Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Geofrey Meena (kushoto) akipokea moja ya Tuzo za Ubora walizoshinda TTB katika maonyesho ya kimataifa ya utalii yanayojulikana kama Outbound Travel Market (OTM) nchini India hivi karibuni kutoka kwa Ofisa Masoko wa bodi hiyo aliyewawakilisha katika maonyesho hayo Bi. Rose Mbwambo.

Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Rose Mbwambo akiwa na Tuzo za Ubora walizoshinda katika maonyesho ya utalii ya kimataifa ya Outbound Travel Market (OTM) yaliyofanyika nchini India hivi karibuni.Mbwambo aliiwakilisha TTB katika maonyesho hayo.

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeshinda Tuzo mbili za Ubora (Award of
Excellence) katika maonyesho ya kimataifa ya Utalii yaliyoshirikisha nchi zaidi ya 400 za mataifa tofauti duniani yanayojulikana kama Outbound Travel Market (OTM) yaliyofanyika nchini India mwezi uliopita.

TTB imeshinda tuzo ya awali katika maonyesho ya OTM yaliyofanyika mji wa Mumbai kati ya Februari 18 na 20 na ya pili wameshinda katika maonyesho kama hayo yaliyofanyika mji wa New Delhi kati ya Februari 24 na 26 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Geofrey Meena alisema tuzo hizo ni za kujivunia kwa bodi hiyo na Tanzania kwa ujumla.

Alisema tuzo hizo zinaonyesha mafanikio wanayopata TTB katika mikakati yao ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini katika nchi mbalimbali duniani ambapo banda la bodi hiyo limekuwa likiwavutiwa watu wengi katika maonyesho tofauti wanayoshiriki.

Alifafanua kuwa vivutio vya utalii vilivyotumika kupamba banda la bodi hiyo
pamoja na bidhaa za kitamaduni vilichangia kwa kiasi kikubwa kuipa ushindi
Tanzania ambapo vivutio vya wanyama pori na milima viliwavuta wengi.

“Tumepata tuzo mbili katika maonyesho ya kimataifa yaliyofanyika hivi karibuni ambapo kwetu ni jambo la kujivunia kama bodi lakini pia ni sifa kubwa kwa nchi ikizingatiwa kuwa tumekuwa na jitihada za makusudi kuutangaza utalii wetu duniani kote,” alisema Meena.

Wakati huo huo TTB itakuwa mwenyeji wa watalii 1000 kutoka nchini India
wanaotarajia kuwasili nchini Julai mwaka huu.

Meena alisema ujio wa watalii hao umechangiwa na mikakati endelevu ya bodi hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini katika nchi mbalimbali duniani.

Alisema watalii hao katika siku tano wakazokuwa nchini watatembelea visiwa vya Zanzibar, Mbuga za wanyama za Serengeti na Ngororo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Lo, naona mwandishi ameteleza kidogo, maana hakuna nchi 400 hapa duniani, achilia mbali "zaidi ya 400."

    ReplyDelete
  2. Dada Uaridi....Big-Up....you look mwaaa!

    ReplyDelete
  3. Bw. Mbele nashukuru sana kwa observation yako. Nadhani labda walitaka kusema 40.Lakini waandishi wetu tunawaomba msiwe na haraka mkaharibu ukweli wa mambo, kwani tunawategemea kuelimisha jamii. Umenifanya nitafute nikaona niweke na hii hapa anayetaka asomeWhile it would appear to be a rather simple matter to determine how many countries there are in the world, it is in fact quite complex. This is due not only to the ever-shifting political landscape, but also because the term ‘countries’ is somewhat fluid and open to interpretation.

    A narrow definition of what a country is might look at a well-established group – such as the United Nations – and take its list of recognized members. In the case of the United Nations, there are 193 recognized states, with 192 being members of the United Nations, and the Vatican City, which is a permanent observer with all rights of a member, save voting rights.

    One could also take an established definition for what a state is, and find all states which match those criteria. The most widely-accepted definition is given by the Montevideo Convention, from 1933. By these guidelines, a state must have a government, be in a position to interact with other states diplomatically, have a defined territory, and possess a permanent population. A rough count of these states would place the number of countries in the world at 201. That includes the 193 states recognized by the United Nations, as well as eight additional states. These are the Western Sahara, Taiwan, Northern Cyprus, Somaliland, South Ossetia, Transnistria, Abkhazia, and Nagorno-Karabakh. These states meet the criteria set out by the Montevideo Convention, but are all in a struggle with another, larger state, for independence, and so far have not been formally recognized by the United Nations.

    La pili hongera sana Aunt Rose for being a nice and dedicated officer despite what others think of you.Keep it up.
    Mariam.

    ReplyDelete
  4. How comes Shirika kubwa kama hilo lifanye maigizo? Eti afisa Masoko anamkabidhi Mkurugenzi wa masoko tuzo? Weee acheni uongo, weka picha ya waliokabidhi tuzo. Msije kuwa mlienda huko mkanunua matuzo yenu alafu mkakabdhiana tu kinyemela. ACHENI HIZOOOO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...