Mji wa Moshi unasifika si kwa utalii pekee bali pia hata kwa biashara ndogo ndogo. Watasha hawa wamekutwa na kamera yetu maeneo ya chuo cha shirika wakiuza chipsi za mihogo na juisi, bega kwa bega na wauza ndizi mbivu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hawa ni wawekezaji,msiwabugudhi...

    ReplyDelete
  2. Habari Bw. Michuzi, maoni yangu hayahusiani kidogo na mada hii isipokuwa nafuatilia hii globu yetu ya jamii lakini sioni habari kuhusu dawa ya ukimwi ya Mchungaji kutoka Loliondo. Tafadhali kama kuna watu wenye habari/picha kutoka huko tutafurahi kuziona hasa kwa sisi ambao tupo Ughaibuni. Mdau kutoka Uingereza

    ReplyDelete
  3. tuangalie kwanza je ni wazawa? basi wauze kama ni hiyvo kwa maana tanzania ni nchi ya mchanganyiko wa watu. Kama tunaishi kwa kibali basi ni upuzi mtupu kwa serekali kuachia upuzi namna hii.Kazi zetu hizo sisi wazawa kulisha familia zetu. Wakachugue benefits makwao za wasubiri.

    ReplyDelete
  4. HAWA WATAKUWA WANAFANYA DOCUMENTARY YA MAISHA KAMA VILE LAZY KIDS WANAONESHA SANA VIPINDI HIVI USA. WANAENDA KUTAMBUWA WATU WANAVYOPATA TABU ALAFU WAO HAWATAKI KUFANYA KAZI WANALALA TU, KULALA SAA TISA USIKU KUAMKA SAA KUMI JIONI... NA HIZI TABIA VIJANA WETU HAPA TANZANIA PIA WANAZO. ILA KWA KUTAKAK UNUNULIWA IPHONE KIBOKO. MZEE JAMES.

    ReplyDelete
  5. he he he he he hivi hao watasha work permit wanayo maana wanachukua ajira za wazaliwa!!! wajasilimaliaa hao wanasevu nauli ya kurudi kwao.

    mdau aracuga

    ReplyDelete
  6. Waangaliwe kama wana work permit, kama hawana waanze haraka sana. Tanzania ni nchi yetu hatujawaomba waje watufundishe umachinga. Au wana lao wanataka nini! wasije wanauza ivo alafu wanajipiga picha wakija huku wanaziuza kwenye tv zao na kujipatia pesa, wachunguzwe hao, haiingii akilini kukuta mtu mweupe anakuwa na ujasiri ivo, labda kama wachina.

    ReplyDelete
  7. Nyie mnaosema work permit bla bla bla basi na nyie muache kuzamia kwenye nchi zao na kuchukua benefits..

    ReplyDelete
  8. Hawa ni watafiti wa maisha ya jamii katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara yaani "Participant Observer"

    ReplyDelete
  9. Hahaha lol.. Hawa ni wahongo,hapo mnapigwa mchanga wa macho,nawajua sana wazungu wanatabia ya kujifanya,ukweli hapo ni wana record documentary tunakuja kuona kwenye youtube,TLC,na Travel channell, im telling you, hawa wako na agenda yao hapo... Mambo ya work permit hacha kuwa conservative Bro,ni watanzania wangapi wanafanya Kazi huku North America Bila vibali?? Give them Papers then... Hahahaha

    John

    Toronto, Canada

    ReplyDelete
  10. hao hata sio wamachinga kama wengi wanavofikiri,,naungana na mdau hapo juu watakua wanafanya documentary ya maisha. hapo wanakusanya data2!

    ReplyDelete
  11. WAKISHA MALIZA KUKUSANYA DATAS ZINAPELKWA NATINAL GEOGRAPH. TRAVEL CHANNEL, ALAFU HUKO WANATUANGALIA MAISHA YETU WENYEWE WAFRICA TUNAVYOISHI, ARAFU WANAPENDA HAO HIZO CHANNEL, ZINALIPIWA KWA BEI WACHA, WANA MAKE MONEY, PASIPO SISI WENYEWE KUJIJUA KAMA WENZETU WAKO KWENYE BUSSINES KWELI AKILI MALI

    ReplyDelete
  12. Wameoa. Nasikia wameisha Work Permit na cha Kijani, ila uraia ndo bado.

    ReplyDelete
  13. hao watakuwa watafiti wa masuala ya jamii na maendeleo, mamlaka za moshi fuatilieni muone kama wana 'ethical clearance' na kama wamefuata maadili yote ya kitafiti na kuhakikiwa na IRBs/Ethics committees. pia zijulikane taasisi/universities wanazohusiana nazo. ikibainika hawajafuata taratibu za kitafiti (mfano: kama wamejitambulisha kama wafanyabiashara/wawekezaj wakat ni watafiti kwa hiyo hakuna informed consent) basi waondolewe mara moja na kama wamepublish paper zozote kutokana na hiyo utafiti zifutwe na wasipewe hizo PhD wanazofanyia kazi, wawadisco kabisa mana hii ni serious protocol violation.

    j, dar

    ReplyDelete
  14. Watanzania tuache USHAMBA. Mmeona weupe basi imekuwa keleele!. Je na wao weupe wakituona sisi tusio weupe huku kwao waseme haya haya juu yetu? Tanzania ni ya wote waishio ndani yake, weusi, weupe, wachina, wahindi, waasia, n.k. Hii ni globalisation era bwana. Mbona wao hawasemi hawataki mkenya mweusi awe raisi marekani? U-rangi unatusumbua wabongo.

    ReplyDelete
  15. wabongo kazi zetu kusema wenzetu tu kuwa ni wabaguzi wa rangi lakini ukifatilia kwa makini utaona kuwa wabongo ndio wabaguzi wakubwa wa rangi duniani

    kama huamini angalia kila kitu kinachofanywa na mzungu utasikia aah mzungu kama hivi kafanya vile mbona wazungu hawaongelei kuwa mtu mweusi kafanya hivi au vile

    utakuta mbongo kama ameowa mzungu lazima atapewa jina nani yule mwenye mke mzungu au yule mwenye mke mhindi n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...