Mwenyekiti wa Baraza la walaji/watumiaji kutoka SUMATRA Bw. Guliadi Ngewe akitoa ufafanuzi kwa waadishi wa habari juu ya kupanda kwa viwango vya nauli za usafiri (daladala) katika jijini la Dar es salaam na mikoa mingine. Amefafanua kuwa ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa gharama za mafuta duniani na ongezeko la vitendo vya uharamia katika bahari ya Hindi huku akibainisha kuwa jiji la Dar es salaam lina waendesha huduma za usafirishaji 3500 na tayari mapendekezo ya kuwa na makampuni ya uendeshaji wa shughuli za usafirishaji yameshawasilishwa serikalini.
Mwenyekiti wa Jukwaa la mabaraza ya watumiaji/walaji Tanzania (TFC) Eng.Prof. Jamidu Katima (kushoto) akizungumza na wadau wa Jukwaa la mlaji/mtumiaji pamoja na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani 2011 itakayoongozwa na kauli mbiu “ Huduma za Kifedha ni Stahiki ya watumiaji” yenye lengo la kusisitiza uwazi, taarifa sahihi, haki na huduma bora za kifedha kwa mtumiaji leo jijini Dar es salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Baraza la watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na TCRA (TCRA –CCC) Bi. Hawa Ng’humbi.
Wadau Baraza la walaji/watumiaji kutoka SUMATRA, EWURA, TCAA, TCRA, NCAC na waandishi wa habari wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa mkutano wa Baraza hilo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...