Home
Unlabelled
lone picketeering against libya attacks in dar es salaam today
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kwa kweli WaTz tunachekesha sana. Tunapoteza muda kwa mambo yasiyo na tija katika maisha yetu kisa eti hawa walibya ni watu wa dini yetu. Mngejua wenyewe walibya wanafurahia hayo majeshi ya magharibi ili ymngoe kadafi msingejitia kimbelembele. Nadhani wewe wala si kimbelembele unajitia bali kinyumanyuma. Bango kama hilo ungelitumia kuijulisha serikali yetu matatizo yanayotukabili wewe unaonea huruma wenzio wasio na hata chembe ya huruma kwako. Jionee aibu mwenyewe
ReplyDeleteHeee, Huyu Juha. katoka wapi?jamaa nahisi ni Bingwa wa reverse,huu ni ujinga usio kuwa na maana,yaani siamini kama bado kuna watu wapumbavu kama hawa,shame on you,eti ana ingiza udini kwenye siasa,kwanza walibya wakimuona Mamluuki kama huyu wana mkata kata,mpumbavu kabisa.. Angalieni wapumbavu kama hawa ndio wale wana itwa mercenaries kule Libya
ReplyDeleteToronto
Canada
Huyu bwana nadhani ana mapungufu kichwani,japo simshangai sana kwani hata serikali yetu bado haijatoa msimamo wake kuhusu Libya,nadhani serikali inaangalia upepo wa nani anaelekea kushinda ndipo itoe tamko la kuunga mkono ,kwa sasa wanaogopa asije akawa mshindi Gadafi wakati wametoa tamko la kumlaani,wakakosa kujengewa misikiti na Gadafi,hiyo ndiyo siasa ya nje ya Tanzania.
ReplyDeleteMdau hapo juu, inawezekana kabisa kumondoa Ghadaffi kwa kwa majadiliano, sio kama walivyofanya hao traitors, jamaa kwenye picha yupo sahihi kabisa, tunahitaji watu kama hawa ndani ya Afrika. Afrika 4 African's. Na Ghadaffi THE TRUE AFRICAN
ReplyDeleteNi uhuru wa kujieleza, na matazamo wa mtu. Hata mdau wa kwanza pia umesukumwa na utashi wako wa kiimani au kimtazamo, kuelezea hisia zako. Ikiwa fikra hizo zina tija kwako au kwa jamii yetu, pia ni mtazamo wako. Kudai haki, lazima kuendane na kutenda haki.
ReplyDeleteYour concepts is correct young man, only you need to get your spellings correct and perhaps your sentences corrected so that your message is clear. Tunaishi ndani ya jamii ya kitaifa na kimataifa, usiji sahau, kesho inaweza kuwa jirani yetu na kesho kutwa kwetu, wamarikani wajitia ubabe sana, mbona wasiwawekee vikwazo vya angaa na kisha kuwa shikisha adabu somalia ambao wanauwana kila leo, na hivyo kusababisha wakimbizi tele wengine wapo TZ, au kwa vile somalia haina mafuta? Fikirini kabla kutoa maoni...
ReplyDeleteHuyu maskini ni njaa tu. amekosa kazi ya kufanya anajitia mjahidina. Hebu cheki lemba hilo.....Unawaahibisha wenzio.
ReplyDeleteHii inabidi ipelekwe kule engrish.com
ReplyDeletekweli kabisa mdau hapo juu umemaliza yote,tujisikitikie sisi wenyewe,kwanza kwa Uislam gani?!
ReplyDeleteww mtoa maoni wa juu hapo ss km hvyo kwann wakatae maongezi hayo majeshi wavamizi washaitwa wakae chini wao hawataki wanataka kuattack tu huoni km raia wasioa na hatia wana kufa , na km marekani na washirika wake watu wa kutaka democracy kwann wasiende ivory coast kwanza wakati jamaa kashindwa uraisi na kagoma kuachia nafasi kwann wasimtoe yule ... na umesema tusiwasupport eti sio kwa sababu dini yetu ndio tuwasupport kuwa na utu ndugu acha chuki binafsi za kidini au rangi leo kwa mwenzako kesho kwako ... fikiria sna hli na maneno yako one day yatakurudia na ww
ReplyDeleteMdau hapo sioni kama una haki ya kumshambulia jamaa hapo, ana haki ya kuexpress maoni yake kama wewe ulivyofanya hapa kwenye blog. Pili,ukiacha suala la dini,leo hii tumesahau jinsi gani Libya wamekuwa wakiisaidia Tanzania kila mara,hapa juzi tu kwenye mafuriko ya Kilosa wamejitolea,ukiacha huko nyuma walimwaga Magari kwa viongozi ya kubeba Viongozi wenu.Nadhani ni yale yale aliyosema Nelson Mandera kuwakatilia Wamarekani na Wengine kuto mtambua Gadaffi na Libya kwa ujumla. Sio kwa Tanzania tu Libya wamekuwa wanamisaada mingi kwa nchi zote za Africa. Sio vibaya kama ukireserve your comment. Kaka hapo hakuna DINI, hayo ni MAFUTA TU. Mbona hawaendi Yemen, Kuwait, Saudia, bila kusahau Zimbabwe. Bora tunyamaze. Na hao hao mapilisi wa Dunia hawana majibu kuhusu haya kila wanapoulizwa kwanini hawaendi na huko kupiga au wanaukufa huko sio watu na hawana Roho.
ReplyDeleteKakodiwa huyo.
ReplyDeleteHuoni kaziba uso kwa aibu.
Hahahaha sasa mtu kama huyu , ukisha mtengeneza hawezi vaa bomu na kuuua wengine wasio na hatia ?, hapo tuu kasimama siku nzima ana hilo bango sijui analipwa na nani, ona alivyo jificha uso kwa hicho kitambaa ka Ki Alqaida , nafsi inamsuta ndio maana ana jificha , ana bahati ningetumai lugha chafu kwake, maan aTanzania tunamatatizo mengi na jitu bado lina jipendekeza kwa matatizo ya nchi nyingine tena asiyo yaelewa , nyambafu!
ReplyDeleteMtoa maoni hapo juu! hakuna alokatazwa kuonesha hisia zake pale anapoguswa na jambo fulani! kwani wanaouliwa kule ni binadamu kama alivo yeye! na nadhani ni uhuru wa kila mwanadamu kusema au kukemea pale anapoona jambo ambalo linatendwa kinyume na haki za binadamu, imma awe wa dini yake au nyingine! so naona ana haki ya kuonesha hisia zake ...Mungu ibariki Dunia na watu wake ....
ReplyDeleteWalibya watakufa kwa mafuta yao. Wajinga hapa wanachekelea huku na wao ndugu zao wakifa kwa maradhi na umaskini. Adui ni yuleyule hata kama ana wanao muabudu miongoni mwetu! matusi na dharau si hulka za dini yeoye, ni udhaifu tu!
ReplyDeleteHuyu mbongo ana haki kabisa ya kueleza maoni yake. ninampongeza kwa hilo. Ila tu hicho Kiinglish kinatosha kubaini uwelewa wake wa mambo ya dunia-mtandawazi. Walibya (Waislamu wa Libya) ndio walioingia mitaani kudai mwisho wa utawala wa kidhalimu wa Gadaffi (mwislamu mwenzao) kama ilivyokuwa kwa Waislamu wa Tunisia na Misri (walifanikiwa kuwang'oa madikteata), na kama inavyoendelea katika nchi nyingine za Kiislamu za Mashariki ya kati. Waislamu hawa walipoandamana ili kumshinikiza Gadaffi aondoke, yeye akawageuzia kipigo na kuanza kuwachinja kama kuku! 'Western" wameingia kuepusha mauaji ya kimbari. Wasingeingilia, bado watu kama nyie mgesema mbona hawaingilii kwa sababu wanaochinjwa ni waislamu!!!! Hiyo ndio dunia-mtadawazi.
ReplyDeleteHicho Kiinglishi hatari mno, mngeandika kiarabu tu :)
ReplyDeleteUJUMBE WANGU KWA MWENYE BANGO. Mimi nina mtizamo tofauti. Chanzo cha vita ni kukosekana kwa demokrasia Libya. Kwa wale ambao mlifuatilia kwa karibu tangu mwanzo wa mgogoro huu, mtakumbuka mtoto wa Gaddafi akikiri kuwepo kwa tatizo la demokrasia, na kwamba alikuwa anamshauri baba yake kufungua milango ya demokrasia. Kuna makundi ambayo walikuwa hawaridhiki na hawanufaiki na utajiri wa Libya. Na pia vyombo vya usalama (usalama wa taifa) vilikuwa vinahusishwa na kupotea kwa watu waliokuwa wanaonyesha dalili ya kupinga utawala wa Gaddafi. Mataifa ya Magharibi yameingilia kati baada ya; (1) kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Libya, (2) baada ya Gadafi kuanza kutumia ndege za kijeshi kushambulia waasi na miji ambayo inapinga utawala wake, (3) Baada ya Gadaffi kugoma kung'oka katika utawala kuacha demokrasia ichukue mkondo wake. Si hivyo tu. Libya ina rasilimali ya mafuta. Na lazima tukubali kwamba rasilimali hiyo ingawa ni ya Libya, lakini inagusa maisha ya kila binadamu tukiwemo mimi na wewe. Panapotokea matatizo ya kivita sehemu zenye rasilimali hiyo bei ya mafuta hupanda, na kila mmoja wetu ulimwenguni huathirika. Hizi ndizo sababu za msingi za mataifa ya magharibi kuamua kuingilia kati mgogoro wa Libya. Lakini pia Uingereza ina maslahi makubwa Libya kwa kuwa kampuni lake la BP lina visima na hisa kubwa kwenye rasilimali za mafuta Libya. Hivyo athari kwa upande wa ajira pamoja na mapato yatokanayo na hisa vitakuwa vimeathirika sana. Vilevile ukichukulia kwamba kampuni hili la BP lilipata matatizo makubwa ya kuchafua Ghuba ya Mexico mwaka jana baada ya mfuta kuvuja, athari kwa kampuni na hatimaye kwa Uingereza zinaendelea kuwa kubwa kiuchumi. Uingereza isingependelea kuwepo kwa vita Libya kwani vinaathari kubwa kiuchumi kwa Uingereza.
ReplyDeleteSasa jamani sisi watanzania tunachotaka ni nini???Watu wakiangalia mpira wa ULAYA mnalalamika(VIJANA WA KITANZANIA WANAJIGONGA)kwanini wasisome vitabu au kuzungumzia mambo ya DOWANS,LIBYA na kadhalika.Sasa mwenzetu amekuja na mtazamo wake tofauti kuhusu LIBYA tunaanza kumpiga madongo na kumshambulia.Sasa tufanye nini katika hii dunia ili tuwe sawa???Kweli mpira wa ULAYA upo juu.MPIRA wa ULAYA oyeeeeeeeeee
ReplyDeleteSasa mbona hakutengeneza bango wakati Gadafi alivyokua anaua watu wake? Au muislamu kwa muislamu kuuana ni halali? Inabidi tueleimike kwanza kabla ya kukimbilia mambo tusiyo yaweza. Matatizo ya kusikiliza station moja tu (State) bila kujua both sides of the story ndio haya. NI haki yake kujieleza lakini ajue ukweli kwanza kabla hajaonekana mjinga...
ReplyDeleteWalibya hapo bongo mbona hawajatembea kupinga haya? Kwani hatuna raia wa Lybia nchini kwetu? Ya kwetu yanatushinda tunakimbilia ya jirani...
sijui nianzie wapi ndugu yangu michu! watu wanaongea kwenye kibiriti kwa sababu naona hata dunia hawajui inakwenda wapi!? bussiness now! tayari ipo kwenye flow, muda mrefu walikua wanapataka ila kuingia mipango ilikuwa inafanywa pale libya sasa sasa mambo ok, wametafutwa pupets' mambo yameanza!! mie nasema hivi, hazina hiyo walopewa nchi nyingi za kiarabu ndio tatizo hapo, kama ni haki basi wangeenda china watu walipouawa uwanjani kwa greda tena wakidai haki zao hawakuwa na silaha, ivory coast rais mpka leo hataki kutoka na anatumia dola kuuwa watu wasio na silaha, sasa libya watu wameshika silaha then hawataki mazungumzo tena ghadf kawaita waje wazungumze, lakin seems hao watu they dont have strong reason! eti only amekaa miaka mingi, ndio mie naona maana hawataki kutokea kuzungumz na ghadaf , hicho ni kivuli cha white man, kama wapumbavu wengine wasio jua. swala la imani naomba waliache kama lilivyo maana hata hao wanaoshambulia libya sio waislam sasa kuna ubaya gani muislam kulizungumzia jambo la muislam mwenzake? hata hapo chadema anatetewa na chadema mwenzake, ccm na ccm mwenzake, sasa suala la kiimani mtu kama alijui bora akae kimya kabisa sio kutoa matusi humu kwenye web. kumbuka likitokea kwako hapo home sijui nani wa kuliongeelea hapo maana western wanauwezo kwa lolote wakitaka sijui utasema nini,...........ila kwa allah kidogo hawataweza .sikiliza ndugu yangu hata wewe unaye ongea utumbo msaada wa ghadaf ushakula kama ujui uliza viongozi wako hapo home ndio utajua, lakin jua kwamba thamani inadondoka kwa mwafrika, hao white man busara nadhan ingeitisha mkutano kwa pande zote mbili ili mapatano yafanyike na ikishindikana basi wagawane kama mataifa mengine, mfano sudan, korea ,kwa mifano north na south, east na west , then wao ndio waende kusimamia hayo mapatano sio watu wanaitwa waende wakasikilzwe hawataki tena na silaha mkononi!? then mnasema wanauliwa anayeonewa anakuwa na silaha?? je umemsikliza putin wa urusi kasema nini ? kuhusu hayo mambo? au watz. tunaongea tu! kwa sababu mtandao upo unaandika tu maoni yako, la hasha basi mengine ukatazwi il tu kuwa kidogo mchunguzi yakinifu wa mambo kidog ndio utoe comment zako!!!
ReplyDeletemdau jap.
Nyie mnaosema mafuta sijui mnafuaatilia haya...Ukweli ni kuwa Marekani hainunui mafuta kutoka Lybia. Sijui france na nchi za huko ulaya lakini USA hawanunui kutoka kwalo. Na hii issue ilikua kwenye CNN juzi ndio wakatoa data zote. Nchi za uwazi hazifichi kitu ndio labda ku nna interest nyingine lakini Obama hakutaka kabisa kuijiingiza huku ila wakamwambia utalaumiwa kama Cliton alivyolaumiwa Rwanda...Sasa tutasikia J3 ataongea nini...lakini tuandike pale kwenye ulweli na ya uwongo tuache pembeni huyu mtu alisema usilamu mbona haoo watu ni waislamu wenyewe kwa wenyewe wameanza kupigana na huyu mwanamke leo aliyevamia hotel wakati waandishi wa habari wakiwa wanaelezwa na Govt kuwa kila kitu ni shwari yeye akasema wame mrape mara wamemkimbiza na kumficha? Je huo ni uuungwana....Watu wanadai haki zao na hao watu wakisha pewa haki zao wasije wakataka haki kwenye siasa tu na kusahau social...manake huko kwao wanawake ni low class
ReplyDelete