Juu na chini ni baadhi ya wanamuziki
wa Five Stars Modern Taarab


Habari zimeingia sasa hivi kutoka mkoani Morogoro kuwa basi la abiria aina ya Coaster likiwa na wanamuziki wa taarabu wa kundi la Five Stars limepata ajali na watu zaidi ya watano wamefariki dunia papo hapo. Majina ya waliopoteza maisha na walionusurika bado kupatikana.

Habari zinasema kundi hilo lilikuwa likitokea Songea mkoani Ruvuma kwa shughuli ya muziki na kuwa baada ya kufika Mikumi takriban saa moja iliyopita basi lao hili liligonga lori bovu lililokuwa limeegeshwa barabarani.

Inasemekana kuwa watu zaidi ya 10 walipoteza maisha yao hapo hapo katika basi hilo linalosemekana lililkuwa na abiria 30 na watano wamekimbizwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro, kwa mujibu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo ambacho kimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Globu ya Jamii inatoa pole kwa Five Stars waliojipatia umaarufu mkubwa kwa wimbo wao wa "Mchumu mchumu.... mmwwaaaaaaaaaaaahhh..." na inaendelea kufuatilia habari hizi za kusikitisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. bwana ametoa na bwana ametwaa,,
    ila wameimba mchum mchum tena,mwaaaa na sio alambaaa,alaamba ya jahazi ankal!

    ReplyDelete
  2. Ankali majina tafadhali tunakutegemea sana.Allah awanusuru kwa hili na lingine tena...

    ReplyDelete
  3. Inna lillahi wa inailahi rajioon, M/mungu awalaze mahali pema peponi. Amin

    ReplyDelete
  4. Hii ni ajali ya kusikitisha sana. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amen. Mnzava- Dar es Salaam

    ReplyDelete
  5. inna lillahi wainna illahi rajiun..Majina ya marehemu hadi sasa ni

    Issa kijoti,( Nichum nichum tena ) Husna, sheba juma,na viongozi 3 na majina yanaelendelea kutolewa..hadi sasa wamefikia watu 12 walifariki..

    Mwenyezi mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi ( Amin )

    ReplyDelete
  6. tunaomba majina na picha za waliopoteza maisha tafadhali... RIP

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa wote wapenzi wa muziki wa taarabu mungu aziweke pema roho za marehemu mahala pema peponi........

    ReplyDelete
  8. nmesikitishwa sana na habari hizo jmani,wadau tuwewavumilivu katika kpnd hk cha majonz.hanifa wa chuchu fm znz

    ReplyDelete
  9. wadau tuwe na subira na tuzipe ushirikiano familia za marehemu. hanifa wa znz chuchu fm

    ReplyDelete
  10. SISI WOTE NI WA MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA, TUNAKUOMBA MWENYEEZI MUNGU UZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMIIN,BIG UP KWA TAARIFA ZA HARAKA TUNAOMBA TUPATIWE TAARIFA ZAIDI NA IKIWEZEKANA NA PICHA ZAO MAANA HII BREKING NYUUUZ TOKEA JANA MPK SASA HATUJAPATA HABARI MPYA KAMA MLIVYO AHIDI

    ReplyDelete
  11. Mimi mpenzi wa Taarab, nimesikitishwa sana na ajali hiyo pia misiba iliyowachukuwa wapendwa wetu, ndugu zetu na wananchi wenzetu wa Tanzania. Niliposoma breaking news hizi nilitetemeka nikasema EE Mungu nipe moyo wa kupokea hii taarifa mbaya. Kwa kweli nipo kazini lakini hata kazi nimeshindwa kuifanya kwa ajili ya taarifa hii nzito. Ankal asante kwa kutuhabarisha. Itakuwa vizuri baadaye ukituwekea picha na jina kwa kila aliyesafiri maana sasa hata majina yao wengine hatuwajui, twazifahamu sura zao. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwa. Poleni familia kwa misiba hii mikubwa na ya ghafla. Mungu atupe faraja na uvumilivu kwa wakati huu wa majonzi. Wote tutaenda njia ile ile na kwa wakati ambao Mungu anaupanga, poleni watanzania wote wapenda Muziki.

    ReplyDelete
  12. ankal 2nashukuru kwa taarifa japo imeniumiza nakunifanya nijiskie nisiye na aman siku nzima;ila nlikuwa naomba utuwekee picha zawote waliofarik ili 2watambue vizur kwa sura;kwan mim mbal nakumfaham issa kijoti hao wengine huwa nawachanganya kwa sura,.ntashukuru ukinisaidia kwa hilo;'2zid kuwaombea ili walazwe mahala pema;.pole kwa familia na wapenz wote wa taarabu kwa ujumla

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...