Huku wakiwa na vikombe mkononi, baadhi ya wakaazi wa jiji la mbeya na vitongoji vyake na kutoka mikoa ya jirani Sumbawanga Iringa Songea wakiandamana kuuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya kupinga kusitishwa kwa huduma ya matibabu ya magonjwa mbalimbali anayotoa kijana Jafari Willina leo
Wananchi wakiwa ofisi ya mkuu wa mkoa mbeya wakiwasubiri wawakilishi wao kuwapatia majibu toka kwa mkuu wa mkoa
Barua ya kusitisha huduma ya tiba ya asili kwa kijana Jafari Willina Iliyoandikwa na mganga mkuu wa halmashauri ya jiji la mbeya Dk Samweli Lazaro. Hadi tunaenda hewani jibu toka kwa mkuu wa mkoa lilikuwa bado hatujapata.
Picha zaidi na libeneke dada la Globu ya Jamii
BOFYA HAPA
Picha zaidi na libeneke dada la Globu ya Jamii
BOFYA HAPA
kwani nani alimpa Babu wa loliondo kibali cha kutoa tiba za asili?
ReplyDeleteTeh Teh!
ReplyDeleteUngesema imetoka kwa Mungu Dogo, wewe unasema imetoka kwa mama? Ona sasa, wakati wewe unaambiwa upeleke dawa yako Muhimbili, Serikali imepeleka wataalamu Loliondo 'kuomba' Dawa ili waipeleke Muhimbili.
Pole Dogo, ulaji huooo.. unayoyoma!
Mnamuonea mbona Loliondo yeye hapelekewi barua? Ni kiwango gani yeye alipasi na huyu nin nini alichofail?
ReplyDeletekama ni kusimamisha simamisheni wote hata waganga wa kienyeji sio huyu tu...
LOLIONDO-MBEYA stop!
ReplyDeleteWatanzania tumekuwa kama vivuli sasa tunafuata tuuuu. Serikali imeona ikomeshe maana ni muda mchache tu mngesikia maelfu ya watu wamepanga mstari mbeya kijijini huko aliko huyo dogo. Hivi hatuwezi ku reason out kwamba huu ni utapeli sisi wenyewe?
ReplyDeleteLoliondo tuliambiwa ni tiba ya kiimani, iweje hii ya Mbeya inakataliwa wakati ni ya kiimani?
ReplyDeleteAu serikali sasa inaingilia imani za watu?
Mnatonea sana sisi wananchi wa huku kusini kwa kuwapendelea wa kaskazini. Serikali onevu kabisa, sisi hatuna pesa za kutufikisha huko Loliondo za kukodi magari yenu ya watalii na kwenda kutalii kwa babu.
mmh wabongo bwana!Huyo dogo alikuwa wapi tangu zamani?Kwa hiyo anataka kutuambia mama yake alikuwa mganga wa kienyeji? au......tutanyweshwa mpaka sumu mwaka huu...mi nasema hivi walikuwa wapiii?
ReplyDeletemwaka huu kazi ipo. Tutakunywa hata mavi ya tembo? DOGO!
ReplyDeleteKwa kweli tuendako siko. Haya nami ngoja nibuni namna ya kuwavuna watu kwa staili ya dawa. Kumbe ni dili kubwa sana hilo!
ReplyDelete