Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mh. Jenista Mhagama (kulia) akiongea kwenye mkutano wa wadau akiwa meza kuu na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara. Kamati ilikutana jijini Dar es Salaam na uongozi wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo kwa dhumuni la kufahamiana na kubadilishana mawazo kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akitoa taarifa ya Wizara yake
Bw. Raphael Hokororo, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, akichangia hoja katika mkutano huo.
Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi akichangia mada katika mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo wakifuatilia mambo kadhaa yaliyokuwa yakiwasilishwa katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma ya Jamii Mh. Livingston Lusinde a.k.a Kibajaj akichangia. Picha zote na mdau Mwanakombo Jumaa wa Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Picha ya pili na ya tano naona mshikaji anameditate!!! Akitoka hapo anadai posho ya kikao kwa nguvu kweli... Mimi binafsi nataka yule mshikaji arudishe posho aliyopewa kuhudhuria hiki kikao. Bongo tambarare!!

    Mdau, Boston, U.S.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...