Ankal habari za leo?

Mimi ni mdau wa Tanzania issues,nimeguswa saana na vitu viwiwli tofauti.

20% KUCHUKUA TUZO 5 PAMOJA

Nimekua ikisikiliza nyimbo za msanii huyu toka anaanza mpaka leo amepata tuzo,imenifariji saana.Jamaa ni mmoja kati ya watu ambae anawakilisha maana halisi ya mtanzania kuanzia mashairi,midundo na hata videos zake its all about us.Juzi wakati tayari amepewa tuzo,nilikua club moja hapa Arusha wakaweka kwenye big screen kwamba amechukua tuzo,watu wote walishangilia ikiwemo na mimi.Ni kweli jamaa anagusa idadi kubwa ya watu kutokana na uasili wake na maudhui katika mashairi yake.

WIMBO MMOJA WA BONGO FLEVA ULIOIMBWA KWA KIINGEREZA MAHADHI YA HIP HOP

Ijumaa mchana nlikua naskiliza ile peoples station,ghafla kuna mtangazaji waga ana sauti nzuri,lakini kuanzia presenting yake akiwa kwenye segment yake ni full uzungu.Sasa yeye ameshirikiana na wengine wawili wameimba hiyo Bongo fleva ya kidhungu.Binafsi sikuipenda,ingekua kaimba Snoop dog labda ingemake sense lakini ni kichekesho nyimbo kuwekwa kwenye Category ya bongo fleva halafu ni uzungu uzungu mwanzo mwisho.

Kwa kuwatazamisha tu,waangalie watu kama Lady jay dee,20%,lina wa Tht na wengine ambao wamepata tuzo ukimwondoa mpoki,Ni uzungu uzungu au ni kusimamia uhalisia wa nyImbo na juhudi binafsi ndo wamefika walikofika?

TUSOME,TUANDIKE ILA MAPOZI TUMWACHIE TASHA MWENYEWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Una maana Mrembo Jeidii na asilimia 20%. Maana Lady Jay Dee na 20% ni udhungu Mtupu! Ukimpenda wapenda tu, hata kiama ni Chongo!, "Beauty is in the eyes of a beer holder!"

    ReplyDelete
  2. NAAM ULICHOSEMA NA SAWA KABISA WATANZANIA LUGHA YETU NI KISWAHILI NA UTAMADUNI WETU LAZIMA UENZIWE SI KUKOPI....SANAA HAISEMI HIVYO.....NA MAENDELEO SI KIZUNGU......

    ReplyDelete
  3. 20% X 5 AWARDS = 100%

    ReplyDelete
  4. tunawaomba wanamuziki waimbe kwa lugha fasaha ya kiswahili nina imani tutazipenda na waweke manjonjo wanayoyajua wao ila wasiweke kizungu hatukipendi na maneno yasiyo na maadili pia wajitahidi tunapenda kuburudika ndo hivyo burudani gharama angalia nyimbo za 20% hakuna uzungu Jamani!!!!!nilitamani na banana zorro angepata hata moja ningefurahi zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...