pole na kazi nyingi na salaam toka Njombe.
Jumamosi 12/03/2011 Laxmi Darts Club ya Tukuyu ilifanya ziara ya mchezo wa kirafiki mjini Njombe na kukutana na Club kongwe ya darts nchini iliyoanzishwa miaka ya 1950 – Kibena Club. Mchezo ulikutanisha kina mama na kina baba kwa pande zote mbili.
Wanyambala wa Tukuyu walionesha mchezo wa hali ya juu kwa kuwagalagaza wenyeji wao ambao wengi wao walikuwa raia wa kigeni kwa ushindi wa jumla wa mabao 15 kwa 3
Mchezaji Hendrick wa Kibena Club na Issa wa Laxmi ndiyo walikuwa nyota kwa pande zote mbili kwa kina baba na Mrs. Hendrick wa Kibena Club ndiye alikuwa nyota na mshindi wa Jumla kwa kina mama.
Hendrick wa Kibena akitoa ngoma kimiani
Mnyambala Issa wa Laxmi akitoa ngoma kimiani
Kibena ilibidi kuita majeshi ya akiba. Hapa Mzee mzima
akijaribu kuokoa jahazi isizame bila mafanikio.
Kina mama wakiwa ulingoni.... haikuwa kazi ndogo
Washindi wa pande zote mbili katika picha ya
pamoja wakisherehekea zawadi zao.
Moja ya mabango ndani ya Kibena Darts Club
yakionesha washindi wa miaka hiyooo ya 1950
Habari hii na picha na Mjomba Juma
wa Globu ya Jamii - Tukuyu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...