo niliyokuwa nayo mimi katika ndoa yangu yenye miaka 5 na nusu sasa!Nami sijabarikiwa mtoto bado

    Mume wangu naye alianza hivyo hivyo mara anasema eti bia za nyumbani sio taamu, au tukiwa pamoja may be mtoko simu ikiita ananyanyuka kwenda kupokelea mbali,na akirudi home ni kushikana shikana tu na mabusu then tuishia kulala kavu eti hajisikii kufanya mapenzi.......nikaanza kujiuliza kulikoni au mwenzangu 'ameshashiba nje'-ni mengi kwa kweli ya kueleza......!!

    Huwezi amini kuna mambo nilikaa na kuyarekebisha katika ndoa yangu,ikiwa ni pamoja na mwenendo, tabia na mmmm.......(sipendi kuyaweka hadharani maana Mume wangu pia ni mdau mkubwa wa blog hii ya Michuzi),,Ila ninachoweza kukudhibitishia ni kuwa Mungu ni mwema sana-juzi kati kama wiki 2 zilizopita nikashangaa mume wangu anakuja kwangu analia na kuniomba msamaha kwa mabaya yote aliyonitendea na zaidi kutoithamini ndoa yake na kuwa hataki tena kusikia makahaba kwa kile walichomtenda.

    Ni story ndefu,maana toka siku ile mume wangu amebadilika sana-leo ndo nagundua kumbe anaweza kurudi nyumbani mapema,maana saa 12 jioni yuko nyumbani amechelewa sana saa 1 usiku ambayo najua ni sababu ya foleni njiani.

    angalau sasa nayafurahia mapenzi,kama yale tuliyoanzana wakati uboy na girl friend.Ikiwezekana nitafute kwa Email hii ( blessingyako@yahoo.com ) tuongee zaidi- hapa noma......!! ........"kama namuona mume wangu anasoma comment hii niliyoandika hapa..ha ha..!)

    Naitwa Miss SM

    "Ur a SURVIVAL" Miss KV

    Thu Mar 24, 07:48:16 AM 2011

    ReplyDelete
  36. Wewe miss KV? Anyway sijui mrs KV!! Au yuleyule mtoa mada wa wabongo na kutazama mpira...potelea mbali!!!..Muhimu mada. Mawazo yako ni mgando. Wanawake wengi hawajitambui na hivyo hawawatambui wenza wao. Wanawake wengi wapenda mapenzi ya love you baby, miss you baby, I cant eat if you are not around baby, my sweet delicious chocolate baby, na uongo mwingi wa hivyo...hujitambui dada. Hebu tuaheni utamadunu ambao si wa kwetu...tunalazimisha utamaduni ndio hapo tunaona ooh mwanaume huyu hanipendi...ooh mwanaume huyu hapigi gym...ooh mwanaume huyu tukitoka hanishiki mkono au kiuna barabarani...ooh mwanaume akinitoa Coco Beach hanikimbizikimbizi hanibebi mchangani...mara hanisukumi nidondokee kwenye maji ya bahari .. na vitu vingi vya hivyo ambavyo si utamaduni wetu.
    Kwahiyo akina dada hasa wa kileo ambao mna hela zenu, ambao baba zenu ni matajiri, ambao nyumbani kwenu kabla hujaolewa muda wote ulikuwa unashinda ktk mi-plasma sijui mnacheki tu ma- soap opera ya sijui Egoli, sijui My angel kitu gani n.k msitake kufananinsha utamaduni mnaouona humo ktk mimuvi na utamaduni wa kitanzania.
    La muhimu kaa na mtu wako muongee mstakabari wa mahusiano yenu na utaona once mkimueleza tu kuwa unaona mapungufu haya na haya kwake usije ukastaajabu kukuta akakuambia mapungufu yako yenye urefu wa foleni ya kwa babu Loliondo...na atakuambia kuwa hayo ndio yanamkera kuhusu wewe.
    Nikupe kisa kidogo cha rafiki yangu:
    Ameowa dada mmoja ana hela ok wote wana hela sababu wamesoma na wanafanyakazi taasisi mbili zenye kulipa vizuri hapa Tz. Dada kabla alikuwa poa tu lakini baada ya ndoa kabadilika hataki tena mshikaji awe kampani na sisi rafiki zake hata naye akiambiwa awepo...anataka wakae na mme wake tu nyumbani waangalie televisheni. Kisa ni hichohicho huyu naye akafanya kila njia mpaka akahakikisha anafunga DSTV nyumbani eti ili bwana asitoke wawe pamoja. Sisi friends wote Mungu katujalia tunamshukuru tuna vipato vinavyokaribia kama vya kwao hivyo hakuna mtu anayetaka kampani na mmewe labda kupiga mizinga ya pesa etc.

    Daah ni nina story nyingi saana tatizo muda...Hivyo jamani tujitambue kabla ya kuanza kutoa lawama na akina dada msifikiri kuwa na mwanaume anayeenda GYM ndio umepata mpenzi wa dhati ujue na utambue mapenzi ni sanaa ambayo hayahitaji gym zaidi ni kutambuana na kuwasiliana tu.
    Nikipata muda nitatoa kisa changu mwenyewe ambacho kitaelezea kujitambua na mawasiliano na kujua sanaa ya mapenzi vilivyo muhimu katika mapenzi....

    Wenu Mchanalaivu

    ReplyDelete
  37. Kwanza ujiulize wewe ni mtamu?
    Wasomi wengi sio watamu na hawajui mchezo ndo maana watu wanatafuta pa kulidhishwa.
    Hujishughulishi kwenye mchezo eti kwa sababu una mshahara milioni 5.
    Mwache mwenzio wakamfanyie masage na watu watee mbee na mbuzi kagoma

    ReplyDelete
  38. Kwa wote.. MIMI NDIE NIMEANDIKA HII.. KWANZA NAENDA NJE LAKINI HUWEZI KUJUA WAPI.. NIMEANDIKA NEW YORK KAMA CODE.. NA NIMETUMIA JINA MISS KV KAMA CODE. HATAWEZA KUJUA.. KABISA..
    TAREHE AU MUDA NAKWENDA HATAJUA..

    MUME WANGU HAJUI WALA HAJALI NAPATA MSHAHARA GANI.. WALA HATAKI KUSIKIA.. ANA HELA ZAKE. SISI HATUNA WATOTO KWA SASA KWAHIYO NDIO MAANA NINA MAWAZO HAYA..

    KINGINE SIKUSEMA.. NIMEGUNDUA ANA CHEAT.. KUNA MARA MBILI NIMEONA CHAIN AMBAYO HAKUNIPA MIMI.. ETI NI ZAWADI YA DADA YAKE..

    SABABU NYINGINE KUBWA SANA SANA SANA YA MIMI KUTAMANI KUCHEAT NIMEAMBIWA NA WATU WATATU WHICH DON'T KNOW EACH OTHER.. THAT HE IS CHEATING.. ONE OF THEM DIDN'T EVEN KNOW I WAS THE WIFE..

    ASANTENI SANA , THANKS FOR THE ADVICE.

    NDIO WANAUME WENGI BONGO LAKINI MUME WANGU ANAJULIKANA SANA.. SIWEZI KUTOKA BILA MIMI KUGUNDULIKA..

    KUMBUKA DAR NDOGO..

    ReplyDelete
  39. nimesoma hii mada nikacheka kwanza halafu nikawaza kweli una masters na unahangaika kuomba ushauri humu?? Sit and talk to your husband mkishidwana ni nyie wenyewe the society issingilie afterall wanaoishi humo ndani ni wewe na mumeo. Kitambi has nothing to do with shuguli mie mume wangu ana kitambi kikubwa na ananiridhisha sawia hahah

    ReplyDelete
  40. Dada yangu pole sana, kwanza napendakukushauri kwamba kila mtu anamatatizo yake, na kila mtu akisema ayaweke hadharani yako yananafuu kuliko, kwani ww Mungu ameshakujalia hata unauwezo wa kumwekea mumeo bia kwenye friji????? Wapo wengine waume zao wanakipato kizuri lakini kutwa kiguu na njia baa au machangudoa, ninachokuomba mwombe Mungu awezekumbadilisha mumeo kwani huyo ndiye wakwako, nitafute zaidi tuwezekushirikiana katika maombi.
    Dd

    ReplyDelete
  41. YAANI HII MADA MASAA MATATU COMMENT 39??? KWA KWELI MICHUZI INAKUWAJE?

    NAONA KUNA HABARI NYINGI ZA MAENDELEO YA UCHUMI, MISIBA NA RAISI AKITEMBELEA WAZIRA MBALI MBALI.. LAKINI COMMENT ZOTE ZIPO KWA HII MADA.

    DUH.. NAFIKIRI MICHUZI UMEGUSA JAMII.. YAANI UKIWA NA MADA KAMA HIZI MBONA JAMII ITAELIMIKA NA VILEVILE KUTOA STRESS..

    HUYU DADA NI MOJA YA WADADA WENGI WALIOSOMA HAPA TANZANIA

    WANAKUJA HAPA JA DEGREE ZAO, AU BABA ZAO MATAJIRI BASI WANATAKA KUAMRISHA WATU

    SAFI SANA JAMAA ANATOKA OUT.. TENA ATOKE SANA..

    WEWE UNAJIONA SANA ..

    MIMI NINA MKE WANGU MAMBO YAKE KAMA YAKO..

    NIMEMTANDIKA WATOTO WATATU BACK TO BACK.. SASA YUPO HOME KAMA KAWA..

    NA MIMI NATOKA OUT KAMA KAWA..

    LEO KUNA MECHI NA SIRUDI NYUMBANI MPAKA SAA SITA..

    KESHO NDIO MARAHA MPAKA BASI..

    VIMADA VIPO VINGI NA HASA FORM 4, 6 NA VIPO VYA CHUO..

    TOTOZI ZINATUKEEP BUSY

    MIMI NASEMA BWANA WAKO ANATAKIWA AKUPE WATOTO THEN ATAWEZA KUZURURA..

    MDAU.. MIKOCHENI.. LEO NA KESHO MPAKA JUMAPILI FULL BATA

    ReplyDelete
  42. LISTEN GIRLFRIEND

    DO YOUR THING.. TANZANIANS WHO LIVE ABROAD ARE BETTER OFF AND THEY ARE MORE CIVILIZED.

    THE HABIT OF STAYING UP IN BARS WATCHING SOCCER IS BAAAD AND ITS IN TANZANIA.

    DUMP THE LOOSER AND GET WITH THE WINNER.

    MICHUZI.. WEKA HII MADA JUU.. MAANA INA UTAMU SANA.

    You have hit the target market and demanded topics.
    Achana na maposti ya siasi.. huko sisi hatuwezi.

    I AM A TANZANIAN WOMAN WHO IS EDUCATED IN UK AND NOW LIVING IN TANZANIA.

    I WAS MARRIED ONCE, I HAD TO DIVORCE THE POOR MLALAHOI. TOTAL LOSS.

    I GOT WITH MBEBA BOX, HE WAS FRESH FROM ONE OF THE STATES IN USA.. SORRY CANT SAY..

    HE IS NOW LIVING IN TANZANIA WITH ME.

    HE IS HOME BY 7 AND MOST 8PM

    WE HAVE DSTV, BBQ, POOL AND JACCUZI IN OUR HOUSE .. WE ALSO HAVE A GYM.. SOMETIMEZ I WONDER

    WHY TANZANIAN MEN LOCALLY RAISED DON'T KNOW HOW TO HAVE A GOOD TIME..

    DOES A GOOD TIME HAVE TO DO WITH DRINKING?? ALL THE TIMES??

    BADALA YA KUNUNUA PRADO YA PILI.. WEKA SWIMMING POOL, JACCUZI AU GAME ROOM HOME..

    TAKE A VACATION WITH YOUR WIFE.. WASHAMBA SANA HAWA.

    GOOD LUCK DEAR..
    IF YOU NEED MORE ADVICE LINK UP..

    HALAFU KAMA NAKUJUA WEWE.. ANYWAYS.. I DON'T EVEN WANNA GO THERE..

    MBEZI BEACH IN THE HOUSE!!!!!!

    ReplyDelete
  43. HUYU NI MUONGO TU HANA LOLOTE KAAMUA KUWAZINGUA WATU HAPA

    ReplyDelete
  44. DUH, hii topic tuu inatosha kwenye blog yako.

    Hatutaki kuona mambo ya dowans au wizara.. tumechoka nao

    Babu wa liondo na huyu dada made my day.

    Weka hii mada front page BANA..

    SITAKI KUSCROLL DOWN KUITAFUTA...

    LEO 3 TIMES NA CHECK COMMENTS..

    Kwi kwi kwi..

    Kweli dunia inakwisha.

    Dada, tulia na mume wako.
    Nenda marekani fanya mambo yako lakini ukirudi kaa kimya.

    Mbeba boksi akiwa vacation , toka nae.

    Kwanza hatakua clean , ikiwezekana mpe nauli ya kurudi..kila mara

    Mimi nina mbeba box wangu yupo London. Nakwambia nikijisikia weekend yupo Bongo.. tupo zanzibar au saaaadaaaniiii.

    Habari ndio hiyo..

    MIMI NIPO TRA.. PESA KIBAO

    ReplyDelete
  45. dah. Mie akili yangu imestack tu kwenye huo mshahara. Mie nina master, nna confidence nafanya interview sehem za maana sijapata bahati ya kazi nzuri that kiasi. Achilia mbali kutopata hata huyo mume anaezingua licha ya kuwa na sifa zote zinazostahili. Pole rafiki ila we tafuta mtoto kwanza na pia mweleze mmeo unahitaji vacation at least ya siku tatu muwe mbali na mazingira utakapoona siku za mtoto zinaruhusu. Mana kama ashaanza kupiga nje atakuletea mbegu nyepesiiiiii then naona kama mtoto atachelewa. Ukishakuwa na wanao wawili u ll be busy with them, stress zitapungua n someday kama vp utaona uwe na wanao tu hadi mmeo utoto utakapoisha.

    ReplyDelete
  46. wewe umeolewa,na mlipooana either msikitini/kanisani uliapa kwa mungu kuwa ndiye mume pekee chaguo pekee alilochagua utakuwa na mume wako katika shida raha na magonjwa. Iweje leo umsaliti na kumtamani mbeba boksi.Mpende mumeo mshawishi mwende kwenye jimu aondoe kitambi muendelee kama kawa labda kama kuna tatizo lingine kuwa wazi.

    ReplyDelete
  47. Wangu hana kitambi wala hanywi pombe wala havuti sigara ila hajui maana ya ndoa ni nini hajui maana ya mke ni nini hajui maana ya familia ni nini hajui maana ya mapenzi ni nini. Hajui mke ana shida gani na anahitaji kuhudumiwa nini na hata ukiumwa basi utajijua mwenyewe ila akiumwa yeye ndio utahangaika mpaka apone.

    Wangu haendi huko kwenye mechi za mpira nini lakini atakwambia yuko kazini kuanzia jumatatu mpaka jumatatu hana cha weekend wala likizo, na hakuna kutoka pamoja kwenda popote na ukijitahidi ndio useme mtoke wote kwenda dinner au lunch basi hata huko atakukimbia tu. Na pamoja kuwa ana gari ukitaka kwenda sokoni basi uhangaike na mizigo kichwani na kwenye madaladala. Yaani ilimradi yeye ni mwanaume mungu kampa mkia basi. Wengine mnaweza kusema labda wewe mwananmke ndio una tabia mbaya labda una gubu au tatizo, la mie ni mkimya sana na hii mambo ya kudanganyana wanawake eti vumilia wanaume wote wako hivyo hivyo ndio inatufanya wanawake wengi tunasema nikitoka hapa naweza kukutana na bomu kuliko hili. Nafikiri kinachochangia kama alivyosema mdau mmoja hapo juu ni inferiority complex kuwa pengine anaona kwa kuwa mie mke nimesoma na nina kipato basi ngoja anidhibiti kwa njia hiyo.

    Jamani mwanaume hasikii ushauri wowote kutoka kwangu, kila unalomshauri la kuleta maendeleo mpaka akawaulize marafiki zake au ndugu zake kwanza. Kwa elimu na ujuzi wangu nimewashauri watu wengi tu wengine wanakuja na wake zao na mpaka sasa hivi wananiona mimi kama ndugu yao kutokana na mafanikio waliyoyapata ama wanayoyapata. Wengine wananizidi umri lakini wananiheshimu na kunithamini lakini sio mume wangu kila umwambiacho anaona utumbo. Matokeo yake anakwenda kufuata ushauri wa ndugu na marafiki na huko keshapata hasara ya mamilioni ya pesa, I repeat mamilioni ya pesa kwenye miradi uchwara ambayo badala ya kuingiza pesa inamfilisi kinachomsaidia ni hiyo kazi yake lakini kama angekuwa ni mfanyabiashara basi angekuwa yu chopi saa hizi.

    Wengine mnamshauri huyo dada wakae chini wajadiliane, sasa wajadiliane nini? Wakati mmojawapo haoni hilo kama ni tatizo kuna mjadala hapo? Huyu wa kwangu tuna miaka kibao sasa yaani hata siku moja hataki mkae chini mjadiliane yeye always yuko right. Na hata ukisema upeleke kesi kwa wazee anawaambia tutayamaliza wenyewe, na badala mkae chini muongelee ishu atakukwepa wee mpaka siku zinapita lakini hakuna mabadiliko yoyote.

    Mwisho na mimi nimeamua kunyoa sasa na kinyozi ni mimi mwenyewe ntaanza kwa mkasi kisha mashine ya kunyolewa kutabaki upara bila ya unywele utosini. Na mwenyewe anajijua hata akiisoma hii atajijua kuwa ni yeye lakini ndio hivyo waswahili wana msemo LAKUVUNDA HALINA UBANI.

    Mama Manka
    Sombetini!

    ReplyDelete
  48. simple answer...

    acha nae... halafu jamaa yule unaempenda akuowe.. usi cheat...

    good luck

    ReplyDelete
  49. Huyo dada kasema ameolewa January ya mwaka gani? Kama ni mwaka huu kweli miezi mitatu mmeshachokana! au mlikuwa mnaishi sasa ndo mmeamua kufunga ndoa? Kama bado wapya basi umeumia, lakini kama mlianza kuishi bila shaka ulishaona mapungufu yake vumilia, but jaribu kumbadilisha kwani hiyo ndiyo kazi ya mwanammke, ukiona vipi basi toka nae japo wewe utakuwa upendi lakini fanya hivyo ili aweze kubadilika, mbinu ni nyingi dada watafute wataalam wa mambo (k.party) watakupa full mikakati.

    ReplyDelete
  50. Nimesoma mada hii hapo juu lakini naomba michuzi uweke mada yangu watu wanisaidie. Mimi nimeolewa huu mwaka wa 4 sasa mume wnagu anakiwanja lakini hana uwezo wa kujenga kwa sasa mimi angalau kidogo najikongoja. sasa naogopa kujenga nae pamoja kwenye kiwanja chake sababu pamoja na kwamba tunandoa ya kikristu lakini yeye ana mtoto wa nje . na akili yake yote ipo kwa huyo mtoto je wadau nifanyeje nisije dhulumiwa nikalia peke yangu.

    michuzi plz iweke mada hii nisaidiwe nipo kwenye wakati mgumu.

    ReplyDelete
  51. jamani wabeba maboksi si wanaume tu hata sie akina dada tupo tunaobeba boksi...sijui tukifika huko home inakuwaje maana nasi huwa hatutaki kukaa home tunakuwa tunashinda bar na hao wenye vitambi kwani hawa walitoka huku wanakuwa tayari wamepigwa baridi hivyo na boksi limewapindisha kisawasawa.

    ReplyDelete
  52. mmhh miss kv pole kwa yaliyokukuta,me ushauri wangu kama unahela yakutosha kwanini umize kichwa mlee mwanao ktk maisha mazuri mpe na elimu bora ili asije akapta shida maishani,nowdayz wanaume wengine wamezoea kulelewa na hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kufata hela na wewe umeshatangaza kuwa unahela kazia ipo watajitokeza kala mtu atataka kuwa na wewe kwa lengo la kukupa unachokitaka kumbe kaja na yake be careful my dear mjini hapa:,frdy_theobald@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  53. Shosti, mie jamaa yangu ana kitambi na anapenda sana kuangalia mpira na kinywaji, lakini hivyo vitu ni kama vinamchochea vile maana anaporudi nyumbani shughuli ni moja tu! anapokuwa uwanjani shughuli ni pevu, yaani rigwaride analijua hasa, kwa kweli ananifikisha kabisa ninapopataka! Sielewi uhusiano wa kitambe chake na madavidavi????? Ni Utundu na kujali tu????

    Hebu kaa chini ujue unachotaka hasa kwa mumeo ni nini? Kujivinjari uwanjani? Asiangalie mpira? Asiwe na Kitambi? Awe anaenda GYM? Au basi tu humpendi??

    ReplyDelete
  54. MISS KV NI FAKE, MSIPOTEZE MUDA WENU - HAKUNA MTU KAMA HUYO, NI MTU MWINGINE AMBAYE AMEKUJA TU KUWAJARIBU WATU NA WAO WAMEINGIA KATIKA MTEGO WAKE NA SASA ANAWACHEKA NA KUWACHORA JINSI MNAVYOJIKANYAGA

    ReplyDelete
  55. Duh WINNING!

    Always wabeba boxes...will be WINNING! DUh! sio science! teh teh teh teh!

    ReplyDelete
  56. Duh dakika mbili nyingi hizo. Ukipata dakika mbili usiku, mbili asubuhi na mbili mkirudi kazini 7 days a week. wow.

    ReplyDelete
  57. Unajua kunawanaume wengine siyo waongeaji,Unajua mwanaume yeyote yule duniani anaitaji vitu vitatu:
    1.Umtambue kama ni mume wako (heshima).
    2.Lugha Nzuri(Noise/Makelele)
    3.Care(delivering)

    Tafuta siku,mfanyie kitu kizuri ambacho anakipenda.kama ni msosi then after mwombe mume wangu naweza ongea na wewe,wakati huo umesha andaa karatasi na peni.
    Mgee then mwambie naomba u`list down Side A mambo yote mazuri Side B weekness zote.Badae compare mazuri na mabaya.Baada ya hapo utajua nini ufanye kujenga Ndoa yako.wewe pia kimpango wako list the same compare mazuri na mabaya.Itakuwezesha kujenga Ndoa yako.kukimbia matatizo siyo solution ya kusolve.Huyo Jamaa unae mwaza atakuwa namadem zaidi ya 15,watz hadi USA.


    Adviser wa Ukweli

    ReplyDelete
  58. Nina rafiki tulipanga kuoana, tumedumu kwa miaka kama 3 lakini naona tabia zake na zangu tofauti, zaidi huniridhishi kabisa kimapenzi. Nimejaribu kumwambia mimi sitaweza kuolewa na yeye lakini anangangania. Sasa sijui nimwambie nini ili anielewe. Naombeni ushauri wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...